Kuna tofauti gani kati ya "Operation Sangara" na "M4C"

Kuna tofauti gani kati ya "Operation Sangara" na "M4C"

Alfu Lela Ulela

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2010
Posts
1,255
Reaction score
77
Wakuu kuna tofauti gani kati ya "OPERATION SANGARA" na "M4C"?

Na ni kwanini CHADEMA wameamua kushift kutoka Operation Sangara kwenda M4C? Yeyote anae jua tafadhali atuelimishe maana na tofauti kati ya hizo movement tajwa.
 
KUNA TOFAUTI GANI KATI YA "OPERATION SANGARA" NA "M4C"
na kwanini CHADEMA wameamua kushift kutoka Operation Sangara kwenda M4C?????? Anyone who knows shld provide public education here for the benefit of the mass.
Haina tofauti ni katika harakati zakumng'oa mkoloni mweusi CCM
 
Hiyo "operesheni Sangara" ndio mbwembwe za CHADEMA zilipo anzia, lakini mbwembwe zao hizo hazikuzaa matunda kutokana na Sangara wote kuliwa na mamba mmoja ambae ni CCM.

Baada ya sangara wa CHADEMA kuliwa bila huruma na mamba la CCM wakajitutumua na kuanzisha harakati nyingine ambayo maudhui yake ni kama ya opereshi sangara, ambayo ndio hiyo M4C.

Sasa na hii M4C tunailia taimingi tu, tukiona inavuka mipaka na minyau basi kama ilivyo ada, tunalifungulia li-MAMBA letu ili litafune vijishabiki vya M4C vyote.
 
Mkuu Alfu Ulela,

Nijuavyo mimi ni haya; (Ila bahati nzuri tuna viongozi na members toka Chadema ambao watajibu vema zaidi).

Chadema wamekuwa na mikakati na harakati yenye kukumbatia na kuhakikisha inawafungua macho jamii na kuwafungua akili ili kuwaamsha wananchi katika masuala ambayo yanawagusa, na ni kwa namna ipi ‘Utawala' na viongozi katika utawala wana shiriki moja kwa moja katika kuathiri maisha ya jamii katika kila Nyanja ya maisha. Kuwezesha mikakati na harakati hizo kumekuwa na oparesheni zenye mlengo huwa wa kuifikia jamii ya Tanzania kila mahala nchini.

Oparesheni kwa sasa ambayo inafanya kazi ndani ya Chadema ni maarufu kwa jina la "Movement for Change (M4C)". Uongozi wa Chadema wamewekeana utaaratibu wa kazi ambao umegawa majukumu dhidi ya viongozi kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na kupita Tanzania nzima.

Nje ya oparesheni hiyo ya M4C kuna oparesheni nyingine mfanano iliyo wahi pia anzishwa kwa malengo ambayo yapo karibu sawa kabisa. Hio opareshini iliyowahi fanywa ni moja maarufu kwa jina la ‘operation Sangara'.

Katika makala hii nimeweka Mh. Zitto Kabwe anaeleza na kufafanua kwa kirefu ni kwa nini oparesheni Sangara ilibuniwa.

Kwa maelezo zaidi, soma hii makala juu ya 'Operation Sangara' pengine itakusaidia.
KWANINI TUMEBUNI ‘OPERESHENI SANGARA'
Raia Mwema|Novemba 5, 2008
NIKIWA Mjini Mugumu, Serengeti katika ziara ya kikazi ya viongozi wote wa CHADEMA katika kujenga chama chetu, ninapata taarifa ya mkutano wa waandishi wa habari ambao Katibu Mwenezi wa CCM, Kapteni John Chiligati aliuitisha kukanusha kwamba nchi imekosa mwelekeo.

Alikuwa akijibu hoja ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kwamba kwa hali ya sasa ya nchi, Rais Jakaya Mrisho Kikwete hapaswi kupewa kipindi cha pili cha utawala. Chiligati anasema nchi imetulia, ni shwari kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Chiligati aling'aka na kuanza kumshambulia Mbowe; huku akitumia maneno yasiyopendeza kana kwamba Mbowe alimtukana Rais Kikwete. Mbowe hakumtukana Rais Kikwete. Mbowe alisema Uongozi umemwelemea Rais Kikwete, na hivyo asipewe kipindi kingine cha uongozi. Huko si kutukana.

Nilikaa na kutafakari kwa kina sana kwa nini Chiligati amesema maneno ambayo hayaendani na taswira yake kama mtu mpole na muungwana? Mimi ninamwona Chiligati hivyo. Sikumjua kabla sijawa mbunge, nimemjulia Bungeni, tena baada ya kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, wakati huo wizara hiyo ilikuwa imebakia na vitengo vya Magereza, Uhamiaji na Zimamoto. Haikuwa Wizara kubwa sana, lakini wizara muhimu kwa usalama wa nchi.

Nilimwona ni mtu muungwana, aliyekuwa akishirikiana kwa karibu sana Waziri wetu kivuli katika Wizara hiyo, Ndugu Mhonga Ruhwanya. Ndiyo maana nilishangazwa sana wakati Chiligati alipoamua kutoka kwenye hoja na kuamua kumshambulia Mbowe huku akitumia maneno yasiyopendeza!

CHADEMA imezindua kampeni maalumu ya kuimarisha chama katika maeneo ya vijijini. Operesheni hii tumeiita ‘Operesheni Sangara'. Kwa nini Sangara? Kwa kweli wala hatukufikiria kwa kina sana kuna nini katika jina hilo. Tuliamua kutafuta kitu kinachowaunganisha wananchi wa mikoa ya Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mwanza na Mara. Tulitafuta kitu ambacho kinahusiana na maisha ya kila siku ya wananchi wa mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga.

Tukakuta Sangara ni jina murua; kwani ni samaki alie katika Ziwa Viktoria, na ni samaki anayeliingizia Taifa mapato mengi sana. Takwimu za Hali ya Uchumi wa Taifa zinaonyesha kuwa samaki wa Ziwa Viktoria wanachangia takriban asilimia 8 ya mauzo yetu nje ya nchi. Thamani ya mauzo ya samaki kutoka Ziwa Viktoria ni karibia Tshs. 150 bilioni kwa mwaka.

Hata hivyo, sehemu kubwa ya fedha hizi zinabaki kwa wawekezaji wachache na Taifa halipati kiasi kinachostahili cha mapato yake kutokana na utajiri huu. Vilevile wananchi wanalalamika kuwa kitoweo cha samaki kimekuwa ghali sana kufuatia samaki wote kuuzwa nje na wao kubakia na mapanki. Jina hili lilitosha kuwa sehemu ya kampeni ya uimarishaji wa chama katika Kanda ya Ziwa Viktoria.

Katika operesheni hiyo, nimepata fursa ya kutembelea majimbo yote ya mkoa wa Mara isipokuwa jimbo la Musoma Vijijini. Musoma Vijijini nimewahi kwenda; Butiama katika misa ya Baba wa Taifa kwa mwaliko maalumu wa mbunge wa Jimbo hilo. Nilikwenda pia Buhemba kwa ziara ya Kamati ya Rais kuhusu Mikataba ya Madini.

Ninaamini kabla hatujaenda mkoa wa Mwanza kuendelea na Operesheni mnamo Novemba 11, tutapata fursa ya kupita katika jimbo la Musoma Vijijini ili kuzungumza na wananchi na kuimarisha chama chetu cha CHADEMA.

Ziara hii imenifumbua macho ya maisha ya Watanzania. Nilipomsikia Chiligati akisema hali ni shwari; kisha nikaangalia maisha ya wananchi wa Buhare (Musoma Mjini), Bukura (Rorya), Nyanungu (Tarime), Muriba (Tarime), Nansimo (Mwibara), Hunyari (Bunda) na Nyamuswa (Bunda), nikasema kweli viongozi wetu wengi hawapo na wananchi (out of touch).

Nikachunguza mara ya mwisho Ndugu Chiligati alikwenda kutembelea wananchi wa vijijini lini toka amekuwa Katibu Mwenezi wa CCM, nikapata taarifa kuwa hajawahi hata siku moja. Nikathibitisha kuwa yeye na wenzake wapo out of touch! Wanajifungia katika maofisi yao yenye viyoyozi Dar es Salaam na kuitisha press conferences na kusema nchi ipo shwari.

Hali ya nchi sio nzuri hata kidogo. Nitatumia mifano halisi niliyoiona katika vijiji vya mkoa wa Mara na kuihusanisha na takwimu za serikali kujenga hoja zangu kwamba CCM imeshindwa kuongoza Taifa letu, imebaki inatawala na ndio maana wao wenyewe wanapenda kujiita ‘Chama Tawala'.

Kwa maoni yangu, hatupaswi kuruhusu CCM kutimiza nusu karne katika utawala; kwani mwaka 2011 tunatimiza miaka 50 ya Uhuru wa upande mmoja wa Taifa letu (Tanzania Bara). Wazalendo wote wa Taifa hili wanapaswa kujiandaa na kuizuia CCM kutufikisha nusu karne; kwani kwa hali ya sasa CCM ni hatari kwa usalama na ustawi wa Taifa letu. Nitajieleza!

Mwaka 2005 wakati wa Kampeni za Uchaguzi, CCM waliahidi katika Ilani yao ya uchaguzi kuwa ifikapo mwaka 2010 watakuwa wamepunguza umasikini wa Watanzania kutoka asilimia 38 ya Watanzania mpaka asilimia 19.

Mwaka 2005 kulikuwa kuna Watanzania masikini takribani milioni 11. Hapa tafsiri ya masikini ni wale watu wote ambao kipato chao kwa mwezi ni chini ya Shs 14,000; yaani chini ya Sh 400 kwa siku. Hiki ni kiwango cha chini sana; kwani kufuatia kupanda bei kwa bidhaa na hasa chakula, hata mwenye kipato cha Shs 30,000 kwa siku bado ni mtu masikini tu.

Mnamo Oktoba 3, 2008 Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo alitangaza takwimu mpya za hali ya umasikini nchini. Takwimu hizo zimefuatia utafiti uliofanywa na Ofisi ya Takwimu nchini na utafiti huo unaitwa kwa kimombo Household Budget Survey. Takwimu hizi mpya zinaonyesha kuwa Watanzania walio masikini wa kutupwa sasa wamefikia milioni 12.7.
Hii inaonyesha kuwa Serikali ya CCM ya awamu ya nne, katika kipindi cha miaka 3 ya utawala wake, badala ya kupunguza umasikini miongoni mwa Watanzania, imeongeza masikini zaidi ya milioni 1. Hii imetokana na ukweli kwamba chama hiki kimekuwa ‘kizee', kimechoka na hakina mawazo mapya.

Chama hiki tukikiacha madarakani, tena kikiwa na ukiritimba wa Bunge ambao hivi sasa CCM inao, kitaingiza watu wengi zaidi katika dimbwi la umasikini.
Njia mojawapo ya kuokoa Taifa letu, ni kutoruhusu CCM kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, na hivyo kuuunda tena serikali. Ikitokea hivyo, basi CCM isiwe na ukiritimba bungeni kama ilivyo sasa ambapo asilimia 86 ya wabunge wanatoka chama hicho kimoja.

Hii ndio mantiki ya Mbowe kusema kwamba tusimruhusu JK kuchukua muhula wa pili. Mbowe hakuwa na maana ya Kikwete kama mtu binafsi; bali CCM. Kwani ikiwa ni suala la Kikwete kama mtu binafsi, CCM watabadili mtu na hivyo kuendelea kutawala. Unachosema, CCM ya awamu ya nne haistahili kupewa muhula wa pili kwani wamechoka na hawana mawazo mapya ya kuondoa umasikini wa Watanzania.

CCM ya sasa haina idara ya sera wala utafiti na hivyo, hawaongozi tena sera za serikali wanayoongoza; bali wanategemea serikali kutengeneza sera na wao wanazikariri katika ilani zao. Lengo la kupunguza umasikini kutoka asilimia 38 mpaka asilimia 19, lilikuwa lengo la MKUKUTA ambapo CCM kwa kutaka kura tu, waliamua kukariri MKUKUTA na kuuweka katika kitabu cha kijani na kisha kuiita ilani.
Watu wa Gazeti la The Economist waliwahi kuita ilani ya CCM kuwa ni ‘Wishlist'. Sasa imedhihirika kuwa lengo hili kubwa la kupunguza umasikini, limeshindikana. CCM wataweza nini?

Leo, CCM imetengeneza mataifa mawili ndani ya Taifa moja la Tanzania. Hivi sasa kuna Taifa la Masikini na Taifa la Matajiri. Masikini wana shule zao zinazoitwa Sekondari za Kata. Matajiri wana shule zao zinazoitwa ‘Academies au English Medium'. Watoto wa masikini katika Sekondari za Kata wanasoma katika mazingira magumu sana. Shule hazina walimu, madarasa hayana madirisha na hata vitabu hakuna.

Nilipokuwa Wilaya ya Rorya nilitembelea Kata ya Bukura. Pale Bukura nilipata bahati ya kutembelea shule ya Kata na kuzungumza na wanafunzi. Shule hii inayoitwa Shule ya Sekondari ya Bukura ina kidato cha Kwanza na cha pili. Shule ya Sekondari Bukura ina Walimu 4 tu na wanafunzi waliniambia walimu wote ni wa masomo ya sanaa. Hakuna Mwalimu wa Sayansi!

Shule ya Sekondari Bukura haina uhakika kama mwakani wataweza kuingiza kidato cha kwanza; kwani wao wamejenga madarasa mpaka uwezo wao, lakini msingi wa darasa la kidato cha tatu bado upo chini kabisa. Hawana msaada wa serikali.

Nimejionea madarasa ambayo hayana madirisha wala milango. Kuna watoto wanatembea kilometa nane kufika shule. Na matokeo yake katika kipindi cha mwaka huu peke yake, watoto wa kike 5 walipata uja uzito.

Wanafunzi wa Bukura, wanaonekana ni wenye akili sana, waliniambia kwa nini vyama vya siasa tunapewa ruzuku badala ya ruzuku hiyo kujenga miundombinu ya shule zao. Niliwaeleza umuhimu wa vyama vya siasa katika uongozi wa nchi. Nikawaambia lazima vyama viendeshwe na bila ruzuku matajiri wachache watamiliki vyama. Wakaniambia mbona tayari vyama vimeshikwa na matajiri?

Wakanisuta na kuniambia mbona ninyi wabunge hamshindi bila kutoa takrima? Wakaniambia mbona wameona rushwa katika uchaguzi wa viongozi wa CCM katika ngazi ya kata na tawi?

Niliwaangalia watoto wale na kukumbuka takwimu za serikali kuhusu elimu. Kwamba hivi sasa kila mwalimu mmoja anafundisha watoto 65 (Rejea PHDR 2007), kwamba watoto 20 wanachangia kitabu kimoja shuleni, kwamba wakati uandikishaji wa watoto umeongezeka na kuvuka malengo ya MKUKUTA, hakuna ufuatiliaji kujua watoto wanasoma nini shuleni.
Kata ya Bukura yenye vijiji vya Nyambori, Bwiri, Thabache na Bubombi, kweli wananchi wake wanaweza kusema hali nchini ni shwari wakati watoto wao hawapati elimu wanayostahili kama raia wa taifa huru?

Tukirudi kwa Chiligati; najua anajua fika kwamba fedha zilizoibwa Benki Kuu kwa akaunti ya EPA peke yake zingeweza kujenga madarasa 24,000. Madarasa 24,000 ni sawa na madarasa mawili kila kijiji; maana Tanzania ina vijiji 12,000.

Hivyo kama mafisadi wasingefisadi fedha hizi, watoto wa Bukura wasingekuwa wanamlalamikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini kuhusiana na vyumba vya madarasa.
Kama fedha za EPA zingejenga nyumba za walimu, zingejenga nyumba 19,000. Chiligati anasema nchi ipo shwari, itakuwaje shwari wakati Serikali ya CCM imeshindwa kutunza Hazina yetu? Kama wameshindwa kuaminika kwa hazina yetu, tuwaamini kweli waendelee kuangalia hazina yetu mpaka 2015?

Tunaposema wasipigiwe kura na kupewa miaka mingine mitano tuna maana kuwa CCM haiaminiki tena kutunza fedha zetu za kodi. CCM na viongozi wake hawajui kuwa kila saa inayopita kuna mwanamke mmoja wa Tanzania anafariki dunia kwa matatizo ya uzazi (Maternal Mortality).

Taarifa ya Hali ya umasikini nchini ya mwaka 2007, inaonyesha kuwa katika kila Watanzania wanawake 100,000, wanawake 578 wanapoteza maisha kwa ukosefu wa huduma nzuri za afya kwa kina mama. Hii ni sawa na kupoteza Mtanzania mwanamke 1 kila saa.
Miaka 47 baada ya uhuru, tunashindwa kulinda afya ya kina mama zetu! Haiwezekani hali ya Taifa ikawa nzuri ilhali tunapoteza mwanamke mmoja kila saa kwa matatizo ya uzazi.

CCM kwa uchovu wake imeshindwa kuona ya kwamba kuna chumi mbili nchini na uchumi mmoja unakua na mwingine umedumaa. Uchumi wa mijini (Urban Economy) unakua na kukuzwa na sekta za madini, ujenzi, mawasiliano na utalii. Sekta hizi ndizo sekta zinazokua kwa kasi ikiwemo pia sekta ya fedha kama mabenki na bima. Wenye kushika sekta hizi ni matajiri wenye fedha. Kwao hali ya uchumi ni shwari sana.

Uchumi wa Vijijini (Rural Economy) umedumaa. Uchumi huu unaendeshwa na sekta ya Kilimo ambacho ukuaji wake umebakia asilimia 4 tu kwa takribani miaka 3. Hivyo watu wa vijijini hali zao zimekuwa mbaya sana kwani wanauza bidhaa zao kwa bei za vijijini na wananunua bidhaa kama mafuta, sukari nk kwa bei za mijini. Hivyo wananchi wa vijijini wanapigwa kweli kweli na maisha.

Serikali ya CCM labda inashindwa kuelewa kuwa baada ya Ndugu Benjamin Mkapa kujenga misingi imara ya uchumi mkubwa (macro) , hii ya Ndugu Kikwete ilipaswa kutafsiri uimara wa misingi hii kwa maisha ya wananchi wa kawaida wanaotegemea kilimo.
Nilitaraji hii ndio ilikuwa kazi ya msingi ya serikali ya CCM ya awamu ya nne. Imeshindikana miaka 3 ndani ya utawala. Ndio maana tunasema hawastahili kupewa kipindi kingine. Na ndiyo maana tumebuni Operesheni Sangara kuwaeleza wananchi ukweli wa mambo!

CC. Zitto, Dr. Slaa, Mikael P Aweda, Mwita Maranya, Molemo, Ben Saanane
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Alfu Ulela,

Nijuavyo mimi ni haya; (Ila bahati nzuri tuna viongozi na members toka Chadema ambao watajibu vema zaidi).

Chadema wamekuwa na mikakati na harakati yenye kukumbatia na kuhakikisha inawafungua macho jamii na kuwafungua akili ili kuwaamsha wananchi katika masuala ambayo yanawagusa, na ni kwa namna ipi ‘Utawala’ na viongozi katika utawala wana shiriki moja kwa moja katika kuathiri maisha ya jamii katika kila Nyanja ya maisha. Kuwezesha mikakati na harakati hizo kumekuwa na oparesheni zenye mlengo huwa wa kuifikia jamii ya Tanzania kila mahala nchini.

Oparesheni kwa sasa ambayo inafanya kazi ndani ya Chadema ni maarufu kwa jina la “Movement for Change (M4C)”. Uongozi wa Chadema wamewekeana utaaratibu wa kazi ambao umegawa majukumu dhidi ya viongozi kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na kupita Tanzania nzima.

Nje ya oparesheni hiyo ya M4C kuna oparesheni nyingine mfanano iliyo wahi pia anzishwa kwa malengo ambayo yapo karibu sawa kabisa. Hio opareshini iliyowahi fanywa ni moja maarufu kwa jina la ‘operation Sangara’.

Katika makala hii nimeweka Mh. Zitto Kabwe anaeleza na kufafanua kwa kirefu ni kwa nini oparesheni Sangara ilibuniwa.

Kwa maelezo zaidi, soma hii makala juu ya 'Operation Sangara' pengine itakusaidia.


CC. Zitto, Dr. Slaa, Mikael P Aweda, Mwita Maranya, Molemo, Ben Saanane

Asante mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo "operesheni Sangara" ndio mbwembwe za CHADEMA zilipo anzia, lakini mbwembwe zao hizo hazikuzaa matunda kutokana na Sangara wote kuliwa na mamba mmoja ambae ni CCM.

Baada ya sangara wa CHADEMA kuliwa bila huruma na mamba la CCM wakajitutumua na kuanzisha harakati nyingine ambayo maudhui yake ni kama ya opereshi sangara, ambayo ndio hiyo M4C.

Sasa na hii M4C tunailia taimingi tu, tukiona inavuka mipaka na minyau basi kama ilivyo ada, tunalifungulia li-MAMBA letu ili litafune vijishabiki vya M4C vyote.

Mtaweweseka sana mwulize bosi wako anayekupa buku7.NAPE MZEE WA TEMBO JEHU MWINGULU wanatambua M4C ninin .
 
Yoye dugu moja

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Utofauti wake ni kama kampuni zinavyobadili majina ili kukwepa kodi. M4C na OS ni majina tu yamebadilishwa na wahuni wachache wa CDM ili waendelee kupata ela za kula na kutumia kwa kukusanya michango. Ndio maaana karibu kwenye kila mikutano yao wanayofanya hasa ya Lema lazima bakuli na ndoo zipitishwe ili muwachangie.
 
operasheni sangara ulikua ni mpango wa kuongeza wanachama na kufungua matawi na kukitangaza chama kiujumla. m4c ni vuguvugu la mabadiliko. lengo lake ni kuwaweka tayari watanzania kwaajili ya mabadiliko ya kiutawala 2015. vilevile chama kinajiandaa kimkakati ni namna gani kitaongoza nchi kwani 2015 sio mbali. hiyo ndo m4c bana. mia
 
Hiyo "operesheni Sangara" ndio mbwembwe za CHADEMA zilipo anzia, lakini mbwembwe zao hizo hazikuzaa matunda kutokana na Sangara wote kuliwa na mamba mmoja ambae ni CCM.

Baada ya sangara wa CHADEMA kuliwa bila huruma na mamba la CCM wakajitutumua na kuanzisha harakati nyingine ambayo maudhui yake ni kama ya opereshi sangara, ambayo ndio hiyo M4C.

Sasa na hii M4C tunailia taimingi tu, tukiona inavuka mipaka na minyau basi kama ilivyo ada, tunalifungulia li-MAMBA letu ili litafune vijishabiki vya M4C vyote.

Na hilo limamba linavyopenda watu wa Mbeya sasa...mmmh! mara matumbo nje iringa, mara kucha, mara meno, mara macho vitolewe bila ganzi. sijui tujifiche wapi jamani na kwetu ni hapahapa! eee Mungu wa Ibrahim tusaidie kuliuwa hili mamba....
 
Wakuu kuna tofauti gani kati ya "OPERATION SANGARA" na "M4C"?

Na ni kwanini CHADEMA wameamua kushift kutoka Operation Sangara kwenda M4C? Yeyote anae jua tafadhali atuelimishe maana na tofauti kati ya hizo movement tajwa.


Tofauti iko wazi

Moja ni 'OPERATION' nyingine ni 'MOVEMENT'
 
Wakuu kuna tofauti gani kati ya "OPERATION SANGARA" na "M4C"?

Na ni kwanini CHADEMA wameamua kushift kutoka Operation Sangara kwenda M4C? Yeyote anae jua tafadhali atuelimishe maana na tofauti kati ya hizo movement tajwa.
Hazina tofauti zote ni mbinu za kuendeleza ulaji; jiandaeni kuchangishwa slaa na genge lake la walaji chini ya mweka hazina Lema wanazisubiri
Chama
Gongo la mboto Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Wakuu kuna tofauti gani kati ya "OPERATION SANGARA" na "M4C"?

Na ni kwanini CHADEMA wameamua kushift kutoka Operation Sangara kwenda M4C? Yeyote anae jua tafadhali atuelimishe maana na tofauti kati ya hizo movement tajwa.

Mantiki ni ilele isipokuwa M4C ni ya kisasa zaidi kuliko Operation Sangara ni samaki wa kanda ya ziwa huko Iringa na Mbeya sangara hupelekwa kwenye viroba.
 
Na hilo limamba linavyopenda watu wa Mbeya sasa...mmmh! mara matumbo nje iringa, mara kucha, mara meno, mara macho vitolewe bila ganzi. sijui tujifiche wapi jamani na kwetu ni hapahapa! eee Mungu wa Ibrahim tusaidie kuliuwa hili mamba....

CCM ni Mamba?????
 
Back
Top Bottom