Kuna Siri gani Katika miujiza hii?

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
1,583
2,697
Wanajamvi imenilazimu kuanzisha mjadala mzito juu ya watumishi wa Mungu ,kwanza kabla sijaendelea nataka niweke wazi kuwa mimi ni muumini mzuri wa Mungu na ninamwabudu Mungu na siyo mungu, Nadhani mnanielewa hapo.

Sababu ya mjadala huu ni baada ya Nabii Geordavie kuvunja ndoa ya mtu, nabii huyo anadaiwa kutembea na mke wa mtu Pamela Geoffrey aliyekuwa secretary wake, ushahidi mzito uliotolewa na mtoto wa Pamela mahakani unadai kuwa, mtoto huyo alikuwa akimwona mama yake akiingia kwenye gari na nabii huyo na kisha linaanza kutikisika.

Mume wa Pamela pia alionyesha ushahidi wa msg za mapenzi mahakamani ambazo nabii alikuwa akimtumia Pamela kwenye simu ya pamela, hakimu aliridhika na kuvunja ndoa, soma zaidi habari hiyo hapa: globalpublishers/nabii geordavie avunja ndoa ya mtu. com
Hoja yangu hapa ni kuwa, hawa watu hata Yesu alisema kuwa siku ya mwisho atawakataa, Mathayo 7:22.

Wengi siku hiyo watakuja kwangu wakisema, BWANA tulifanya unabii kwa jina lako, Na kutoa pepo kwa jina lako, Nami nitawajibu.

Ondokeni kwangu nyie watenda maovu.
Hawa manabii feki wanatoa wapi uwezo wa kuombea wagonjwa na wakapona? au jina la Yesu hata kama likitamkwa na mwenye dhambi linafanya kazi? Na utajiri huo wanautoa wapi wakati hawafanyi biashara yoyote?

Nini chanzo cha miujiza hiyo na siri yake ni nini?

CC:mshana jr ,mzizimkavu, rakims na wadau wengine tujadili hili jambo, hawa watu ni hatari na wamevunja ndoa nyingi za watu na mbaya zaidi wana wafuasi wengi balaa. ni yaleyale ya Joseph Kibwetere wa Uganda ambaye hadi leo hajulikani alipo baada kuua wafuasi wake wote.
 
Last edited by a moderator:
Mleta mada hili sio tatizo la hawa manabii na mitume wa kizazi cha dot com, dini zote tangu kuanza kwake mambo ndio haya. Ndio maana mimi huwa sishangai kuona msahafu umeandika karatasi nyingi za binadamu kuwaua wenzao kama Mungu alivyoagiza, yaani Mungu anaamuru jeshi lifyeke na kuangamiza watu!

Huyo nabii anatimiza maandiko matakatifu,maana yameandikwa humo.
 
ni mtihani kwa kweli,lakini hayo yooooote yasitukatishe tumaini letu kwa Mungu.
 
Endelea kutenda mema ili uwe karibu na Mungu na lolote atakalo litafanyika kwako nawe utakuwa na Amani ya Bwana siku zote hata ...ujapopita katika bonde la uvuli wa mauti hutaogopa mabaya... Waache wanaokimbilia short cut ways of solving their problems wakawekewe mikono na mwishowe wanawekewa dus......!!!
 
Ila kumbuka tumetahadharishwa kujihadhari na manabii wa uongo. Nabii wa kweli haendi kinyume cha mapenzi ya Mungu. Tofauti na hapo ni lazima tulitilie shaka jambo hilo isije ikawa lile alilotutahadharisha Yesu.
 
hayo yote hayanabudi kutokea kwani ni dalili kuwa ule mwisho unakaribia
 
Wanajamvi imenilazimu kuanzisha mjadala mzito juu ya watumishi wa Mungu ,kwanza kabla sijaendelea nataka niweke wazi kuwa mimi ni muumini mzuri wa Mungu na ninamwabudu Mungu na siyo mungu, Nadhani mnanielewa hapo.
Sababu ya mjadala huu ni baada ya Nabii Geordavie kuvunja ndoa ya mtu, nabii huyo anadaiwa kutembea na mke wa mtu Pamela Geoffrey aliyekuwa secretary wake, ushahidi mzito uliotolewa na mtoto wa Pamela mahakani unadai kuwa, mtoto huyo alikuwa akimwona mama yake akiingia kwenye gari na nabii huyo na kisha linaanza kutikisika.
Mume wa Pamela pia alionyesha ushahidi wa msg za mapenzi mahakamani ambazo nabii alikuwa akimtumia Pamela kwenye simu ya pamela, hakimu aliridhika na kuvunja ndoa, soma zaidi habari hiyo hapa: globalpublishers/nabii geordavie avunja ndoa ya mtu. com
Hoja yangu hapa ni kuwa, hawa watu hata Yesu alisema kuwa siku ya mwisho atawakataa, Mathayo 7:22.Wengi siku hiyo watakuja kwangu wakisema, BWANA tulifanya unabii kwa jina lako, Na kutoa pepo kwa jina lako, Nami nitawajibu. Ondokeni kwangu nyie watenda maovu.
Hawa manabii feki wanatoa wapi uwezo wa kuombea wagonjwa na wakapona? au jina la Yesu hata kama likitamkwa na mwenye dhambi linafanya kazi? Na utajiri huo wanautoa wapi wakati hawafanyi biashara yoyote?
Nini chanzo cha miujiza hiyo na siri yake ni nini?
CC:mshana jr ,mzizimkavu, rakims na wadau wengine tujadili hili jambo, hawa watu ni hatari na wamevunja ndoa nyingi za watu na mbaya zaidi wana wafuasi wengi balaa. ni yaleyale ya Joseph Kibwetere wa Uganda ambaye hadi leo hajulikani alipo baada kuua wafuasi wake wote.
Mwayachunguza sana maandiko mwadhani mnauzima ndani yake, neno huua lakini roho huuhisha.

Ndugu njia za Mungu hazichunguziki hata kidogo. Agizo la kuu liko mathayo 28 ambalo ni, Nendeni mkawafanye mataifa wote kuwa wanafunzi wangu.

Mungu analitazama neno lake apate kulitimiza, lakini Mungu hamsikilizi mwenye dhambi. Vyovyote utakavyokuwa, kama unalifahamu neno na ukalitamka Mungu atalitenda kwasababu ameahidi kulitenda ila wewe utabaki kama ulivyo(quotation yako ya wengi watakataliwa siku ya mwisho)

Kitu kingine, Mungu anathamini sana roho za watu. Either wewe unafanya kwa hira au la, yeye anawatu wake ambao wako wanakusikiliza ambao kupitia wewe watamuona Mungu, na hawajichanganyi kama wewe.

Kwa hiyo ndugu, hiyo isikupe shida sana, ndio maana kuna roho mtakatifu anayezungumza, kufundisha na kuelekeza nini cha kufanya. Kama uko vizuri wala hautapata shida kwasababu atakuongoza usali wapi au ubaki pale pale kwa msaada wa roho zingine.
 
Back
Top Bottom