Nimefuatilia jinsi TBC1 ilivyofanya kazi ya kuripoti vikao vya CC na baadaye NEC Dodoma na kugundua kwamba bado TBC1 wanafanya kazi kwa maelekezo/ushabiki wa Lowassa.
Kwanza kwa Dodoma na Dar es Salaam matukio makubwa hurushwa moja kwa moja na zaidi kama yanamhusisha Rais ama tukio lenye mvuto kwa jamii. Kwa vikao vya Dodoma na baada ya NEC kuruhusu waandishi wa habari na TBC1 kurekodi badala ya kurusha live inatia shaka.
Pili baada ya kurekodi, inasikitisha sana sisi tuliokuwamo katika hiyo Press Conference tumeshangazwa na TBC kukatiza alipoishia Chiligati na kutomtoa kabisa Nape alipokua akiwataja moja kwa moja kina Lowassa, Rostam na Chenge.
TBC1 fanyeni kazi, Lowassa hasafishiki na habebeki na hata kama akifanikiwa kuwa kiongozi endeleeni na kazi bila kujali, na kama munamjali Rais ajaye (kama akipata) na kumwacha Rais aliyepo.
Tulidhani baada ya kuondoka Tido itakua yameisha maana Tido alimhoji Pinda na kumpa Lowassa nafasi ya kumalizia ili amfunike, lakini na sasa munaendelea kuonyesha kwamba munaandamwa na kivuli cha Lowassa. Fanyeni kazi acheni unazi wa aibu hasa kwa mafisadi.
Hata kama akifanyaje keshatia doa la damu nguo yake nyeupe wala watanzania hawasahau ng'o. Ingekuwa kipindi kile cha ....Naapa naahidi mbele ya chama mapinduzi nitakurinda mpaka kufaaaaaaaa! hapo tungekuwa na wasiwasi.Nyie msitudanganye hata kidogo. Huu ni mkakati wa mh L kutwaaa uraisi na huu ndio mwanzo wake kujitokeza hadharani
Kakti mawaziri wakuu waliopita watendakazi ni wawili 2, Moringe sokoine na Lowasa, mkibisha sawa, mkikubali sw, EL ni bora mara mia ya JK& Makamba na Mukama as well, katika safu ya wawajibikaji toka 2005 hadi leo ni wachache sn wameonesha uwajibikaji kumkaribia EL lkn mabaya yapo na mazuri pia yapo, si teti ufisadi ila utendaji kazi uliotukuka, nawahakikishia Mukamba ni nothing kwa kichaka cha mafidi kilivyo jipanga,matawi, tukimchukia kiongozi, tumchukie kwa mabaya/ufisadi wake lakini tusiwe na chuki binafsi dhidi yake. Kwa vile EL kachafuka na uchafu wa Richmonduli, sasa ndio imekuwa nongwa?!. Asifanye chochote kwavile ni mchafu hivyo atachafua?!.
Japo mimi sio mtetezi wa EL, ukimuondoa Sokoine, hatujawahi kumpata waziri mkuu mwingine yoyote anayemkaribia hata kwa mbali, lakini kati ya wote, angalau angalau ni EL tuu, sasa ulitaka nani amzungumzie Moringe?!.
Mambo ya EL siku zote nasisitiza 'Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni'!.
hapo umenena Mwanazuoni..mnyongeni haki yake mpeni....kuna mambo EL,kayafanya lakini watu hawayaoni wanaona mabaya yake tu ndo msemo unasema ukitenda mazuri watu wanayasau mabaya tu ndio wanayakumbuka..