Kuna nini TBL? Ajira za wazawa mashakani

Blasio Kachuchu, Ownership ya TBL ikoje?

Hao wageni wanapataje vibali vya kazi kama Watanzania wanaoweza kufanya hizo kazi wapo?

Tz imekosa vijana wenye ubunifu na hapohapo ana nidhamu ya kazi. Vijana wamejaa tamaa, wizi na uvivu......

Mtu akipata madaraka rushwa za ngono kwa dada zetu kupata ajira zinatamalaki.....

Hatuna spirit ya kazi kama wa kenya
 
Kuna mtu hapo anaitwa wa pr. Ni mtu hatari sana maana ndio anakwenda kuhonga maigresheni ili hao wenye pua ndefu wapate vibali vya kufanya kazi. Huyo ni mpini anaisaidia shoka kukata miti. Adui wa mtanzania ni mtanzania kwani hiyo mikaburu ilialikwa na watanzania.
 
Siku si nyingi zilizopita niliingia duka moja la simu za tecno, sijui kama linamilikiwa na Mtu binafsi au kampuni ila pale wanauza simu za tecno tu.

Niliwakuta Wadada wawili, hawakuchangamka kabisa nikawa nauliza maswali mmoja wao akawa ananijibu tena kwa mkato, baadae walinipotezea kabisa na wakaanza kupiga stori zao wao kwa wao nami nikiwa hapo hapo, na nilikuwa Mteja peke yangu kwa wakati huo.

Ilibidi tu niondoke nikiwa na maswali mengi kichwani na kuwasikitikia wenye duka lile ambao wanajua wana Wafanya kazi.

Waswahili hawajali kazi kabisa hata kama wamesomea, na bado mwisho wa mwezi wanatarajia mshahara.
 
Serengeti Lite inaifanya TBL isiwe vizuri ipumue shida..yani kama vile Pepsi walivyokuja kuifunika Coca Cola..
Mkuu kuwa serious basi. Serengeti wao wanatengeneza pombe wakati TBL wanatengeneza bia. Hii tofauti huwezi kunielewa nini namaanisha.

TBL ni inauza mpaka nje ya nchi wakati Serengetiwao ni hapa bongo tu.
 
Mkuu PR TBL wapo wawili Director yule dada nshomile aliyetoka Vodacom Georgia na Zenna ni yupi mchawi hapo uliyemsema
Kuna mtu hapo anaitwa wa pr. Ni mtu hatari sana maana ndio anakwenda kuhonga maigresheni ili hao wenye pua ndefu wapate vibali vya kufanya kazi. Huyo ni mpini anaisaidia shoka kukata miti. Adui wa mtanzania ni mtanzania kwani hiyo mikaburu ilialikwa na watanzania.
 
Wakati serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya viwanda kufanikisha ajenda yake ya Tanzania ya viwanda, bado kuna dalili za sekta hiyo badala la kukua na kuwainua Watanzania baadhi ya makampuni yana muelekeo wa kuwakandamiza wafanyakazi wake Watanzania na kunufaisha raia wa kigeni.

Moja ya kampuni kubwa nchini ambayo hivi sasa inawanyima fursa wafanyakazi wake wazawa, wasomi na wenye uzoefu wa kazi na kukumbatia wageni ni Tanzania Breweries Limited (TBL), chini ya kampuni ya ABInBev.

Kampuni imefikia hatua ya kuajiri raia kutoka Afrika Kusini kuongoza vitengo vya Logistic, Mauzo na Masoko, wakati kuna Watanzania wengi wengi ujuzi na uzoefu wa fani hizo. Jambo la kujiuliza raia wa kigeni ambaye hata hajui jiografia ya nchi hii atawezaje kusimamia uuzaji wa bia katika mikoa, wilayani mpaka vijijini ambako wapo watumiaji wa bidhaa za kampuni?

Mbona kuna makampuni mengi nchini kama Azam, MO, viwanda vya soda nk. unakuta bidhaa zake zinapatikana mpaka vijijini na kazi ya usambazaji na masoko inafanywa na watanzania?na hata TBL inao wenye ujezi. Suala la kuuza bia ndilo waswahili wanaonekana hawana uwezo, wageni wanaotambua maeneo kwa kutumia ramani za Google ndio watajua? au kuna ajenda ya siri ya kuua viwanda na kutorosha fedha nje ya nchi kwa urahisi?

Baadhi ya wafanyakazi wa kigeni TBL, ambao wamekabidhiwa jukumu la kuongoza vitengo wakati watanzania wenye sifa na ujuzi wa kufanya kazi hizo ni Lise Kruger (Afrika ya Kusini)-Logistic Director, Doreen Tumureebile (Afrika ya Kusini)-Mkurugenzi wa Mauzo,na Uendelezaji wa Masoko,Bruno Zambrano, amekuwa akifanya kazi kama Mkuu wa Kitengo cha fedha japo amekuwa akitambulishwa kama Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara .Pia yuko Mkurugenzi wa Masoko , Neil Hobkirk, ambaye amekuwa akifika nchini mara kwa mara kama mtalii kufuatilia masuala ya masoko kama vile hapa nchini hakuna mtu kwa kufanya kazi hizo.

Swali la kujiuliza wageni kama hawa ambao wanakuja kufanya kazi zinazoweza kufanywa na watanzania nani anawapatia vibali vya kufanya kazi nchini?.Uhamiaji mko wapo? NBAA mkoa wapi?

Wakati umefika wa Serikali kuwa macho na wawekezaji ambao wanaangalia zaidi maslahi yao na kukandamiza watanzania, na kuwakatisha tamaa sambamba na kuua taaluma zao.

Baadhi ya wawekezaji wanakuja na kivuli cha uwekezaji wakati wanafanya ulaghai na kunufaika na raslimali walizozikuta, mfano mwekezaji anayeendesha kiwanda hiki tangu aingie nchini amekuwa akiongelea suala la kujenga kiwanda cha bia mkoani Dodoma, lakini hadi sasa hakuna chochote kinachoendelea.
Mkuu umechunguza kupata taarifa ya umiliki wa hiyo kampuni? yaani nani ni major shareholder? ok ukishajua hilo mmilikiwa kampuni huajiri watu kwenye vitengo kulingana na unyeti wa kitengo hicho, profession, experience na mengineyo
 
Baada ya kuangalia vizuri management ya TBL nadhani kwanini wanaletwa wageni sababu mwenye Mali wa Sasa baada ya Kuuzwa Sabmiller na kununuliwa na AB Inbev hataki masihara kwenye profit optimization.

Wabongo wengi tuna ukakasi kwenye kutenda kazi angalia mabosi wa kibongo Wana vyo abuse vyeo deal nyingi, kazi Hana.

Ukiangalia watu uliwataja akina Bruno hiyo ni degree ya Texas mzee degree sio ya mil 2. Work attitude, problem solving etc

Doreen University of Kwazulu Natal na was a good performer. Mhamiaji huyo katoka Rwanda kaenda Kusoma SA. Alikaza kweli mpaka kupata u sales manager SA breweries Tena mgeni sio kichwa maji.

Kwa ufupi ni utendaji wenye Kasi ndio unawapa hizo nafasi plus all the benefits. Mwisho wa siku wanatakiwa wa break even the given target Sasa mbongo shelukindo mpaka atoke Mbweni kaamka nazo kichwani ataweza kuwaburuza mfikie Target kweli na technology pia wabongo hatujui ku apply kazini.
 
Chukua mfano TPC ( Twiga cement) haifi na Haina upuuzi sababu wazungu wenyewe Heidelberg wako top Hali kadhalika Lafarge mbeya cement inaiza mpaka DRC cement, TPC Moshi sukari unauzwa mpaka Abi Dhabi ukiangalia deep down makaburu wenyewe wametulia wanapiga kazi na Bata leeefu Kama mama dangote
 
Sisi no wezi, sisi sio waadilifu. Hata ingekuwa mimi nisingewaajiri. I'm sorry but that's how it is.
 
Wao wana hisa nyingi hivyo kuwafanya wawe na sauti na maamuzi, na kuamua nini afanye nani na wamlipe vipi.

Huwezi kuwa na hisa nyingi halafu wakurugenzi waendeshaji ukawapa watu baki usio wajua.

Siku zote ukiwa na hisa kubwa au ukimiliki kiwanda au biashara vitengo muhimu utawapa watu unaoweza kuwa tawala na mnaelewana.

Hao wamiliki sio wendawazimu wakupeni nyie idara nyeti, wao huchaguana huko huko S.Afrika na kuwaleta, na hufanya vikao vyao nyeti huko huko na hutoka maamuzi huko huko, wakifika Tanzania ni utekelezaji tu.

Mkipewa nyie mnaiba, mpaka leo kuna kesi za wanahisa mahakamani.

Wawape mamlaka tena muanze ku mismanage kampuni?!

Nyie mnaweza ulinzi na kulewa basi.
 
Ukifanya Kazi na makaburu piga hasa kama una nafasi, hata wao ni wezi wazuri tu hawajaja all the way from SA kuremba, kwanza wana tabia Ya kujilipa mishahara mikubwa Sana tofauti na wazawa.
 
Kwa kweli kampuni za TBL chini ya AB-inbev wafanyakazi wamekuwa watumwa hawana raha, maslahi kwa Sasa siyo mazuri, viongozi wa kampuni ambao ndiyo wazawa wa nchi wako radhi kuwakandamiza wafanyakazi kwa lengo la kuwafaidisha wageni.
Uwepo wa kiwanda ni kwa faida ya wazawa wa nchi husika.
Kwa kweli serikali ya wanyonge ijaribu kuangalia mazingira ya wafanyakazi wa TBL.

Fanyeni kazi
 
Nadhani Shana ya Ubebari hujaijua vizuri maana yake maskini mfanyakazi anyonywe Sana na tajiri apate kingi.

Management wanalipwa mpaka bonus Kama watapunguza Operational cost, Hii inaingia mpaka kwenye overtime zenu wafanyakazi, compensation etc

Nilisikia watu wa sales Wana operate under zero budget siku hizi baada ya Inbev kuingia zile shobo za ma pickup ya TBL kuunguruma Air con huku sales rep anapiga story na mteja zimekwshia aliondoka nazonJakaya.

Pigeni kazi mkipata faida Basi mtagawana bonus.
Kwa kweli kampuni za TBL chini ya AB-inbev wafanyakazi wamekuwa watumwa hawana raha, maslahi kwa Sasa siyo mazuri, viongozi wa kampuni ambao ndiyo wazawa wa nchi wako radhi kuwakandamiza wafanyakazi kwa lengo la kuwafaidisha wageni.
Uwepo wa kiwanda ni kwa faida ya wazawa wa nchi husika.
Kwa kweli serikali ya wanyonge ijaribu kuangalia mazingira ya wafanyakazi wa TBL.
 
Back
Top Bottom