MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 714
- 1,137
Siasa za Tanzania zinabadilika kwa kasi ya ajabu. Hazitabiliki hata kidogo. Magifuli kazibadilisha mpaka zinawachanganya CCM wenyewe mpaka wapinzani.
Kuna wana CCM walikimbia chama chao na kujiunga na upinzani kwa jinsi chama chao kilivyokuwa kikiongozwa.
Cha kushangaza baadhi ya wabunge wameacha ubunge wao na kurudi kwenye chama chao cha zamani. Japo upinzani unadai kuna kununuliwa kwa baadhi yao, lakini kuna cha kujifunza. Mtu kama Pauline Gekuru sikuamini kama angeacha ubunge na kurudi CCM.
Siasa za nchi hii zimebadilika sana. Kuna uwezekano siku zijazo wabunge na wanachama wengi wenye usjawishi ndani ya upinzani wakajiunga na CCM siku zijazo.
Ni kutokana na ukweli huo siku moja sintoshangaa kumwona mzee Edward Lowassa akipewa nafasi ya kugombea urais baada ya Magufuli kuondoka. Hili linawezekana sana kwani tayari njiani zimesha anza kunyoshwa kwani akina Mallya, Mollel, Kalanga, Gekuru, Mtatiro, Kantambi, Mwita, Machali, Kafulila, Professor Kitilya Mkumbo, Anna Mgwira, Kisandu, madiwani wasio na idadi walisharudi kusafisha njia.
Inawezekana kabisa Lowassa, Sumaye na Nyalandu na wengine wengi wakarudi kwao CCM siku wakipewa uhakikisho wa wayatakayo huko CCM.
MAGUFULI kaanza kuonyesha njia kwa kuwateua waliokuwa CCM wakaenda upinzani kisha wakarudi tena nyumbani kwao waliko zaliwa na kukulia CCM.
Kwakuwa Lowassa alizaliwa huko na kukulia huko haitashangaza sana akirudi nyumbani kwao. Mtu akirudi kwao siku zote hupokelewa kwa furaha kubwa hata kama alitoka kwa kuiba, kutukana au kugombana. Nyumba hata kama ina mfugo huchinja ili kumfanya mtoto ajihisi yuko salama.
Kuna kisa kwenye Bible sikikumbuki vema cha mwana mpotevu alivyorudi na kufanyiwa sherehe kubwa mpaka mtoto mtiifu kwa baba yake akajisikia vibaya kwa kutopewa thamani kama yule mtoto mtukutu.
Ndio maana kwa kadhia hii kuna CCM asilia na kindakindaki wanajiskia vibaya sana kuona akina Mwita et al wakipewa vyeo pamoja na usaliti wao waliounyesha kwa kukihama chama na kukinanga vibaya sana wakati wakiwa upinzani.
Siasa ni game kama game zingine hivyo usiweke mapenzi ya kudumu huko kwa wanasiasa kwani kuna siku watakishangaza mpaka utaumwa. Hawaaminiki hata sekunde moja.
THEY TALK THE TALK BUT DON'T WALK THE TALK.
IN POLITICS TRUST NO BODY AND SUSPECT EVERY BODY.