Wanabodi, napata shida sana na kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu. Katika nchi yetu kuna shida gani kubwa inayopelekea institutions ambazo zipo kisheria kushindwa kusimamia sheria.
Nchi Jirani kama hapo uganda tunasikia vyombo vya habari vimekataa kutangaza habari za kumpendelea Rais Mseveni vikisema kufanya hivyo wakati wa uchaguzi ni kukiuka sheria, Jana tumesikia tume ya uchaguzi ya Uganda imelionya jeshi la polisi kutowazuia wagombea wa upinzani kufanya kampeni.
Hapo Kenya tulisikia mahakama imefuta matokeo ya uchaguzi wa Rais, Malawi tulisikia Mahakama imesema mpinzani ameshinda uchaguzi.
Hivi hizi institutions za Tanzania zina mapungufu gani hasa, hawa wateule wanaongoza hizo tasisi wanazo sifa kweli za kusimamia sheria sawasawa na walivoapishwa.
Haya yaliyokea kwa wabunge wa chadema yanaashitia nini kuhusu uadilifu wa taasisi zetu hizi, nini hasa msingi wa hayo yote. Ninaomba wajuzi wa mambo haya watudadambulie tuweze kuelewa kuna tatizo gani.
Inakuwaje spika anaapisha wabunge nje ya ukumbi wa bunge kinyume na katiba yetu ambayo ameapa kuilinda. Kwani hatuna vyombo vyenye mamlaka ya kulinda katiba yetu ili viweze kuchukua hatua kwa kukiukwa katiba mchana kweupe kabisa.
Sisi watanzania wa kawaida hatuelewi kumetokea nini sasa hivi. Wote tumeona polisi wakiwa wameshika mabegi ya kura za wizi, hivi karibu wakati wa uchaguzi wameishia wapi wale waliokuwa na yale mabegi. Kuna shida gani hasa katika hiki chombo kinachoitwa jeshi la polisi.
Kwanini halisimamii sheria kama inavotakiwa.mifano iko mingi ya kutosimamia sheria, kuna tatizo gani kama IGP amekula kiapo cha kulinda katiba na sheria za nchi, kwanini hayo ya nafanyika na hachukuwi hatua zozote.
Naomba kutoa hoja
Muhanila