Tee Bag
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 7,220
- 5,627
KUNA PERSECUTION NA PROSECUTION
BOBI Wine alipohojiwa na Al-Jazeera akiwa Marekani hivi karibuni alisema alichofanyiwa Uganda kilikuwa Persecution kuliko Prosecution. Naam, Persecution ni Mateso na Prosecution ni Mashitaka.
Katiba ya Tanzania, Ibara ya 13 (6) kifungu (b), inasema; ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mwenye kosa hilo mpakaitakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosahilo.
Sheria ya Makosa ya Jinai Tanzania ibara ya 50 (1), inataja kipindi ambacho polisi wanaruhusiwa kumshikilia mtu kwa mahojiano ya kipelelezi ni muda usiozidi saa 4. Ibara ya 51, inaeleza kuwa kama polisi wanaona saa 4 hazikutosha, watamtaarifu anayeshikiliwa ili kuongeza saa 4 nyingine. Baada ya hapo, kama wataona bado kuna ulazima wa kuendelea kumshikilia, wanapaswa kwenda mahakamani kuomba kibali cha hakimu.
Ibara ya 51 (2), sheria hiyo inasema; polisi hawatakiwi kuongeza kipuuzi muda wa kumhoji mtu au kwa lengo la kumuudhi. Na anayehojiwa zaidi ya muda uliotajwa anaweza kudai fidia.
Kuhusu dhamana ni haki ya mshitakiwa. Sheria ya Makosa ya Jinai, ibara ya 64 (1) kifungu (C), inasema, polisi wanapaswa kumwachia huru mtu waliyemkamata baada ya saa 24, ikiwa hakuna mashitaka yaliyofunguliwa, isipokuwa kama afisa polisi anayehusika anaamini kosa kubwa limetendeka.
Najiuliza kuhusu Shaffy Dauda, Soudy Brown, Maua Sama na wengine wote ambao wana wiki nzima tangu walipokamatwa kwa makosa yenye kuhusika na mitandao.
Dauda, Soudy na wengine; kosa lao ni kuendesha akaunti za YouTube (Online TV), Tovuti na Blogs bila kusajili.
Maua na Soudy; kuposti video mtandaoni, video ambayo inaonesha watu wakichezea fedha za Tanzania.
Unamkamata mtu kwa kosa la kumiliki akaunti ya mtandao bila kusajili.Unamkamata mtu kwa kupost video yenye maudhui yenye kuvunja sheria. Halafu unamshikilia wiki nzima bila dhamana wala kumfikisha mahakamani. Unapeleleza nini sasa?
Ndiyo kusema sheria za nchi zinavunjwa ili kushughulikia watuhumiwa. Hii siyo Prosecution ni Persecution. Kukamata kwanza halafu upelelezi unafuata.
Polisi, TCRA na vyombo vyote vya mamlaka ya nchi, vinapaswa kufanya kazi kwa misingi ya kuijenga hii nchi. Si kukomoana.
Ndimi Luqman MALOTO