Kuna tofauti kati ya Bongo Flava na Hip Hop

AmaniGK

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
1,148
361
Wadau poleni sana na "Joto la Balali" linaloendelea humu ndani.
Kwa wadau wa muziki wa kizazi kipya hebu nitoeni tongo tongo kuhusu Hili suala la Bongo flava na Hip Hop
Wazee ya! wa Hip hop kama Nako 2 Nako,Geez Mabovu,Mapacha,Adili,BLac na wengine wengi wamekua wakisimamia kuwa Hip Hop ni Hip Hop na hakuna uhusiano au ufanano na Bongo flava.

Lakini watangazaji wengi wa redio za huko nyumbani pamoja na wadau wengine wanajumuisha vitu hivi viwili.

Kwa uelewa wetu naomba kupata darsa kuhusu yafuatayo

A:Je nguzo za Hip Hop ni Sawa na zile za Bongo flava
B:Hip Hop ya nyumbani ni sawa na ile ya nchi za ng'ambo kwa misingi ya nguzo zake?
C:Kuna haja ya kuunganisha vitu hivi viwili ili kuunyanyua muziki wa kizazi kipya?

Ni hayo tu wadau naomba kuwasilisha.
Amani
 
Huu mjadala nadhani ni kati ya ile ambayo itanifaa sana...

Kwa kweli kwa hapa Bongo kama utataka kuniambia kwamba Bongo Flava na Hip Hop ni kitu kimoja kwa kweli utakuwa unakosea sana na ni kwamba haya yatakuwa ni matusi kwa Hip Hop ya Bongo. Hip Hop ya bongo haitakuja kuwa Bongo Flava lakini kuna wasanii wa Bongo flava wengi wametoka katika Hip hop ya Bongo na kuingia huko wakisaka maslahi bora zaidi.

Ukitaka tuendelee salama katika hili usijaribu ongelea watangazaji wa Redio za bongo. Ni wachache mno kati yao wanajua muziki (Sidhani kama wanafika 5%) na hata wanaoujua wameishia kuleweshwa na sifa za kusikika redioni na kutoka kabisa on the right track.

Well unapoongelea nguzo za Hip na ukasema zinafanana na Nguzo za Bongo Flava utakuwa unaleta masikhara. Kwanza ulikuwa watakiwa kutufahamisha hapa nguzo za Bongo Flava ambazo waziongelea ni Zipi? Muziki wa hapa nyumbani woote iwe ni bongo Flava ama Hip Hop ni ule ambao tunataraji ya kwamba utawa na maudhui, na ambao utaweza elimisha jamii ya Tz kwa namna moja ama nyengine, lakini jinsi ambavyo Hip Hop inawakilisha Ujumbe ni tofauti kabisa na Bongo Flava.

Pia ifahamike kwamba katika Muziki wa Kizazi kipya wa Tanzania Hip Hop ilianza kuibuka mwanzoni mwa miaka ya Tisini na waasisi wa kwanza kabisa akina Saleh Jabir, 2 Proud (Kwa Sasa Sugu), KU Crew na wengine wengi sana. Miaka ya 2000 ndipo imetokea diversion kutoka katika Hip Hop na kuingia hii aina mpya ya muziki ambao nia na madhumuni ya wale ambao wanafanya ni kukubalika haraka na kutengeneza pesa. hich they trully have achieved as most of hip hop Artist bado wanapambana na ukali wa maisha. Wengi wa Wasanii wa Hip Hop wameishia kupata Respect (Heshima).

Kuhusiana na Hip ya nyumbani na ile ya nchi za nje kwa kweli haziko sawa. Kitu ambacho wasanii wa Hip Hop hapa Tanzania wanajaribu kukifanya ni kwamba wanachukua Hip Hop ya nje ambako ndo Chimbuko lake na kujaribu igeuza ili iweze kukubalika katika jamii ya Watanzania. Kwa misingi ya Nguzo utaona kwamba zile Nguzo za Hip Hop ya Nje wasanii wa Hapa Bongo wamezikumbatia lakini kuna vitu vingine ambavyo vimeongezeka ama kupungua katika hayo ili kuhakikisha ya kwamba Hip Hop hiyo inakubalika katika Jamii ya Watanzania.

Mwisho ni kwamba xhakuna haja ya kuunganisha Hip Hop na Bongo Flava ili kuinua mziki wa Tanzania. Hili jambo halihitajiki kabisa. Kama ni kunyanyua muziki wa kizazi kipya nna uhakika kwamba the Utambulisho wa Muziki wa Kizazi Kipya wa Bongo utatokana na Hizo aina mbili za Muziki hapa bongo i.e. Bongo Flava na Hip Hop!

Ntarudi Tena.
 
Muzee Mzozo.
Asante kwa kunipoatia darasa na japo kunifungua macho kidogo.
Kwa upande wangu mpaka sasa sijatake side yoyote katika mjadala huu.
Isipokua ni vyema iwapo tukaonesha ni wapi Bongo Flava inapotengana na Hip Hop (Dermacation line).Hii ni kuwa tu wapo school of thought wasemao Muziki wowote wa kizazi kipya uimbwao kwa kiswahili ni Bongo flava.Kwa maana hii,Hip Hop imetumbukizwa ndani ya Hili kundi

Nafahamu unajua HIp ina nguzo kama Deejaying,MC,B-Boy na kadhalika.Swali langu ni kuwa Hip Hop ya Bongo imebeba nguzo hizi? na kama haijazibeba kwa nini tusiwajumuishe na wabana pua wa bongo flava
 
Amani,

Pole kwa kuwa nimepotea kwa mda flani lakini natumaini kwamba yale ambayo ninayo leo yatasaidia kuangaza zaidi juu ya hii topic.

Kwanza tunatakiwa kujiuliza je Bongo Flava ni muziki wa aina gani na Hip Hop ni muziki wa aina gani. Kwangu binafsi bado sijapata maana xhalisi na uasilia wa muziki wa Bongo flava lakini naweza kukuambia husiana na Hip Hop ambayo inafanyika hapa nyumbani Bongo. hii yote ni kutokana na upeo wa mimi.

Muziki wa kizazi kipya hapa Bongo upo wa aina tofauti wenye 'genre' tofauti kwa kila msanii kutoka kivyake jinsi anavyojua yeye. Ukiangalia utaona kwamba kuna makundi mengi ya wanamuziki ambao kwa ujumla wamechukuliwa wanaimba Bongo Flava lakini ni ladha tofauti ndo maana unaona ya kwamba Bongo Flava haina Identity! Hapa inabidi tutaje majina ya wasanii. hebu angalia aina ya muziki ambao anaimba Mr. Blue, Matonya, Proffessor Jay, Dully Sykes, Jay Moe, Adili aka Hisabati, Mansulii, Mapacha, Raha P, Ray C, Mr Nice na wengine woote... Ukimuuliza Mbongo atakuambia hao wote wanaimba Bongo flava lakini wewe kweli inaweza kukujia kichwani kwamba muziki wa Zay B na Ray C, Jay Moe na Matonya ziwe katika 'genre' moja yaani Bongo Flava. Tutakuwa hatuna malengo ya kupata true identity ya Muziki wa Tanzania hapo.

Wanaosema kwamba muziki wowote ambao unaimbwa kwa kiswahili ni Bongo Flava wanahitaji Maombezi kwa kweli. Hawako sawa vichwani...hii ni sawa na kujaribu kusema kwamba vimiminika vyote ni maji! Inawezekana kwamba kwa asilimia ckubwa vitakuwa vinajumuisha maji lakini haviwezi kuwa maji.

Hip Hop ya Bongo ipo katika 'crude stage' na ni kwamba inafanyika kutokana na 'context' ya Bongo. Na hata Hip Hop ya Motoni kwa sasa ni kwamba inafuata nguzo lakini si zote, kwa hiyo hapa Bongo Hip Hop inafanyika na ni Hip Hop ya ukweli na huwezi hata siku moja kuwajumuisha na jamaa wa kubana pua.

Sema kuna tatizo moja husiana na wasanii wa Bongo ambalo linasababisha iwe vigumu kujua kama ni Hip Hop ama Bongo Flava. Hawana msimamo wa ukweli husiana na muziki wanaofanya kwa hiyo unakuta wanahama hama kufuata upepo wakijaribu Muziki ambao unalipa zaidi. Watazame Juma Nature, Solo Thang, Mr. Blue, Dully Sykes na wengine wengi utaona ukweli wa jambo hili. Kutokana na hilo ndo unatokea mkanganyano wa Habari husiana na haya mawili. Watu wanakuwa hawafahamiki kama ni Hip Hop ama Bongo Flava ambayo wanafanya.

Kama unataka tofautisha Hip Hop na bongo Flava inatakiwa uwaangalie watu kama Sugu, Jay Moe, Mapacha, Mansu-Li, Binamu, Fareed Kubanda Nako II Nako, Hisabati na wengine kisha weka watu kama Q. Chief, Mr. Blue, Dully Sykes, Mr. Nice and you will see the difference! To quote one of Tanzania Artist:

"kila mtu anatoa definition yake kuhusiana na bongo flavour,kwa jinsi anavyoelewa yeye!nionavyo,hakuna mahala imeandikwa ama imeagizwa ya kuwa ili mtu awe anafanya hiphop ni lazima afanye nguzo zote 5 za huo utamaduni…kuna mcs,djs,wafanyao michoro (graffiti),wachezaji nk…watu wanaoifanya wanagawana majukumu kulingana na uwezo wa kila mmoja..najua sio kila rapper anafanya hiphop,binafsi natambua nani anafanya hiphop na nani bongo flavour kwa kuchambua contents za sanaa zao,namna ya uandikaji na michano yao….anaweza kuwa anaongelea kitu chochote tu,haijalishi,lakini jinsi anavyokiwakilisha inanisaidia kujua upeo na kundi linalomstahili(japo sijawahi na wala sitarajii kujipa haki ya kuwatenganisha hadharani)"

Na kingine kinachofanya watu washindwe jua Hip Hop ya Bongo ni ipi ni kutokana na Radio station zetu kufanya mambo yao ya kijinga na kukumbatia zaidi wabana pua kama ambavyo wawaita wewe na kuiacha Hip Hop nyuma lakini as always Muziki wa Kweli unatoka!!!

Hip Hop inasimama yenyewe hata kama ni ya hapa bongo ama kwengine na ni kwamba mtu yoyote ambaye anafahamu Hip Hop ukimfikisha hapa bongo na akasikiliza nyimbo za hapa nyumbani atakuchambulia na kuweka Hip Hop kando, wala haitajalisha kama nguzo zote zimefuatwa ama la!!!

Hip Hop Bongo nilisahau wafanya hip Hop Ngumu KIKOSI CHA MIZINGA!

Narudi tena!
 
Amani GK,

Nilikuwa najaribu ongea na wadau wakuu wa Sekta hii ya Muziki wa Bongo na naomba nisubmit Majibu ya Joseph Mbilinyi a.k.a. Sugu ambaye ni mmoja wa Waasisi wa Muziki wa Kizazi Kipya hapa Nyumbani.

"ebwana ndio...wacha nikupe mtazamo wangu katika hili...
ki ukweli mzee bongoflava ni jina lililobuniwa kutambulisha muziki wa rap/hiphop ya bongo ambao ulikuwa hauna utambulisho zaidi ya kuiga kila kitu kutoka hiphop ya mtoni.ikiwemo kurap kwa english ya lafudhi ya kimarekani...
tatizo ni kuwa muziki huo ulipopata umaarufu na kukubalika....baadhi ya wadau kwa kutumia nguvu ya media zao wakaamua kupotosha maana ya bongoflava kwa kuingiza aina nyingine za miziki na kuziita bongoflava wakati ukiskiliza unaskia kabisa kuwa hizo aidha ni zouk,rhumba n.k...
ushahidi mmoja kuwa neno bongoflava linahusiana na rap/hiphop ni kuwa huwezi kukuta neno 'flava' likitumika kwenye aina nyingine yoyote ya muziki zaidi ya hiphop and r n b...so bongoflava maana yake ni flava za bongo...ambazo zinatakiwa zipatikane kwenye rap/hiphop na r n b tu....coz u dont get a 'flava' in taarab,rhumba,injili,rock n roll,jazz etc etc...
kumbuka sio mara ya kwanza kwa hiphop ya sehemu fulani ya dunia kuwa na utambulisho wake kaka...dr dre alianzisha na kuiwakilisha ipasavyo g-funk kwa sapoti ya wasanii kibao wa westcoast...master p naye alikuja na utambulisho wake na dirtysouth style huko louisiana na hatimaye lil' jon na washkaji zake wakaja na style yao ya hiphop waliyoiita crunk!!!hata senegal wana senerap na burkina faso wana ougahiphop....
huku kote husikii watu wakijadili whats what...coz we all know whats what unless we dont know nothing about this game or we r just keeping kufuata upepo...the all world knows bongoflava is tanzanian rap/hiphop...just like the all world know westcoast got g-funk and atlanta got crunk style and now they got new thing called 'trap music'...even miami got they own 'trill music'....man i cant finish this list for real!!!...anyway...real hiphop is just when u r real...
kuhusu nguzo kaka nnavyojua mimi ni kuwa muziki na u-dj vilifunika nguzo nyingine kwa kuvutia washiriki wengi zaidi...na ndo maana kuna jay-z wa hiphop ya ku-mc lakini hakuna figure ya namna hiyo kwenye washiriki wengine wa hiphop wa kwenye nguzo nyingine kama grafitti na hata breaking...nadhani unanielewa kaka....
na zaidi kila kitu kinaenda na wakati...kama breaking ni sehemu ya hiphop na ilikuwa na wakati wake wa kutamba japo haikuwa kwa muda mrefu kama unavyotamba u-mc...kumbuka marekani kulikuwa na kina bugaloo wakati bongo tulikuwa na kina digadiga na wengine waliokuwepo kabla yao ambao walikuwa wanafanya breakdance...yaani kwa maana nyingine unaweza kusema walikuwa wanafanya hiphop thru breaking way back kabla hatujaanza kurap!!!
kwa kukamilisha mi naona kinachotakiwa kufanyika ni aidha kuweka wazi na ku-retain title ya bongoflava kwa maana yake halisi au otherwise tukae kimya tu kwani zaidi ni kwamba tunaji-contradict tu na ndo maana tunashindwa kupeleka muziki wetu mbele zaidi...
huku huwa naenda kwenye colleges na universities kufanya progarams za muziki sometime...kuna watu hawajawahi hata kufika bongo nakutana nao na wanachojua wao ni kuwa bongoflava ni rap/hiphop ya tanzania full stop...
SUGU"
 
Mkuu,

Mkumbushe jamaa kuwa "Hip Hop HAIUZI"... Hahaha hiyo nyimbo inawakera sana jamaa haswa pale jamaa anapoimba kuwa "Wote wanaoimba hip hop wakauze pipi".

Si mchezo
 
Asante Mizozo na Invisible kwa inputs nzuri.

Mizozo nasema Asante kwa kuwa umechukua hatua zaidi na kwenda kuwauliza wadau hasa mdau sugu mtu wetu wa pale sinza kumekucha.

Kwa maelezo ya sugu,napata ufahamu kwamba Bongoflava ilianza ikiwa imeibeba HIp Hop kama nguzo mama ndani yake,Sawa.Siko upande wowote bado, Ila ninaloliona ni kuwa,Kwa kuwa neno BongoFlava lilianza wakati huo wakina Sugu wakiwa kwenye game na kwa kuwa style nyinge za Muziki kama Zouk,Rhumba,Wabana Pua (sorry),Zenji stlye vilikuwa havipo then,Kuja kwa hizi style na kutumbukizwa kwenye kundi moja na Hip hop kunaonesha kuwa kulikua hakuna swhwmu nyingine ya kuliweka kundi hili.

Vile vile, kwa kuwa Flava ina maana ya Ladha na Bongo ina maanisha Tanzania.Kuna tatizo gani?Iwapo tutajumuisha hizi ladha zetu za Bongo Hip Hop ikiwa mojawapo?

Mimi sehemu inayotenganisha Bongo flava na Hip HOp ndiyo nashindwa kuiona jwa kutumia maelezo yako na Sugu.
Sifichi mimi ni mpenzi wa Hip HOp zote za nyumbani na za nje ila utenganisho wake na Bongo flava wanitatiza.
Wadau wengine mwaonaje juu ya hili
 
Saleh Rajab akua mdau wa hip hop yeye alikua ni Kiswahili rapper...Hip hop walikua KU crew, diplomatz ..etc, ku-foka foka sio maana wewe ni bongo hip hop artist, hip hop ni universal na chipuko lake ni kutoka kwa vijana kule marekani (NY)...ni way of life na sio muziki pekee..ina matawi mengi na sio lazima uwe rapper kuwa mdau wa hip hop...Bongo flava ni neno ambalo maana yake ni mzika wa kizazi kipya...hilo neno limekuja baadae wakati mziki wakizazi kipya umeanza kupewa attention zaidi na kiukweli uliwajumlisha bongo rappers, hip hop, RnB, zouk, etc...ilimradi ni nyimbo ya kizazi kipya ambayo imetokea bongo... bahati mbaya wadau wa type nyingine za mziki wa bongo flava hawakujaribu categorize miziki yao hence wote wakarundikwa kwenye bongo flava ambako pale mwanzoni hata wale kiswahili rappers and bongo hip hop artist walikwepo pia....Problem ikaanza walio endelea nakupendwa zaidi na walio kuwa celebrities na wakafanikiwa ku-commercialise mziki wao hawakua wadau wa hip hip ndio BEEF iko hapo sana sana...Wadau wa Hip hop ya bongo wanajaribu kuji-distance from Bongo Flava bila kuelewa wanacho ji-ditance from...lakini hadi sasa its too late na hamna njia ya kurudi na kufanya categorization ya Bongo Flava tena ilikieleweke nini ni Bongo Flava na nini Bongo Hip Hop, RnB, Soul au Zouk...etc....
 
HIP HOP sio muziki wa kibiashara ,wasanii wengi hiki ndio kitu ambacho kimewashinda na wamehamia kwenye Bongo fleva.HIP HOP haibadiliki but Bongo fleva unakwenda na matakwa ya mashabiki so haina IDENTITY.Kuna baadhi ya wasanii walianza na HIP HOP but now wamehamia Bongo flava
Juma Nature,AY ,DUDUBAYA na wengine walianza na HIP HOP now wamehama

Hip Hop Msanii anaeleza halihalisi na haogopi kusema ukweli ndio maana wadau wa muziki(MADJ,RADIO PRESENTERS ,PROMOTERS) hawaipendi sababu jamaa wanaeleza ukweli kuwa MADJ+PROMOTERS wanawanyonya sana wasanii
Wasanii wengi wa HIP HOP wanakatishwa tamaa na DJ,RADIO PRESENTERS & PROMOTERS
Baadhi ya wasanii wamekuwa wajanja imebidi wachanganye HIP HOP & BONGO FLEVA ili wapate soko.PROF J,MwanaFA ni baadhi ambao wameangalia soko wakaona bora wachanganye.
Napenda kuwapongeza baadhi ya wasanii ambao wanakomaa na HIP HOP kama FIDQ,JOE MAKINI,NAKO 2 NAKO,MAPACHA,GEEZ MABOVU,ADILI,MANSU LI,JMOE&KIKOSI

Hip Hop IS kNowLeDge..............
 
Naomba niongelee neno LADHA ZA BONGO

Neno Lenyewe kama ambavyo linasomeka na kueleweka linamaanisha vionjo vya muziki wa hapa nyumbani (Bongo Flava). Ukilichukulia neno hilo kama ambavo nimelitafsiri utaona ya kwamba hili linajumuisha Vionjo vya Sanaa ya Muziki wa hapa Nyumbani. Sasa tunapoongelea Muziki wa Nyumbani ni kwamba tunakuwa tunaongelea zaidi ya aina ishirini za Muziki ambao watu wanaoufanya hawatajua wanadondokea katika kundi gani ukiwaweka katika Kundi moja kubwa la Ladha za Nyumbani (Bongo Flava).

Kuna Mchangiaji mmoja (CottonEyeJoe) ameandika kwamba Bongo Flava ni Muziki wa Kizazi Kipya. Sasa kabla hatujaenda Mbele tungewekana wazi kwanza kuhusiana na hili suala la Bongo Flava kuwa ni Muziki wa Kizazi Kipya, je kizazi kipya katika mantinki hii ni kipi ambacho muziki wake unaweka katika kundi la Bongo Flava? Na je katika hilo la kizazi kipya Waimbaji wa Nyimbo za Dini na Miziki mingine yenye asili ya Afrika (Bongo Dansi) nao watajumuishwa katika kundi la Bongo Flava.?

Mwisho kwa sasa ni kuhusiana na suala la kuamua kuchukua muziki wote na kuujumuisha kwa pamoja kisha kuupachika jina Bongo Flava, ni vigumu kupinga jina hilo kwani ndio jina ambalo linatumika kwa muziki wa Bongo karibia kila pembe ya Dunia. Naomba mniambie ni vitu gani haswa ambavyo vinasababisha aina fulani ya muziki wa Wasanii wa hapa nyumbani ku-qualify kujumuishwa katika kundi la Bongo Flava mathalani wasanii wa Hip Hop?

Kisha tutarudi tena tuongelee kwa nini Hip Hop ni tofauti na Bongo Flava.
 
Mizozo,cottonna Belo:
Ahsanteni kwa michango yenu Anuai ambayo inafungua watu macho kuhusiana na rabsha hii kati ya Bongo Flava na HIP HOP.
Ama kwa hakika nakubaliana na wale wasemao kuwa mihimili ya HIP HOP haiwezi kunchanganywa na Bongo Flava.Ila Iwapo Bongo Flava ni Ladha za bongo hii inatusukuma tuilundike HIP HOP kwneye kundi hili.

Inawezekana ama ni ukweli kuwa neno Bongo Flava lina maana zaidi ya Ladha za Bongo,maana wakati linaanza waliokuwa juu hatubishani kwa hili walikua ni wanmuziki wa HIP HOP.Lakini kuna wizi uliofanyika kwa jinsi ya ajabu kunya'nganya wadau walioanzisha na kuchanganya na Miziki minigne kama Baibuda, Zouk tec thanks to Bongo radio presenters!!!!

Kwa kuwa wafanyao HIP HOP ya ukweli si watu wa kung'ang'ania debate iso na mwisho then wakaamua kusimamia HIP HOp nje ya Bongo Flava.Ielweke kuwa kuna wakati hawa wasanii wa HIP HOP wa nyumbani nao wanrudi katika upande mwepesi wa Bongo Flava aidha kwa kutokujua au kwa kushawishika.Mfano, Kipindi cha Bongo Flava cha Radio Clouds ambacho kinaendeshwa na DJ Fetty kina alika wnamuziki wa HIp HOP,realy HIP HOP nao bila kufahamu wanjumuika na kukishabikia.

Siwalaumu watu wa HIP HOp.Lakin napongeza harakati za kusimamisha HIP HOP kama OKOA HIP HOP ya akina Adili na wenzake na Kadhalika.Harakati hizi basi ni vyema zikasimamiwa na wote waaminio kuwa kuna Tofauit kati ha HIP HOP na Bongo Flava.

Medani ya muziki ina vizingiti vingi ambavyo vyweza kumuhamisha mtu kutoka kwenye GENRE moja hadi nyingine.Tatizo la "MHINDI" kushikilia master na kumpatia msanii SHILINGI mia tatu (300) per tape ni tatizo linalowa fanya watu kama akina PROF JAY kuchanganya HIP HOP na Bongo flava na kisha kupoteza maana.Heko kwa wauzao nyumbani :Nako 2 Nako, Mapacha na kadhalika.

Nitarudi!!
 
Nafikiri hata SUGU,SOLO wameamua kutafuta option nyingine baada ya kuona WAHINDI bado wanawakandamiza wasanii but HIP HOP WILL NEVER DIE
 
hakuana kitu mnacho jadili hapa kwani hata mwisho wake mtakosa jibu..
Hiyo bongo flava ni impact ya FM station in Africa -result is that!!!...pili wanao jaribu kusema hip hop ni wale wanao kimbia haibu!! -Kweli kuna tofauti...



bongoflava ni matokeo ya effect ya radio communication kwa jamii..Lakini matokeo bado ni mazuri.Tena ni zaidi ya mawazo yanayo dhalau Bongoflaver .rabda bila short wave FM isinge weza!!

Labda swali zuri la kujiuliza ni nani alie tunga jina Bongoflaver?
and let MR two be God fether of it!!
 
Nafikiri hata SUGU,SOLO wameamua kutafuta option nyingine baada ya kuona WAHINDI bado wanawakandamiza wasanii but HIP HOP WILL NEVER DIE

Bello Chali Angu !!!
We ni mzee wa Watengwa Records nini hapo A town Maana naona unasimamia ile ile!!
 
BONGO FLAVA WANALIALIA OUT OF TUNE HUKU HIPHOP WANAONGEA (MASSAWE ALIKUWEPO) NA KUFOKAFOKA.
ONLY HIPHOP I CARE ABOUT IS BY AY- THE BOY GOT SKILLS AND TUNE.

BONGO FLAVA NI BENDERA FUATA UPEPO- MTU AKITOKA KWA KUIMBA HUKU AKIBANA PUA BASI REKODI ZOTE ZA MWAKA HUO NI ZA KUBANA PUA. MTU AKITOKA NA NGOMA ZA KIENYEJI BASI ZOTE NGOMA ZA KIENYEJI, MTU AKITOKA NA BEATS ZA SA BASI MTAKOMA KWA BEATS ZA AFRIKA KUSINI

ILI MRADI SHIDA!!
 
hakuana kitu mnacho jadili hapa kwani hata mwisho wake mtakosa jibu..
Hiyo bongo flava ni impact ya FM station in Africa -result is that!!!...pili wanao jaribu kusema hip hop ni wale wanao kimbia haibu!! -Kweli kuna tofauti...


bongoflava ni matokeo ya effect ya radio communication kwa jamii..Lakini matokeo bado ni mazuri.Tena ni zaidi ya mawazo yanayo dhalau Bongoflaver .rabda bila short wave FM isinge weza!!

Labda swali zuri la kujiuliza ni nani alie tunga jina Bongoflaver?
and let MR two be God fether of it!!

Naomba uniambie unasema wanaofanya/wanaodai wanafanya hip Hop wanakimbia aibu... Ni aibu gani ambayo wewe wasema xya kwamba wanaikimbia!!?

Na husiana na Sugu kufanywa Godfather wa Bongo Flava nadhani kama ungesoma maelezo yake vizuri ambayo nilipost ungepata ufahamu zaidi kuhusu yeye na kwamba anasimama wapi!

HIP HOP Lives!
 
BONGO FLAVA WANALIALIA OUT OF TUNE HUKU HIPHOP WANAONGEA (MASSAWE ALIKUWEPO) NA KUFOKAFOKA.
ONLY HIPHOP I CARE ABOUT IS BY AY- THE BOY GOT SKILLS AND TUNE.

BONGO FLAVA NI BENDERA FUATA UPEPO- MTU AKITOKA KWA KUIMBA HUKU AKIBANA PUA BASI REKODI ZOTE ZA MWAKA HUO NI ZA KUBANA PUA. MTU AKITOKA NA NGOMA ZA KIENYEJI BASI ZOTE NGOMA ZA KIENYEJI, MTU AKITOKA NA BEATS ZA SA BASI MTAKOMA KWA BEATS ZA AFRIKA KUSINI

ILI MRADI SHIDA!!

Bi Mkubwa,

Kama wewe ni kweli mpenzi wa AY na Muziki wake na unaipa Support Hip Hop to the fullest then nadhani hujui ni kitu gani ambacho unakiongelea. Na unapokuwa unaongelea Bendera kufuata upepo nadhani hata msanii Hip Hop yake ndo pekee you care about anaanguka katika kundi la Bendera kufuata Upepo. Pole kwa hilo.

Nikiwa kama mdau mkubwa sana wa muziki wa kizazi kipya hapa Bongo na mmoja wa wanaharakati wa kuokoa HIP HOP katika ile Project ya Chapakazi Productions (OKOA HIP HOP) naweza kusema kitu kimoja tu, HIP HOP ni muziki wa kweli na ni muziki ambao unaweza kusimama na kujisimamia wenyewe na kuweza kupata identity yake hapa Bongo. Hilo halipingiki.

Ukienda Upande wa Bongo Flava ni kwamba nyimbo zao na style yao ni ile ambayo mimi huwa naita "Bubble Gum Flavor" watafuna mda huu na baada ya nusu saa hakuna utamu tena. Ndio maana ukiangalia kwa undani Bongo Flava huwa inakuwa na mashabiki wa Muda ambao wanapenda wimbo flani na si aina ya Muziki, kutokana na hilo sidhani kama kutakuja xkuwa na identity ya Bogn Flava.

Upande wa hip Hop ni tofauti, unaposikiliza wimbo kama KINA KIREFU, hausikilizi unbanaji wa pua ama beat. Unasikiliza Muziki, yaani ndani yawimbo huo iunakutana na Rhyming and Reasoning na kwa hakika kama utafanikiwa kwenda above and beyond utaona kwamba kuna elimu ndani yake tena kubwa! Hip Hop is Life.

Mwisho kabisa kama mmewahi hudhuria katika show ambazo zimejumuisha wasanii wa Hip Hop na wengineo nadhani utafahamu ya kwamba Show kama hizo huwa zinabebwa na watu gani!!!

Mwisho nakubaliana na wote wanaosema kwamba wanaopoteza Utambulisho haswa wa huu Muziki ni Redio Presenters and FM Radio Stations!!!
 
Naona Mizozo umeamua kushusha darsa.Mi bado nipo upande huo usemao HIP HOP ina stand out of Wabana pua's.Big UP wazee ya wote wa OKOA Hip HOp na Wale wapiganao kusimamisha Hip Hop huko A town City.

HIP means Knowledge
and HOP means.....
 
Naomba uniambie unasema wanaofanya/wanaodai wanafanya hip Hop wanakimbia aibu... Ni aibu gani ambayo wewe wasema xya kwamba wanaikimbia!!?

Na Kusiana na Sugu kufanywa Godfather wa Bongo Flava nadhani kama ungesoma maelezo yake vizuri ambayo nilipost ungepata ufahamu zaidi kuhusu yeye na kwamba anasimama wapi!

HIP HOP Lives!

Inaonekana Wewe ni mshabiki tu...
Hii kazi tuachie!! lakini sio mbaya niki ku elimisha kidiogo...
Nilianza Hip hop 1988!! nikiwa mdogo sana!! Baadae nika ona tofauti!! kubwa kati ya vijana waliopo Dar na wale waliopo Mikoani!! Dar Kulikua na FM stations nyingi zaidi kuliko sehemu Nyingine...hata vijana walio kimbilia kua Ma produser huko Dar ilikua ni rahisi kupata software na ufahamu zaidi wa vipaji vyao!! kuliko Kijana alieko Sumbawanga!! kwa kina Mizengo Pinda!! Hata hivyo Vurugu yote hiyo ilikua ni mwangwi wa miziki ya West!! ....ya wamarekani Weusi!!


Kama Fm station wange rusha kwa muda mrefu miziki ya Zuku...leo hii hiyo unayo iita Bongo flaver ingekua Zuku!!...kitu fulani kinacho fanana na Zuku..


au ingekua Jazz basi leo ingekua Bongofalaver yenye jazz!!

Hata kama Tanzania ingepiga marufuku tape na radio transmition za Rap na Hip hop ikapiga nyimbo za utamaduni..leo hii kungekua na real bongoflaver/kama country music unazo zipenda kuzisikiliza!!....

lakini haya yote ni matokeo ya muingiliano wa jamii...Bongo falver ni matokeo ya muingiliano wa sauti na utamaduni wa kisasa...wa jamii yetu...
Ni kitu kizuri...

Usije ukajiona mjanja..kwa kuwaona wakina mwana FA wajinga eti kwasababu wanaimba bongo flaver!!...watu wote bado wanaimba bongo flaver!!...icho mnach kiita Hip hop kianatokea mara cahace sana!! ndani ya Bongo flava!!

mna mdhalau sana Mr 2...kama ilivyo tabia yenu nyie mnao jiita wabongo!!...Mr 2 ni zaidi Swahele jabili...japo wote nawapa heshima...kama bado mnasubili Godfather wa Art in Africa* basi anzeni kukubali Mr2 ni Master wa bongoflaver!!

wanakimbia aibu...hawataki kuenekama kwamba wako full affected na other people's art!! lakini ukweli ni kwamba hata Michael Jackson has been affected with other people's art!!

Take care this massage comes to you from some one who have been affected in art by James Brown
 
Inaonekana Wewe ni mshabiki tu...
Hii kazi tuachie!! lakini sio mbaya niki ku elimisha kidiogo...
Nilianza Hip hop 1988!! nikiwa mdogo sana!! Baadae nika ona tofauti!! kubwa kati ya vijana waliopo Dar na wale waliopo Mikoani!! Dar Kulikua na FM stations nyingi zaidi kuliko sehemu Nyingine...hata vijana walio kimbilia kua Ma produser huko Dar ilikua ni rahisi kupata software na ufahamu zaidi wa vipaji vyao!! kuliko Kijana alieko Sumbawanga!! kwa kina Mizengo Pinda!! Hata hivyo Vurugu yote hiyo ilikua ni mwangwi wa miziki ya West!! ....ya wamarekani Weusi!!


Kama Fm station wange rusha kwa muda mrefu miziki ya Zuku...leo hii hiyo unayo iita Bongo flaver ingekua Zuku!!...kitu fulani kinacho fanana na Zuku..


au ingekua Jazz basi leo ingekua Bongofalaver yenye jazz!!

Hata kama Tanzania ingepiga marufuku tape na radio transmition za Rap na Hip hop ikapiga nyimbo za utamaduni..leo hii kungekua na real bongoflaver/kama country music unazo zipenda kuzisikiliza!!....

lakini haya yote ni matokeo ya muingiliano wa jamii...Bongo falver ni matokeo ya muingiliano wa sauti na utamaduni wa kisasa...wa jamii yetu...
Ni kitu kizuri...

Usije ukajiona mjanja..kwa kuwaona wakina mwana FA wajinga eti kwasababu wanaimba bongo flaver!!...watu wote bado wanaimba bongo flaver!!...icho mnach kiita Hip hop kianatokea mara cahace sana!! ndani ya Bongo flava!!

mna mdhalau sana Mr 2...kama ilivyo tabia yenu nyie mnao jiita wabongo!!...Mr 2 ni zaidi Swahele jabili...japo wote nawapa heshima...kama bado mnasubili Godfather wa Art in Africa* basi anzeni kukubali Mr2 ni Master wa bongoflaver!!

wanakimbia aibu...hawataki kuenekama kwamba wako full affected na other people's art!! lakini ukweli ni kwamba hata Michael Jackson has been affected with other people's art!!

Take care this massage comes to you from some one who have been affected in art by James Brown

Hivi Ndugu huu mjadala umeudakia njiani ama umeanza nao mwanzo ukajaribu kuelewa vizuri? Na je unaweza kutofautisha kati ya Shabiki na mtu kama wewe. Je kuanza Hip Hop mwaka 1988 (Which i doubt maana sijui kama ilikuwa hapa Bongo ama somewhere else maana miaka hiyo....3 years after utawala wa Nyerere mengi yalikuwepo). You should know this I am Hip Hop.

Katika game ya Muziki ya Tanzania nimekuwa nayo toka inaanza. Nimekuwa na hawa Artists wa Bongo toka wakiwa katika Mihangaiko ya kutoka na kutafuta maana na uhasilia wa Muziki wao ambayo sidhani kama wameipata. Umeongelea Sumbawanga, sisi tumefanya Show Sumbawanga miaka ile unafika na kukutana na Nyimbo za Mr II (Sugu) pekee maana ni album yake tu ndo FM waliweza ifikisha kule. Mimi ni shuhuda wa Muziki wa Bongo wa Kizazi Kipya toka mwanzo mpaka muda huu. Nilichokuwa najaribu kukufahamisha ni kwamba huwezi Mcrown Sugu ati Godfather wa Bongo Flava!!! Utakuwa unamtusi kikuu. Katika kuhakikisha Hip Hop ya Bongo inasimama ndo maana SUGU mwaka 2005 alikuja na HIP HOP SUMMIT YA TANZANIA! Na pia nilikuwa Key Player katika hilo. Unataka nikuambie ni nini yalikuwa madhumuni na Madhumuni ya hiyo SUMMIT?

Hakuna mtu aliyemuona FA ama Matonya ni wajinga ama Kikosi, Adili na Fid Q wamepotea njia katika aina ya Muziki wanayofanya. Hili ni jambo la kufahamu ni nini haswa ambacho unataka ku-achieve katika yote ufanyayo.

Unaongelea vijana wa mjini na mikoani unajua nini juu ya hilo? Unafahamu aina ya Muziki inayofanywa na undergrounds wa Mikoani kwa kiasi kikubwa ama? Unafahamu haswa muziki wa Bongo unaendaje wewe? Na unafahamu hivi kuna aina ngapi za muziki zinafanya Bongo Flava ama?

Mwisho unasema vurugu yote ilikuwa ni Mwangwi wa Wanamuziki wa Marekani (Weusi), huoni kwamba ilikuwa si mwangwi (Echo) maana eventually mwangi hupotea, kinachofanyika kila siku ni kuchukua Muziki wa Kigeni na Kujaribu ufitisha katika Jumuia ya Bongo na kufanya tuwe na identity yetu.

Fikiri kwa umakini kabla ya kujibu!


SOME GOT WAYS AND MEANS, WE GOT HOPES AND DREAMS!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom