Kuna nini Ethiopia? ndio nchi ya kwanza kutumia treni ya umeme Afrika kusini mwa Sahara lakini..

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,962
Ethiopia imezindua treni yake mpya ya kutumia umeme ambayo itakuwa imerahisisha sana usafiri nchini humo, pia Ethiopia tunaona shirika lake la ndege lilivyo maarufu na ndege nyingi kubwa
Lakini Ethiopia kumetokea maandamano makubwa ya wananchi kuipinga serikali yao na watu wengi wameuawa wiki iliyopita na serikali kutangaza siku 3 za maombolezo
Pia tunashudia kwenye taarifa za habari raia kadhaa wa ethiopia wakakikamatwa Tanzania wakielekea Afrika Kusini kutafuta maisha
Kuna nini, ina maana serikali inafanya miradi ambayo haiwasaidii wananchi au wananchi wenyewe tu hawaridhiki kama ilivyo kwa asili ya binadamu?
 
Serikali inashindwa kuweka priority ya mambo ya kufanya, wananchi hawatakula treni wala ndege za mapanga, wananchi wanataka maji safi, barabara zinazo pitika, ajira na uhuru wa kuongea na kupata haki zao za msingi
Hata hapa bongo naona tunaelekea huko, ajira umekaa mwaka mzima hujatoa una nunua mapanga boi ni ngumu mwana nchi wa kishapu au matombo au malinyi ulanga huko kuelewa umuhimu wa vitu hivyo, kama hapati maji safi, hapiti kwenye barabara nzuri au hapati elimu bora.
Serikal zetu zijifunze kuweka vipaumbele kwenye mambo ya msingi yanayo saidia wana nchi wa chini.
*sijasema wasinunue ndege, ila kama una nunua ndege ajira hutoi , maji hakuna unakuwa huna maaana vile vile , tangulia vidogo njoo vikubwa
 
Serikali inashindwa kuweka priority ya mambo ya kufanya, wananchi hawatakula treni wala ndege za mapanga, wananchi wanataka maji safi, barabara zinazo pitika, ajira na uhuru wa kuongea na kupata haki zao za msingi
Hata hapa bongo naona tunaelekea huko, ajira umekaa mwaka mzima hujatoa una nunua mapanga boi ni ngumu mwana nchi wa kishapu au matombo au malinyi ulanga huko kuelewa umuhimu wa vitu hivyo, kama hapati maji safi, hapiti kwenye barabara nzuri au hapati elimu bora.
Serikal zetu zijifunze kuweka vipaumbele kwenye mambo ya msingi yanayo saidia wana nchi wa chini.
*sijasema wasinunue ndege, ila jama una nunua ndege ajira hutoi , maji hakuna unakuwa huna maaana vile vile , tangulia vidogo njoo vikubwa
Mimi mwenyewe nahisi hivyo mkuu, maana nchi hii uchumiwake umekuwa kwa kasi sana, lakini wananchi wake taabani
Ni vema serikali ikaangalia maendeleo yake kiuchumi yanaboreshaje welfare ya watu wake
 
Ubaguzi ndio tatizo, unaweza leta maendeleo kwa nchi lakini ubaguzi wa kikabila au maeneo ukaleta shida, ndio kinachotokea huko kuna aina ya watu wa sehemu fulani maendeleo kwao yamesahauliwa pia watu wao hawafaidi keki, masuala ya ajira nyongozi n.k kwa hiyo ni bomu la kutengenezwa mda mrefu.
 
Ethiopia imezindua treni yake mpya ya kutumia umeme ambayo itakuwa imerahisisha sana usafiri nchini humo, pia Ethiopia tunaona shirika lake la ndege lilivyo maarufu na ndege nyingi kubwa
Lakini Ethiopia kumetokea maandamano makubwa ya wananchi kuipinga serikali yao na watu wengi wameuawa wiki iliyopita na serikali kutangaza siku 3 za maombolezo
Pia tunashudia kwenye taarifa za habari raia kadhaa wa ethiopia wakakikamatwa Tanzania wakielekea Afrika Kusini kutafuta maisha
Kuna nini, ina maana serikali inafanya miradi ambayo haiwasaidii wananchi au wananchi wenyewe tu hawaridhiki kama ilivyo kwa asili ya binadamu?
Ngoja nifuatilie but nahisi ikawa haina tofauti na walichokifanya walibya kumtimua na baadae kumuua Gadafi kwa kulaghaiwa na nchi za magharibi.....Jukumu la Serikali ni kuweka mazingira wezeshi ya kijami na kiuchumi na jukumu la wananchi ni kuzalisha jukumu ambalo kwa waaafrika wengi hatulifanyii kazi.
 
Ethiopia siyo ya kwanza Africa
South Africa,Morocco ...nahisi hata Algeria zimetangulia
Ni ya kwanza kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara, kufuatana na BBC
==============================================================================
Treni ya umeme yaanza kutumika Ethiopia - BBC Swahili
Ethiopia imezindua rasmi usafiri za treni ya umeme ya kubeba abiria mijini, ambayo ndiyo ya kwanza katika nchi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.

Treni hiyo itatumika katika mji mkuu wa nchi hiyo Addis Ababa kwenye reli ya umbali wa kilomita 34, ikipita mji huo kutoka kaskazini kwenda kusini.

Mradi huo umegharimu $470 milioni (£300 milioni, ukifadhiliwa kwa kiasi kikubwa na Uchina. Mamlaka nchini humo zimesema mradi huo, utafanyakazi kwa saa 16 na unatarajiwa kupunguza msongamano wa magari barabarani, huku watu milioni moja wakitarajiwa kuutumia kila siku.

Nauli inatarajiwa kuwa chini ya nusu dola kwa kila safari.
Mwandishi wa BBC mjini humo Emmanuel Igunza, aliyehudhuria uzinduzi wa treni hiyo, anasema raia walijawa na msisimko mkubwa na kila mmoja alitaka kuwa wa kwanza kuiabiri
.
150921123531_train_ethiopia_512x288_afp.jpg
 
Ngoja nifuatilie but nahisi ikawa haina tofauti na walichokifanya walibya kumtimua na baadae kumuua Gadafi kwa kulaghaiwa na nchi za magharibi.....Jukumu la Serikali ni kuweka mazingira wezeshi ya kijami na kiuchumi na jukumu la wananchi ni kuzalisha jukumu ambalo kwa waaafrika wengi hatulifanyii kazi.
Libya walikuwa hawana uhuru ndio, lakini wanahama nchini kwao kwenda kutafuta ajira kwingine? hapana
Ethiopia wanakamatwa kila mara wakihamia Afrika kusini
 
Ethiopia imezindua treni yake mpya ya kutumia umeme ambayo itakuwa imerahisisha sana usafiri nchini humo, pia Ethiopia tunaona shirika lake la ndege lilivyo maarufu na ndege nyingi kubwa
Lakini Ethiopia kumetokea maandamano makubwa ya wananchi kuipinga serikali yao na watu wengi wameuawa wiki iliyopita na serikali kutangaza siku 3 za maombolezo
Pia tunashudia kwenye taarifa za habari raia kadhaa wa ethiopia wakakikamatwa Tanzania wakielekea Afrika Kusini kutafuta maisha
Kuna nini, ina maana serikali inafanya miradi ambayo haiwasaidii wananchi au wananchi wenyewe tu hawaridhiki kama ilivyo kwa asili ya binadamu?
Una uhakika? Afrika ya kusini, Tunisia, Morocco etc au ulitaka kusema nchi za sub-Sahara isipokuwa SA
 
Ethiopia imezindua treni yake mpya ya kutumia umeme ambayo itakuwa imerahisisha sana usafiri nchini humo, pia Ethiopia tunaona shirika lake la ndege lilivyo maarufu na ndege nyingi kubwa
Lakini Ethiopia kumetokea maandamano makubwa ya wananchi kuipinga serikali yao na watu wengi wameuawa wiki iliyopita na serikali kutangaza siku 3 za maombolezo
Pia tunashudia kwenye taarifa za habari raia kadhaa wa ethiopia wakakikamatwa Tanzania wakielekea Afrika Kusini kutafuta maisha
Kuna nini, ina maana serikali inafanya miradi ambayo haiwasaidii wananchi au wananchi wenyewe tu hawaridhiki kama ilivyo kwa asili ya binadamu?

One uhakika kuwa Ethiopia nfiyo nchi ya kwanza kuwa na treni ya umeme? Check na Zimbabwe na South Africa.
 
Ethiopia imezindua treni yake mpya ya kutumia umeme ambayo itakuwa imerahisisha sana usafiri nchini humo, pia Ethiopia tunaona shirika lake la ndege lilivyo maarufu na ndege nyingi kubwa
Lakini Ethiopia kumetokea maandamano makubwa ya wananchi kuipinga serikali yao na watu wengi wameuawa wiki iliyopita na serikali kutangaza siku 3 za maombolezo
Pia tunashudia kwenye taarifa za habari raia kadhaa wa ethiopia wakakikamatwa Tanzania wakielekea Afrika Kusini kutafuta maisha
Kuna nini, ina maana serikali inafanya miradi ambayo haiwasaidii wananchi au wananchi wenyewe tu hawaridhiki kama ilivyo kwa asili ya binadamu?
Inatakiwa watu waache fikra kuwa uchumi kuwa juu ni kula bata,nenda uingereza ndio utapata jibu ,ukikaa miezi sita tu utakumbuka Tanzania.Huli bila ya kufanya kazi na kila mtu yuko bize na maisha yake ,hakuna nyumba ya jirani kuomba mboga wala lift ya bure kumpeleka mwanao hospitali kisa anaumwa ni kazi kazi tu,na unatumiwa ipasavyo kiasi cha kwamba hela yote inaishia kulipa kodi.Hakuna mafanikio amabayo yanapatikana kwa kulala jamani lazima tukubali kuna kupigika sana ili kuwe na mafanaikio,kwahiyo unachokiona Ethiopia ndio katika harakati za kuwa na uchumi imara.
 
Na uhuru pia unabanwa huko uingereza?
 
Waethiopia wanapenda sana maisha bora
hao wanaokwenda kwa malori wanalipa hadi dollar 3000 ili kusafirishwa

wakifika huko wanatafuta pesa zaidi kwa familia zao.....

sio malofa kihivyo unavyo dhani
 
Mali bila usawa katika kugawana rasilimali ni bure, ndio maana marekani kuna maendeleo ila maandamano ya watu weusi kutokana na kuuwawa kwai hayaishi, sawa na Ethiopia kuna jamii wanajiona miungu watu hakuna usawa katika mgawanyo wa rasilimali na madaraka kutoka makabila tofauti tofauti.
 
Back
Top Bottom