Kuna nini tanesco kilimanjaro?

Kuna nini tanesco kilimanjaro?

RC.

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2012
Posts
444
Reaction score
43
Ndugu zangu wanajamvi,kwanza kabisa poleni na majukumu!ktk ziara zangu za kikazi,katika mkoa huu wa Kilimanjaro,nimepata wakati mgumu sana kitekeleza majukumu yangu ya kikazi kwasababu ya tatizo la kukatikakatika kwa umeme hususani wakati wa saa moja na nusu na saa mbili kamili usiku,tatizo hili limekuwa sugu mpaka linakera,hatujui tatizo ninini? Waziri wa nishati na madini amelitangazia taifa kuwa hakuna mgao wa umeme,sasa iweje huku umeme ukatekate bila sababu za msingi halafu TANESCO wako kimya?na hata kama ni marekebisho ya mitambo kama wanavyosingizia ndio iwe kila siku?au kunasababu yoyote ya maana ambayo imekuwa sugu kwao kulitatua?au ndio hujuma kwa majimbo yote yanayoongozwa na upinzani tuadhibiwe ili tuchukie upinzani? Na kama tatizo ni miundo mbinu mibovu kwanini mkurugenzi asjiuzulu kabla hasira za wananchi kumuangukia na kumchoma moto humo ofisini?tatizo hili limedumu kwa mwaka sasa,huku likichafua hali ya hewa kwenye familia,mioyo,na nafsi za watu na ktusababishia pressure kwa hasira tulizo nazo kwa TANESCO?Naomba mtambue kuwa mnyonge unapomwonea ujue ipo siku atajikakamua na kutumia kila mbinu ili akushinde! NARUDIA TANESCO KERO HII INACHAFUA HALI YA HEWA KTK MIOYO NA NAFSI ZA WATU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Naomba mtutatulie hili tatizo kabla hatujaingia mabarabarani kama watu wa MTWARA MUGU IBARIKI NCHI YANGU!
 
Back
Top Bottom