barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,375
- 29,732
Habari zenu!
Moja kwa moja ktk mada, nafikiri uongozi wa udart, wanaoendesha mabasi yaendayo haraka (Mwendokasi) yanahitaji kuwa na konda ndani, lengo kubwa la konda sio kukusanya nauli hapa, bali kupanga watu ndani.
Haiwezekani watu mnasubiri mabasi kwa dk kadhaa linakuja basi linaonekana limejaa full kumbe abiria % kubwa wamekushanyana mlangoni ilhali katikati kuna nafasi kubwa tu ambayo kama wangesogea basi abiria wengine wengi tu wangepanda na kuwahi waendako. Kibaya ni pale uliepo nje unawaambia waliomo ndani wasogee ila wankikodolea tu macho bila kusogea ila na wewe ukiingia badala ya kuwasogeza kituo kinachofuata abiria wa nje wanakwambieni segeeni ila na wewe raundi hii unawakodolea tu macho waliopo nje bila kusogea!
Mfumo wetu wa kimaisha umetuathiri sana, bila kusukumwa ni vigumu sana kufanya mambo kwa ufasaha! Tubadilike watanzania ktk vitu vya msingi, tusiwe wa kusukumwa sukumwa tu!!