Kuna nini kati ya maji Uhai na Kilimanjaro?

Kuna nini kati ya maji Uhai na Kilimanjaro?

Mkuu tofauti kubwa iliyopo kati ya product hizi mbili ni potential of hydrogen yaani ph, kilimanjaro ina kiasi kidogo cha acid na base kulinganisha na uhai!
You nailed it mkuu, kilimanjaro wana maintain sana quality.. PH yao ni 7.0 na hata ukinywa unaona kabisa,

sasa uhai kuna label zinaonyesha 7.3 wakati mwingine 7.5 yan hakuna standard na ukiona label tu inakosewa basi jua hata maji yenyewe unaweza kuta ph inafika 9.0 ukipima ndo mana sometimes yanatest kama yana chumvi hivi au yanateleza

Watu wa kipato cha kati kwenda juu ndo wanywaji wakubwa wa kilimanjaro, uhai inauzwa sana uswazi kwasabu ni cheap
 
Kilimanjaro wanafanya viziri nchi nzima. Kanda ya ziwa Jambo na Maisha ndio wauzaji wakubwa. Mbeya, katavi, tabora .a kigoma Dew drop ndo anatesa kwa mauzo. Maeneo ya pwani Azam anasumbua sana.
 
Nimetembea mikoa mingi Tanzania, kasoro Lindi, Mtwara, Shinyanga na Kigoma, mikoa yote upatikanaji wa maji ya Kilimanjaro ni wa uhakika na sijaona maji ya Uhai. Inamaana Uhai imeshindwa kupenya soko la maji mikoani? Huwa najiuliza sana. Uhai utayakuta Moro na Tanga tu. Interest yangu ni kujua tu maana kuna biashara nataka kuanzisha inayofanana na maji.
mkuu kwa lindi, mtwara maji ni ndanda spring tu.
 
Mimi naishi Dar hakuna maji sijawahi kunywa kati ya hayo mnayataja tuache ushabiki Kilimanjaro hayana ya kufananisha..kidogo Ndanda Springs yanafuatia
 
Jambo anakuja kwa kasi sana nae, kanda ya ziwa yote ameshaiteka.
 
Nimezunguka karibia Tanzania yote na kunywa aina mbali mbali za maji. Kilimanjaro anapata endorsement ya Serikali, lakini naye anasubiri kwa Dew Drop, Udzungwa na maji fulani ya Asante yalikuwepo Dom
 
Back
Top Bottom