Amani,
Pole kwa kuwa nimepotea kwa mda flani lakini natumaini kwamba yale ambayo ninayo leo yatasaidia kuangaza zaidi juu ya hii topic.
Kwanza tunatakiwa kujiuliza je Bongo Flava ni muziki wa aina gani na Hip Hop ni muziki wa aina gani. Kwangu binafsi bado sijapata maana xhalisi na uasilia wa muziki wa Bongo flava lakini naweza kukuambia husiana na Hip Hop ambayo inafanyika hapa nyumbani Bongo. hii yote ni kutokana na upeo wa mimi.
Muziki wa kizazi kipya hapa Bongo upo wa aina tofauti wenye 'genre' tofauti kwa kila msanii kutoka kivyake jinsi anavyojua yeye. Ukiangalia utaona kwamba kuna makundi mengi ya wanamuziki ambao kwa ujumla wamechukuliwa wanaimba Bongo Flava lakini ni ladha tofauti ndo maana unaona ya kwamba Bongo Flava haina Identity! Hapa inabidi tutaje majina ya wasanii. hebu angalia aina ya muziki ambao anaimba Mr. Blue, Matonya, Proffessor Jay, Dully Sykes, Jay Moe, Adili aka Hisabati, Mansulii, Mapacha, Raha P, Ray C, Mr Nice na wengine woote... Ukimuuliza Mbongo atakuambia hao wote wanaimba Bongo flava lakini wewe kweli inaweza kukujia kichwani kwamba muziki wa Zay B na Ray C, Jay Moe na Matonya ziwe katika 'genre' moja yaani Bongo Flava. Tutakuwa hatuna malengo ya kupata true identity ya Muziki wa Tanzania hapo.
Wanaosema kwamba muziki wowote ambao unaimbwa kwa kiswahili ni Bongo Flava wanahitaji Maombezi kwa kweli. Hawako sawa vichwani...hii ni sawa na kujaribu kusema kwamba vimiminika vyote ni maji! Inawezekana kwamba kwa asilimia ckubwa vitakuwa vinajumuisha maji lakini haviwezi kuwa maji.
Hip Hop ya Bongo ipo katika 'crude stage' na ni kwamba inafanyika kutokana na 'context' ya Bongo. Na hata Hip Hop ya Motoni kwa sasa ni kwamba inafuata nguzo lakini si zote, kwa hiyo hapa Bongo Hip Hop inafanyika na ni Hip Hop ya ukweli na huwezi hata siku moja kuwajumuisha na jamaa wa kubana pua.
Sema kuna tatizo moja husiana na wasanii wa Bongo ambalo linasababisha iwe vigumu kujua kama ni Hip Hop ama Bongo Flava. Hawana msimamo wa ukweli husiana na muziki wanaofanya kwa hiyo unakuta wanahama hama kufuata upepo wakijaribu Muziki ambao unalipa zaidi. Watazame Juma Nature, Solo Thang, Mr. Blue, Dully Sykes na wengine wengi utaona ukweli wa jambo hili. Kutokana na hilo ndo unatokea mkanganyano wa Habari husiana na haya mawili. Watu wanakuwa hawafahamiki kama ni Hip Hop ama Bongo Flava ambayo wanafanya.
Kama unataka tofautisha Hip Hop na bongo Flava inatakiwa uwaangalie watu kama Sugu, Jay Moe, Mapacha, Mansu-Li, Binamu, Fareed Kubanda Nako II Nako, Hisabati na wengine kisha weka watu kama Q. Chief, Mr. Blue, Dully Sykes, Mr. Nice and you will see the difference! To quote one of Tanzania Artist:
"kila mtu anatoa definition yake kuhusiana na bongo flavour,kwa jinsi anavyoelewa yeye!nionavyo,hakuna mahala imeandikwa ama imeagizwa ya kuwa ili mtu awe anafanya hiphop ni lazima afanye nguzo zote 5 za huo utamaduni…kuna mcs,djs,wafanyao michoro (graffiti),wachezaji nk…watu wanaoifanya wanagawana majukumu kulingana na uwezo wa kila mmoja..najua sio kila rapper anafanya hiphop,binafsi natambua nani anafanya hiphop na nani bongo flavour kwa kuchambua contents za sanaa zao,namna ya uandikaji na michano yao….anaweza kuwa anaongelea kitu chochote tu,haijalishi,lakini jinsi anavyokiwakilisha inanisaidia kujua upeo na kundi linalomstahili(japo sijawahi na wala sitarajii kujipa haki ya kuwatenganisha hadharani)"
Na kingine kinachofanya watu washindwe jua Hip Hop ya Bongo ni ipi ni kutokana na Radio station zetu kufanya mambo yao ya kijinga na kukumbatia zaidi wabana pua kama ambavyo wawaita wewe na kuiacha Hip Hop nyuma lakini as always Muziki wa Kweli unatoka!!!
Hip Hop inasimama yenyewe hata kama ni ya hapa bongo ama kwengine na ni kwamba mtu yoyote ambaye anafahamu Hip Hop ukimfikisha hapa bongo na akasikiliza nyimbo za hapa nyumbani atakuchambulia na kuweka Hip Hop kando, wala haitajalisha kama nguzo zote zimefuatwa ama la!!!
Hip Hop Bongo nilisahau wafanya hip Hop Ngumu KIKOSI CHA MIZINGA!
Narudi tena!