Kuna nini TRA Mwanza na Ukamataji Hovyo Wa Magari?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,798
71,218
Kwa siku kadhaa jiji la Mwanza limekumbwa na zoezi linaloendeshwa na TRA kwa kushirikiana na Madalali.
Jambo la ajabu magari yanayodaiwa hayajalipia motor vehicle licence wengi wanazo nyaraka zinazoonyesha wamelipia NMB au CRDB lakini katika system ya TRA hazionekani. La ajabu wao hawataki kuchunguza ni kwanini hali hiyo inajitokeza wao wanataka ulipe tuu. Hizo pesa zinaingia wapi kama system yao haionyeshi?na mbona hawana mpango hata wa kuchunguza hilo? Huku kulipishana mara mbili ni kuwaibia wananchi. Watoe ufafanuzi.
 
Hali ya nchi ni mbaya. Hata kwa kudhulumu, lazima pesa ipatikane.
Ok,sasa kama fedha zimelipwa benki na hazipo katika system ya TRA zinakwenda wapi? Na kwa nini maafisa wa TRA wana ignore swali hili wanapoulizwa? Na hili nimeambiwa sii Mwanza tuu



Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom