Kuna ndoa hapa kweli Ke(BACHELOR OF LAWS), Me(certificate)...

Phlagiey

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
3,485
2,000
Habari za hapa, natumaini kila mmoja amejaliwa afya njema,
kama ni kinyume na hivyo basi pole na mwombe mungu atakuponya.

Leo kuna jambo limenileta hapa lengo ikiwa ni kutafuta msaada wa mawazo yenu,
basi naomba nielekee moja kwa moja kwenye jambo husika;

Kuna binti nimekuwa nae katika mahusiano kama wapenzi wa muda wa miaka kadhaa mpaka leo,
tukiwa katika masomo ya sekondari kwa wakati huo tukisoma shule moja, alisoma hapo kwa muda badae akawa amehamia shule nyingine (inje ya wilaya) kwendelea na masomo yake.
Kwa kipindi hicho ndio nilikuwa naanza zile harakati za kufukuzia,baada ya kuondoka nilipata wakati mugumu sana,
kwa kuwa tayari alikuwa ameshaanza kuniingia kumtima kama mnavyojua mapenzi ya kisekondari zile pilika pilika za hapa na pale, kila wakati mnatama kuonana.

Badae nilizoea nikajipa moyo ipo siku atakuwa wangu, kweli baada ya kufunga shule (rikizo) akawa amerudi kama kawaida nikaendeleza kale kamchezo, ilifika wakati jibu lake likawa ndio hapo ni baada tayari nikiwa nimesha kula ruti za kutosha kumvizia kwao,na kwa nyakati hizo hatukuwa na uwezo wa kumiliki simu hivyo njia pekee ilikuwa ni kuvizia.

Basi masomo na mapenzi(mlenda na pirau) yakaendelea , ikafika mwaka wa kuhitimu masomo yangu,huku yeye akiwa amebakiza mwaka mmoja kuhitimisha masomo, mwaka ulio fuatia ukawa wa mavuno kwangu baada ya kulima na kupanda kwa miaka minne, kiukweli mavuno katika shamba langu hayakuwa mazuri, nikaamua kuingia mtaani sikutaka kurudi nyuma.

Ukafuatia mwaka wa huyo mpenzi wangu tuliekuwa kukishiriki nae mlenda na pilau, baada ya kuhitimu akawa amechaguliwa tena kwendelea kwa miaka mingine miwili ya kidato cha tano na sita, nyota yake ikaendelea kung'ara haikuishia hapo akachaguliwa tena kujiunga na masoma ya chuo kikuu kozi ya sheria, ikawa bahati kwangu kwa vile chuo kile kilikuwa katika mkoa nilio hamia nikitokea nyumbani kuanza maisha.

Hali ya mahusiano iliendelea kama kawaida japo kuna wakati tulikuwa tunakosana baadae tunarudiana tena huo ndo ukawa mchezo wetu kwa wakati huo akiwa kidato cha tano na sita, alipoanza chuo mahusiano yaka shamili kutokana na ukaribu uliokuwepo hapo u serious ukaanza kuonekana.

Harakati za maisha yangu zika endelea huku na huko nikaamua kujiunga na chuo fulani kupata ujuzi(cheti) ukanisaidia kujiendeleza kimaisha hapa mjini, nikafahamika na watu wengi sana tukokana na kazi yangu, kwa muda wa mwaka mmoja nikawa nimejipanga vya kutosha malengo niliokuwa nimeyapanga kwa wakati ule yakawa yametimia kiasi kikubwa na maisha yanaendelea mpaka leo.

Katika mahusiano yetu kuna mambo mengi tumejipangia likiwemo hili la uchumba mpaka kufikia katika ndoa na ndo mipango yetu kwa kila siku.

Maswali yanayo isumbua akili yangu kila siku ni je kwa utofauti huo kielimu kuna ndoa hapo?
Na je siku ya siku wazazi wake watamkubalia?
Na kama ndoa itafungwa itaheshimika?(kama mnavyo wajua baadhi ya watoto wa kike walio soma)
Yani maswali yako chungu nzima na huwa sipati majibu yake.

Ikumbukwe kwamba;
Yuko mwaka wa nne,
Chuo anachosoma kiko mkoa ninao ishi,
Tunaonana karibu kila weekend,
Tume tokea mkoa mmoja ila makabila tofauti,
Tumetekana kimawazo kutokana na hizo ahadi zetu,
Upande wa pili sijui anachoniwazia kutimiza malengo yetu binadamu hubadilika,
Siku wahi kufanya nae mapenzi mpaka alipo kuwa ameingia chuo.

Tafadhali, ninacho hitaji hapa mimi ni ushauri na kama unaswali unaweza kuuliza, matusi na kejeli naomba vinipite mbali.
Nakama unajijua hauna uweza wa kushauri chochote basi kuwa msomaji tu inatosha.

Natanguliza heshima zangu kwenu wote mtakao changia mawazo yenu hapa.......
 

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,067
2,000
"Legum Baccalaureus in Latin-LLB" sio elimu ya kutisha!Na kama Mke hakupendi sio kwa sababu yy ana LLB bali HAJAKUPENDA tu ulivyo!

Una rudi home usiku wa saa 9 usiku tena chakari umejikojolea then demu asikuache sababu utasema umeachwa kwa vile ana elimu zaidi yako?Thubutu!

Nasema tu uachwe tu yaa uachwe tu ahahahahaha
 

Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,540
1,225
^^
Endelea mbele zaidi, inawezekana ni kati ya wanawake toleo la kwanza wanaojitambua wanataka nini katika Maisha.
Upande wa pili, suala la usaliti, kuachana, pesa n.k yakitokea basi ndio ubinadamu wa mapenzi ulipotufikisha.
^^
 

Phlagiey

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
3,485
2,000
Acha kujishtukia na kujihukumu. Mapenzi hayana elimu, kuna mifano mingi ya mama kuwa naelimu kumzidi mumewe na wakadumu kwenye ndoa.

Sawa inawezekana tukawa tumependana lakini pia wazazi wananafasi katika hili je wakimkatalia.
 

CORAL

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
2,699
2,000
Maadam yeye yuko serious na wewe, songa mbele na mipango yenu kama yatatokea ya kutokea uwe tayari kukubali matokeo. Ujiandae kwa lolote kama zuri au baya.
 

Phlagiey

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
3,485
2,000
^^
Endelea mbele zaidi, inawezekana ni kati ya wanawake toleo la kwanza wanaojitambua wanataka nini katika Maisha.
Upande wa pili, suala la usaliti, kuachana, pesa n.k yakitokea basi ndio ubinadamu wa mapenzi ulipotufikisha.
^^
Sawa mkuu ila kuna wakati huwa na hisi labda kwa sababu nimemzidi umri na nina uwezo wakushawishi ndo hivyo nimemteka kimawazo hivyo siku akishituka sitakuwa nae tena.
 

Phlagiey

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
3,485
2,000
Acha ushamba!
Umesema uulizwe!
Hiyo hadithi yako ipo kitaarifa zaidi!
...
Ni lazima uweke wazi hofu yako iko wapi na kwa ground zipi!
Pambaf!
Mwanzoni nimekuona kama unakuja na mwelekeo mzuri lakini umejivua na kujiacha utupu kwa hizo kauli zako, ustaarabu sio mpaka uende darasani jamaa yangu, jipange kisha ni uliza swali lenye akili.
 

Mashaxizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
6,712
1,225
Mwanzoni nimekuona kama unakuja na mwelekeo mzuri lakini umejivua na kujiacha utupu kwa hizo kauli zako, ustaarabu sio mpaka uende darasani jamaa yangu, jipange kisha ni uliza swali lenye akili.

Ok!
Issue iko wapi ktk maelezo yako???
Or nini kijadiliwe?
 

Phlagiey

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
3,485
2,000
Maadam yeye yuko serious na wewe, songa mbele na mipango yenu kama yatatokea ya kutokea uwe tayari kukubali matokeo. Ujiandae kwa lolote kama zuri au baya.
kwa maneno yake yanaonesha hivyo lakini sasa hicho sio kipimo sahihi cha kujua ukweli wa moyo wake.
Kumbuka kama litatokea mbaya lolote litaniadhili kisaikorojia na kuinipeleke kufanya maamuzi yasio kuwa sahihi kwa kuwa ni muda tumekuwa pamoja na akili yangu imejenga matalajio makubwa ya kufikia malengo hayo.
 

Mu7

JF-Expert Member
Jun 15, 2013
721
1,000
Wanawake wengi huwadharau waume kama wanawazidi elimu au kipato. Huyu wako anakuzidi elimu, kama ww unamzidi kipato, atatulia. Kama anakuzidi vyote 2 kuna walakini, vinginevyo awe alilelewa na akaleleka. Ni nadra kuwapata wa hivyo leo. Ni mtazamo wangu.
 

Phlagiey

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
3,485
2,000
wanawake wengi huwadharau waume kama wanawazidi elimu au kipato. Huyu wako anakuzimi elimu, kama ww unamzidi kipato, atatulia. Kama anakuzidi vyote 2 kuna walakini, vinginevyo awe alilelewa na akaleleka. Ni nadra kuwapa wa hivyo leo. Ni mtazamo wangu.
Nimeipenda hii na imenipa changamoto nijipange zaidi kimaisha asante sana, much respect to u.
 

Jerrymsigwa

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
13,953
2,000
What is the issue bro? Unataka ufanyiwe nini na wana Jf, naona wengine wanajibu kwa mazoea.
 

Phlagiey

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
3,485
2,000
Ok!
Issue iko wapi ktk maelezo yako???
Or nini kijadiliwe?
Swala kubwa ni utofauti kielimu
Nakutakuawa na heshima ndani ya ndoa
Na nini kifanyike ili kuleta usawa japo kuna utofauti kielimu
Na haita niadhili kiasaikorojia kama malengo yasipo timia sababu sifikili mwinigine tofauti na yeye.
Yako mengi mkuu lakini sio mbaya ukianza na mchango wako katika hayo.
 

Phlagiey

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
3,485
2,000
What is the issue bro? Unataka ufanyiwe nini na wana Jf, naona wengine wanajibu kwa mazoea.

Swala kubwa ni utofauti kielimu
Nakutakuawa na heshima ndani ya ndoa
Na nini kifanyike ili kuleta usawa japo kuna utofauti kielimu
Na haita niadhili kiasaikorojia kama malengo yasipo timia sababu sifikili mwinigine tofauti na yeye.
Yako mengi mkuu lakini sio mbaya ukianza na mchango wako katika hayo.
 

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
10,739
2,000
Mkuu mimi nawaogopa sana hawa dada zetu coz always kinachowaendesha ni external forces zenye magnitude na directions tofautitofauti....Chombo(in this case mwanamke) hufuata direction ya force yenye magnitude kubwa...


Mimi ni hayo tu kwa leo!!!!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom