Kuna siri gani ya ufugaji bata na linepolice

dansmith

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
2,305
2,094
Jana nimetembelea line police maeneo ya Changombe nimekuta bata kibao na halo hiyo nimeshaona line police kibao je kuna siri gani ya bata na haya maeneo
 
Mimi naona ni katika hali ya kuigana tu katika kufanya mambo. Jirani anafuga hiki au anafanya biashara hii na mimi naiga hivyo hivyo. Sidhani kama kuna siri yoyote zaidi ya hii hali ya kuigana.
 
Ni Kwa vile kambi nyingi kunakuwa na Maji uhakika ambayo ni bure pia chakula Cha mahabusu kinakuwa cha kutosha yani availability of food ndo inapelekea bata wanashamili mnoo
 
Nafikiri kuna sababu kuu mbili, ya kwanza ameisema Bonesmen kuwa urahisi wa upatikanaji wa chakula.
Pili, ujenzi wa nyumba nyingi za polisi ni wa mabati na wengine zile nyumba zao zina ua ambao inawapa uhuru wa kufuga bata kwenye kwa vile ujenzi wa mabanda ni rahisi na nyumba zao hazina wapangaji wengine ambao huenda wasingependa karaha na usumbufu wa hao bata.

Hauwezi kukuta bata wanafugwa kwa kasi hiyo kwenye makazi ya nyumba za kupanga, utagombana na watu bila sababu.

Kingine nafikiri ni usalama, mwizi wa kwenda kuiba bata polisi anatakiwa afanye mahesabu makali sana japo nasikia kuna mwendeshabodaboda amembaka mjeda!!!!!!
 
Hapo katika red naomba ufafanuzi tafadhali

MKUU kuna uzi ulikuja jana hapa kwamba kuna dereva wa bodaboda kampakia mjeda kisha njiani akafanya vitu vyake kesi inaunguma. Nikiupata huo uzi ntatupia link.
 
Nafikiri kuna sababu kuu mbili, ya kwanza ameisema Bonesmen kuwa urahisi wa upatikanaji wa chakula.
Pili, ujenzi wa nyumba nyingi za polisi ni wa mabati na wengine zile nyumba zao zina ua ambao inawapa uhuru wa kufuga bata kwenye kwa vile ujenzi wa mabanda ni rahisi na nyumba zao hazina wapangaji wengine ambao huenda wasingependa karaha na usumbufu wa hao bata.

Hauwezi kukuta bata wanafugwa kwa kasi hiyo kwenye makazi ya nyumba za kupanga, utagombana na watu bila sababu.

Kingine nafikiri ni usalama, mwizi wa kwenda kuiba bata polisi anatakiwa afanye mahesabu makali sana japo nasikia kuna mwendeshabodaboda amembaka mjeda!!!!!!
we jamaa kwa hiyo licha ya kuiba bata line polisi kuwa kugumu ila mshikaji kaiba uroda wa kamanda
 
Ni Kwa vile kambi nyingi kunakuwa na Maji uhakika ambayo ni bure pia chakula Cha mahabusu kinakuwa cha kutosha yani availability of food ndo inapelekea bata wanashamili mnoo
Kumbe mahabusu ula na kusaza kiasi hicho? Wakishasaza kinachofuata ni familia nyingi za polisi kupishana jikoni kuchukua mabaki ili kuwapelekea bata wao!
 
kweli bhana ! line polisi nyingi wanafuga bata na enzi hizoooo miaka hiyoooooo nimetafuna saaaana line.
 
Muanzisha mada anajiuliza, kwa nini line polisi wafuge bata kwa wingi kuliko viumbe vingine vinavyo fugwa kama kuku, ng'ombe n.k.

Sababu ambazo mimi ninaona ni hizi hapa.

1. Bata hawafi ovyo kwa magonjwa.

2. Gharama za uendeshaji kuwatunza ni nafuu.

3. Upatikanaji wa chakula na maji.

4. Tabia ya kuigana.
 
Ni Kwa vile kambi nyingi kunakuwa na Maji uhakika ambayo ni bure pia chakula Cha mahabusu kinakuwa cha kutosha yani availability of food ndo inapelekea bata wanashamili mnoo
Makes sense. Nimeipenda
 
Back
Top Bottom