Kuna Tatizo gani benki ya CRDB?

Kufuatilia mkopo wapo, nadhani unajua anapata commision kwa kila mkopo unao kamilika.. so anakuona mtu muhimu sana.

Hutakiwi kumpa hata cent 5.

Siyo kila taasisi inampa loan officer commission. Tena nyingi ni target driven,loan officer usipofikisha kwa muda flani kazi huna. Na wengi wanaotoa kitu kidogo ni wafanyabiashara na lengo ni kutengeneza mazingira mazuri baada ya mkopo(marejesho). Loan officer akiamua kufuata sheria kabisa za marejesho,unaweza kuichukia Taasisi. Ila mfanyakazi haina haja ya kubembeleza sana kwani Taasisi nyingi zinawatafuta
 
Kufuatilia mkopo wapo, nadhani unajua anapata commision kwa kila mkopo unao kamilika.. so anakuona mtu muhimu sana.

Hutakiwi kumpa hata cent 5.
Utakuwa ulizaliwa miaka ya 1960s mpaka 1970s... kwa msamiati unaoutumia.

Wa siku hizi wangisema, hutakiwi kumpa hata mia! / jero / buku...
 
CRDB kupata mkopo baada ya mwezi 1 hata kama umejaza na kurudisha form.
Huwa wanadanganya mfumo lakini si kweli wanatoa kwa mafungu.
CRDB imeondoka na Kimei
 

Kweli kabisa.
Juzi nime download app yao.
Nikaweka taarifa zote.
Mwisho ikagoma .

Makato sim banking ni makubwa sana.
 
Kuna rafiki yangu alijaza fomu ya kuomba mkopo ilichukua wiki 3 ndio akapata. Nikamuuliza loan officer akaniambia wana shida kwenye system yao. Nikamuuliza tena nikianzisha mchakato inachukua muda gani kupata,akaniambia hana uhakika maana makao makuu ndio wanazingua.
Baada ya kama wiki moja tena nikamuuliza,akaniambia ni bora nicheki kwingine maana kwao kwa sasa system haieleweki. Anasema wamewaandikia barua makao makuu ili wawaelekeze mfuko utakaa sawa lini,makao makuu wamepiga kimya hawajibu.
 
Hao ABSA utaratibu wao wa mikopo ukoje mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…