Use your common sense to think!!Pamoja na yanayoendelea nchi, nikili kuwa kwenye jeshi letu kuna shida kubwa sana.
Nimekuwa nikijiuliza sana, je tuna jeshi kweli, tuna polisi wenye weledi, au ni vibwengo tu? Unaambiwa kuua na unatii tu.
Kwa mtazamo wa kimataifa, amri inayokwenda kinyume na sheria haipaswi kutekelezwa. Kwa hiyo, si kosa kukataa amri ya mkuu kama amri hiyo ni haramu au inavunja misingi ya utu. Askari au polisi wana wajibu wa kufikiri, kuchuja, na kulinda raia, si kutekeleza kila kitu.
Swali kubwa linabaki: tatizo linaanzia wapi? Je, ni kwenye mchakato wa uajiri (recruitment) ambapo watu wasio na uwezo wa kufikiri kwa kina wanachukuliwa (Machawa) na kuingizwa kwee jeshi letu? Au ni mfumo wa mafunzo na uongozi unaowafinyanga watu kuwa watendaji bila akili zao?
Kwa hali ilivyo, inaonekana kabisa kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimejaa vilaza, watu wasiokuwa na maadili ya kazi wala uwezo wa kubeba majukumu makubwa ya kulinda raia. Ndiyo maana swali hili linaumiza kichwa: je, ni kosa kukataa amri ya mkuu inayokwenda kinyume na sheria? .
Tukubali kwamba, nchi inahitaji reformation kubwa sana, karibu katia kila taasisi.
Kuendelea kuwepo kwa Samia madarakani,ndio ucheleweshaji wa mabadiriko hayo, na nchi yetu itaendelea kuteseka sana. Miezi michache inayokuja, Tanzania itakuwa hali ngumu sana. Kumbuka haya maneno.
Watanzania, hii hali sio shwari, achana na wanaojitoa akili zao, huku wakitumia mgongo wa dini, kwamba watu wanamkataa Samia kisa dini yake, ni sababu za kipuuzi, na ni wapumbavu.
Watanzania wote ni ndugu, haijalishi wewe ni Mkristo au muislam, au kabila lolote, tuwapuuze hawa mapumbavu wanaotaka kuwatenga watanzania.
View attachment 3511365