Kuna udanganyifu kwenye ujazo wa mitungi ya gesi ya kupikia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna udanganyifu kwenye ujazo wa mitungi ya gesi ya kupikia?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by IshaLubuva, Sep 16, 2009.

 1. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2009
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Katika kuitikia wito wa serikali wa kupambana na uharibifu wa mazingira niliamua kuachana na matumizi ya jiko la mkaa na kununua jiko la gesi. Aidha niliamini kuwa gesi itkuwa na gharama nafuu zaidi (wenyewe wauzaji waliniambia kuwa gharama inakuwa kubwa wakati wa kuanza kwa sababu utalazimika kulipia gharama za mtungi) kuliko mkaa. Lakini hali haikuwa kama nilivyotarajia. Gesi ya Mtungi wa kilo 30 ambao hapa Dodoma unagharimu sh. 28,000.00 haikuweza kuhimili matumizi kwa mwezi mzima kwa familia ya watu watatu pekee. Nilinunua gesi tarehe 11/08/2009 na ilipofika tarehe 08/09/2009 mtungi ulikuwa chwee kabisa. Hali hii imenifanya nirudi kwenye matumizi ya mkaa kwani gunia la mkaa ni sh. 10,000.00 ambapo kwa gharama ya mtungi wa kilo 30 naweza kulumbana na muuzaji wa mkaa na kupata gunia tatu ambazo zinaniwezesha kukata zaidi ya miezi miwili.

  1) Ninachojiuliza ni iwapo hii mitungi ya gesi kweli huwa inajazwa kama inavyostahili. Jana niliona tangazo la EWURA wakitoa unyo la udanganyifu kwenye biashara ya gesi ya kupikia

  2) Je mimi kama mteja ninayenunua mtungi nitajuwaje kama mtungi ninaonunua umejaa inavyostahili?

  3) Kwa hali hii itawezekana kweli wananchi kuachana na matumizi ya mkaa ili kuepusha ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na hivyo kupunguza uharibifu wa mazingira?

  4) Serikali iko wapi katika hili, wenzetu Ulaya gesi ni bidhaa ya umma na inapewa ruzuku (kumbukeni mzozo kati ya Urusi na Nchi za Ulaya baada ya gesi ya UUrusi kusimama wakati fulani kupelekwa kwao walivyokuwa wanahaha)
   
 2. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Umeuliza swali la msingi.
  Nimesikia kuna maeneo wanapima kwa mizani, ila sijaona ni wapi wanafanya hivyo.
  Kwa hali ilivyo, ni bora mnunuzi aende kupima mtungi wake kila baada ya kununua. Hii ni sehemu ya kukabiliana na tatizo.

  EWURA wamesemaje? Walieleza udanganyifu unafanywa wapi?
  (Maana kuna wanaouza, wasambazaji, wanaojaza.)

  Niliwahi kusikia kuna mipira ya kuhamisha gesi kupunguzia kwenye mtungi mtupu. Na kwamba hili ni zoezi jepesi.
   
 3. b

  bnhai JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,206
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Duh basi kama na kwenye gesi wameshaanza kugusa hawa jamaa ni hatari. Kuna wakati tunalaumu serikali bure, sisi wananchi ndio tumezidi. Okey sasa hebu ona hao wauzaji wameshapoteza mteja kwa ujanja wa kijinga. Mie nilikuwa na familia ya watu watano na gesi ilikuwa inaenda miezi mitatu
   
 4. Keen

  Keen JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 620
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ishalubuva: Hapo unaponunulia wanapashwa kuwa na mzani na kama una wasiwasi na mzani wao, tafuta sehemu nyingine kapime. Hata hivyo, jaribu kuchunguza pia matumizi yake nyumbani kwako inawezekana vitu vya kuchemsha vimeongezeka baada ya kupatikana njia nyepesi ya kuchemsha-yaani gesi. Imewahi kunitokea pia wakati naanza kutumia gesi zaidi ya miaka 2 iliyopita. wengine walikuwa hawaogi maji ya moto, wakaanza kuoga eti tu kuna gesi!!.
   
 5. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2009
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Bahati mbaya tangazo la EWURA nililiona wakati linamalizikia kwa hivyo sikuweza kupata undani wake.

  Uogaji wa maji ya moto hauko kwa wingi katika familia yangu na ndiyo maana ninahisi huenda kukawa na udanganyifu kwenye hii biashara
   
 6. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2009
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nilikutana na hayo hivi majuzi, wauzaji wakanieleza wazi wao hawana kipimo cha kuhakikisha imejazwa kama inavyostahili. Wakanishauri niachane na mitungi ya zamani ambayo mamlaka husika ipo katika harakati za kuiondoa na ambayo ndio yenye matatizo ya kutokuwa na ujazo kamili. Nikatakiwa ninunue mtungi mpya...hii mipya kwa kati ya laki moja na laki moja na ishirini nikafanya hivyo...I hope...this time sitakutana na hali hiyo
   
 7. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  inawezekana wakadanganya hao either Oryx,mihan etc kwani ndo wajazaji.pia mtuma thread kg 30 kwa 28,000? nadhani ni kg 15 mkuu,mimi natumia kg 15 kwa 1.5-2months nina family ya 4 people! but watch yafuatayo
  1.hakuna leakage katika maungio(gas jar to cooker)
  2.matumizi ya hapo hme (usikute mtu anachnsha maji ya kunywa pekee yanachemshwa for hrs!
  3.mara nyingi may be mnapika maharage/makande/vitu vya kuiva mda mrefu (nakushauri nunua pressure cooker)
  4.unaponunua wawe na mizani ucheki kwa macho yako kuwa ni kweli uzito uanonunua?
  5.wafundishe watoto/wife/hg si kila wanapojisikia kuwasha jiko wanawasha hata maji ya kuoga,sometimes maji ya kufulia Hg anaweza chemsha!
  6. Je jiko lako usikute linatoa/choma gas nyingi sana,tafuta ushauri kwa wauzaji/mafundi kama hakuna control ya gas!
  7.Mkaa ni ghali sana kaka ukizingatia uharibifu wa mazingira kwa wewe na vizazi vijavyo,tumia gas tunayopewa bure ardhini na mungu,haina uharibifu.nunua tena uzingatie matumizi utafurahia!!
   
 8. Keen

  Keen JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 620
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pole mkuu, hayo ndiyo maisha ya bongo.
   
 9. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2013
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,032
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  jamani hizi kampuni za kuhuza gesi ya kupikia. Je ni hipi yenye gesi ya ukweli
   
Loading...