Pi Network
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 290
- 319
Wakuu kwa kipindi kirefu nimekuwa nikitumia hizi Card mbili za bank kwa ajili ya kupata huduma za ki-fedha katika ATM zote zinazo ruhusu kutumia (Visa card & Master Card) zilizopo hapa nchini bila shaka na hata nje ya nchi. Lakini pia nimekuwa nikizitumia kununua bidhaa online, ikiwa ni pamoja na kulipia baadhi ya Apps muhimu pale inapohitajika.
Kwa kweli ni jambo zuri sana na ni mradi unaofaa zaidi hasa katika jamii yetu ukilinganisha na changamoto mbalimbali zilizopo ndani ya mabenki na uchache wa mabenki hasa huko vijijini na maeneo ya mashambani ambako hakuna bank isipokuwa ATM.
Lakini yote tisa, kumi, licha ya Card hizi kupigiwa debe duniani kote, na ma-Bank karibu yote hasa hapa nchini kuanza kutoa kadi hizi; bado sijajua tofauti kubwa iliyopo kati yake.
Na kwanini hizi Card? Nini kimejificha ndani ya hizi Card?
Je, kuna hatari yoyote iliyojificha ndani ya mpango huu?
Kuna siri nimeisikia japo ni kwa jujuu tu na sitaki kuiamini sana, hivyo pengine yawezekana humu ndani tunao watu wanaoijua vizuri zaidi na wanaweza kujuza na sisi.
Mwisho: nawatakieni weekend njema kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya utakao ambatana na mambo mapya.