kuna nini kichwani mwa mke wangu

Mkuu mimi mdogo wangu ni handsome balaa halafu pia ni mpole, Mimi ni exactly the opposite (i.e Ugly and well, na mkali pia). Na mara nyingi kama sio zote wale ma-gf wangu wanayekutana naye kwa mara ya kwanza kwa kweli huwa anawachanganya sio polepole. Sasa unajua mimi huwa nafanya nini? Yaani kwanza honestly hicho kitu huwa hakiniumizi kichwa hata kidogo, kwa sababu kwa kweli, msichana wangu akianza tu kuwa dah unajua mdogo wako sijui hivi au vile, mimi sasa ndio anakuwa kama amefungua encyclopedia ya sifa za dogo, kwa sababu nitamwaga sifa lukuki hapo hadi mwenyewe atabloo. Halafu sio kwamba namwaga kwa kinyongo, yaani ni kwa moyo mweupeeeeeeeeeeee. Mara zote huwa hawarudii tena hizo habari.

mkuu hii nitaifanyia mazoezi na kuitumia
nadhani kuna kitu na kosea ndio maana kula sana hivi nyimbo za sifa kwa dogo.
ulichosema kinafafana lakini inasikitisha sana maana dogo yeye bado mbichi
wakina mama/dada hapo watakuwa hawafanyi haki mbona mimi sifanyi hivyo
 
usimwambie mkeo juu ya mawazo yako sbb;
..ukimwambia kama kweli wana lao jambo itakuwia vigumu kuwagundua sbb watakua makini,
..kama mkeo hana nia mbaya kama unavyomuwazia utamkwaza sana na hatakuwa na uhuru tena na shemeji yake.

..Mdogo wako akijua unamuwazia haya wkt wana upendo wa kawaida tu utamuumiza sana,chukulia mfano ingekua ni ww unahisiwa hlf sio kweli ungejisikiaje?

Wewe unaonkana unampenda sana mkeo,ni jambo zuri,lkn pia unaonekana una wivu sana kiasi hata mkeo akifurahi na nduguyo wa damu unaona unaibiwa.

MUOMBE SANA MUNGU,unaweza hata kufunga siku moja kulikabidhi hili jambo kwa Mungu,yeye anajua zaidi yetu sisi wote,na yeye ndiye atakayekupa jibu.

USIKURUPUKE,wala usianze sijui kuajiri wapelelezi au kuanza kuomba omba watu ushauri huko mitaan,wee kaa kimya,ongea na mungu wako,soma mazingira kimyakimya.

Hebu jaribu kuzigeuza hizo sifa kuwa ni kitu positive hadi pale utakapoona dalili inayowasha taa nyekundu,kumbuka kama kweli kuna kitu kati yao utaona tu siku vikiwakolea,hawataweza kujificha milele.
ukweli mputu
 
pole sana kaka kwa kuwa na hisia hizo najua zitakuwa zinakusumbua sana ndani ya kichwa chako
 
nafikiri mpaka hapa ushapata la kuchukua mawili matatu

nimejaribu hiyo moja ya kumsifia zaidi ya yeye anapomsifia, naona haifanyia kabisa
nakuwa kama nimemmezesha tape
kila sifa ninapoimwaga yeye anaiongezea zaidi na kuweka na ushahidi ya hiyo sifa
nafikilia kumtuma dogo kwa maza kwa muda fulani nione inakuwa je.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom