Kuna nini Old Moshi high school

Toxicer

Member
Joined
Jul 6, 2013
Posts
42
Reaction score
0
Kwa aliyechaguliwa hapo form5 2013 jaman tuwasiliane kupitia 0758949340.
 
Old moshiiii... My school... I luv the school.. Unaenda combination gani kijana??? Kama pcm utamkuta gwiji la namba..mr. Kinunda.... Mpe salamu zetu sana...

Me nimechaguliwa pale Pcb vp lakin mazingira hiyo combination hapo ? Na je nilazima kwenda prepo kila siku au?
 
Mkuu vp uazimishaji wa vitabu shuleni vipo vya kutosha? Hasa vya phys, Chems &bios!
 
Me nimechaguliwa pale Pcb vp lakin mazingira hiyo combination hapo ? Na je nilazima kwenda prepo kila siku au?

Mazingira ni mazuri... Hayana shida... Waalimu wa biology kipindi naondoka walikuwepo.. Hata chemistry waliletwa.. Physics ndio sina uhakika..maana niliskia mwalim msami a.k.a pdidy amepandishwa cheo na kua mkaguzi.. Huyu ndo alikua gwiji la physics balaa... Alinisaidia sana kupata A ya physics bila hata tution.sasa sijui kama kuna waalimu wengine wameletwa..ila mazingira ya shule sio mabaya.... Prep kwenda ni wewe mwenyewe... Hakuna ulazima..taa zipo on usiku kucha.. Sio kama seminari.. All in all.. Sijawahi kuenjoy maisha ya kusoma sekondari zaido ya oldmoshi.. Ma hata matunda yake mwisho wa form six yalikua mazuri kwangu
 
Me nimechaguliwa pale Pcb vp lakin mazingira hiyo combination hapo ? Na je nilazima kwenda prepo kila siku au?

Hamna atakaye kilazimisha kwenda Prepo...Ila!!! Kama ni kukesha utakesha bila kupenda....

Mazingira ni tulivu sana na majirani zenu ni Mucoobs...

Mabweni ya Hanang na Meru yako poa sana...
 
kijana pale ni hakuna kulala ni msuli kwenda mbele.... nenda kajisahau ulale utavuna chako.....ulichopanda ...kasome kijana ....msuli yatima pale ndo utakutoa lasivyo..... ukifika msalimie mzee Omy

Mzee Omy bado yupo aisee na jiko lake...
Mzee Chami yupo sana na Mana Recho kama kawaida yao...Nilitoka hapo majuzi...
 
Inaelekea ulikuwa mzee wa Kitandu sana kunywa mbege na kuzamia harusi hapo Ushirika...
 
Old moshiiii... My school... I luv the school.. Unaenda combination gani kijana??? Kama pcm utamkuta gwiji la namba..mr. Kinunda.... Mpe salamu zetu sana...

Kinunda! dah, unanikumbusha mbali sana mkuu, nilikua namkubali sana mzee PDD (Msamy) kwenye suala zima la physics ila siku hizi amekua mkaguzi.
 
kijana pale ni hakuna kulala ni msuli kwenda mbele.... nenda kajisahau ulale utavuna chako.....ulichopanda ...kasome kijana ....msuli yatima pale ndo utakutoa lasivyo..... ukifika msalimie mzee Omy

Dah, mzee Ommy... nakumbuka peregee. Kuna mwalimu wa chakula alikua anaitwa Lisapita sijui bado yupo?

Toxicer, Kuhusu mambo ya prepo hiyo ni wewe tu, hakuna mtu ana time na wewe,shule iko very free, ukiamua kuishi mtaani, sawa, ukiamua kushinda library ya town sawa, ila kilichokua kinanikera ni kulazimishwa kurudi darasani baada ya chakula cha mchana na waalimu kulipwa kama hela ya ziada. Tulikua tunatozwa mchango wa lazima elfu 10 ila niliwahi ongoza mgomo 2003..
 
Kuna yule mama wa chem bd yupo?

Na yule alipandishwa cheo, si alikua anafundisha PCM Chemistry? nilishawahi kuwa na mgogoro nae kisha tukaweka sawa baada ya kuwa nawasainisha daftari la kufundisha masomo ya ziada jioni.
 
Kinunda! dah, unanikumbusha mbali sana mkuu, nilikua namkubali sana mzee PDD (Msamy) kwenye suala zima la physics ila siku hizi amekua mkaguzi.

Vp maticha wa tuitionz moshi mjini wanapatikana kwa upande wa Phys , Bios and Chems??????
 
Mzee Omy bado yupo aisee na jiko lake...
Mzee Chami yupo sana na Mana Recho kama kawaida yao...Nilitoka hapo majuzi...

nilitoka hapo 2009, na mwaka jana mwishoni nilipitia gamba langu, mazingira ni yaleyale ila waliongeza michepuo ya arts, kwa sasa h/m anaitwa Angalo aliyekuwa anafundisha physics kinunda still yupo na hajaacha mkawara wake.
Inspecta chami yupo pia
kwa upande wa accademic dogo nikwambie pale ni wewe na akili kichwani, ukitaka kusoma utatoka, ukiwa mpenda starehe hakuna wa kukufuatilia.
Walimu wapo wa kutosha na wanahudhuria vipindi bila kudoji ila hawana time y kumfuatili mwnafunzi kama ameingia darasani au la
pia kuna maabara tatu za physics chemistry na biology na practical ni kila wiki.
"ONGOZA VYEMA ANGAZA"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…