Kuna ndoa hapa kweli Ke(BACHELOR OF LAWS), Me(certificate)...

Ndoa si Elimu, jiamini tu. mbona tangu mwanzo hajakuacha kwasababu ya elimu yako ndogo? Usjidharau, km mnapendana oaneni tu achene uzinzi.
 
Habari za hapa, natumaini kila mmoja amejaliwa afya njema,
kama ni kinyume na hivyo basi pole na mwombe mungu atakuponya.

Leo kuna jambo limenileta hapa lengo ikiwa ni kutafuta msaada wa mawazo yenu,
basi naomba nielekee moja kwa moja kwenye jambo husika;

Kuna binti nimekuwa nae katika mahusiano kama wapenzi wa muda wa miaka kadhaa mpaka leo,
tukiwa katika masomo ya sekondari kwa wakati huo tukisoma shule moja, alisoma hapo kwa muda badae akawa amehamia shule nyingine (inje ya wilaya) kwendelea na masomo yake.
Kwa kipindi hicho ndio nilikuwa naanza zile harakati za kufukuzia,baada ya kuondoka nilipata wakati mugumu sana,
kwa kuwa tayari alikuwa ameshaanza kuniingia kumtima kama mnavyojua mapenzi ya kisekondari zile pilika pilika za hapa na pale, kila wakati mnatama kuonana.

Badae nilizoea nikajipa moyo ipo siku atakuwa wangu, kweli baada ya kufunga shule (rikizo) akawa amerudi kama kawaida nikaendeleza kale kamchezo, ilifika wakati jibu lake likawa ndio hapo ni baada tayari nikiwa nimesha kula ruti za kutosha kumvizia kwao,na kwa nyakati hizo hatukuwa na uwezo wa kumiliki simu hivyo njia pekee ilikuwa ni kuvizia.

Basi masomo na mapenzi(mlenda na pirau) yakaendelea , ikafika mwaka wa kuhitimu masomo yangu,huku yeye akiwa amebakiza mwaka mmoja kuhitimisha masomo, mwaka ulio fuatia ukawa wa mavuno kwangu baada ya kulima na kupanda kwa miaka minne, kiukweli mavuno katika shamba langu hayakuwa mazuri, nikaamua kuingia mtaani sikutaka kurudi nyuma.

Ukafuatia mwaka wa huyo mpenzi wangu tuliekuwa kukishiriki nae mlenda na pilau, baada ya kuhitimu akawa amechaguliwa tena kwendelea kwa miaka mingine miwili ya kidato cha tano na sita, nyota yake ikaendelea kung'ara haikuishia hapo akachaguliwa tena kujiunga na masoma ya chuo kikuu kozi ya sheria, ikawa bahati kwangu kwa vile chuo kile kilikuwa katika mkoa nilio hamia nikitokea nyumbani kuanza maisha.

Hali ya mahusiano iliendelea kama kawaida japo kuna wakati tulikuwa tunakosana baadae tunarudiana tena huo ndo ukawa mchezo wetu kwa wakati huo akiwa kidato cha tano na sita, alipoanza chuo mahusiano yaka shamili kutokana na ukaribu uliokuwepo hapo u serious ukaanza kuonekana.

Harakati za maisha yangu zika endelea huku na huko nikaamua kujiunga na chuo fulani kupata ujuzi(cheti) ukanisaidia kujiendeleza kimaisha hapa mjini, nikafahamika na watu wengi sana tukokana na kazi yangu, kwa muda wa mwaka mmoja nikawa nimejipanga vya kutosha malengo niliokuwa nimeyapanga kwa wakati ule yakawa yametimia kiasi kikubwa na maisha yanaendelea mpaka leo.

Katika mahusiano yetu kuna mambo mengi tumejipangia likiwemo hili la uchumba mpaka kufikia katika ndoa na ndo mipango yetu kwa kila siku.

Maswali yanayo isumbua akili yangu kila siku ni je kwa utofauti huo kielimu kuna ndoa hapo?
Na je siku ya siku wazazi wake watamkubalia?
Na kama ndoa itafungwa itaheshimika?(kama mnavyo wajua baadhi ya watoto wa kike walio soma)
Yani maswali yako chungu nzima na huwa sipati majibu yake.

Ikumbukwe kwamba;
Yuko mwaka wa nne,
Chuo anachosoma kiko mkoa ninao ishi,
Tunaonana karibu kila weekend,
Tume tokea mkoa mmoja ila makabila tofauti,
Tumetekana kimawazo kutokana na hizo ahadi zetu,
Upande wa pili sijui anachoniwazia kutimiza malengo yetu binadamu hubadilika,
Siku wahi kufanya nae mapenzi mpaka alipo kuwa ameingia chuo.

Tafadhali, ninacho hitaji hapa mimi ni ushauri na kama unaswali unaweza kuuliza, matusi na kejeli naomba vinipite mbali.
Nakama unajijua hauna uweza wa kushauri chochote basi kuwa msomaji tu inatosha.

Natanguliza heshima zangu kwenu wote mtakao changia mawazo yenu hapa.......

USHAURI: kuna utofauti katiyamaisha ya uchumba na ndoa! wakiingia makazini ndio usumbufu unaanza. nadhani usimuoe mapema, kuwa nae hadi miaka kama kumi..... umsome akipata kazi.ndoa ni KABURI WANAUME WENGI HUJIZKA WAKIWA HAI.. wanasema unaweza kukosea kujenga nyumba lakini sio kuoa mke
 
we oa achana na mawazo potofu..kama vp na ww piga shule kwani siku hizi mbona mtu unajiendeleza tu mpka unakuwa na phd ukitaka tatizo lik wapi

mimi nina rafiki yangu ni mwanasheria na mume wake ni dereva taxi na wanaishi vizuri sana, ila mume kajiendeleza hadi sasa yuko chuo
 
USHAURI: kuna utofauti katiyamaisha ya uchumba na ndoa! wakiingia makazini ndio usumbufu unaanza. nadhani usimuoe mapema, kuwa nae hadi miaka kama kumi..... umsome akipata kazi.ndoa ni KABURI WANAUME WENGI HUJIZKA WAKIWA HAI.. wanasema unaweza kukosea kujenga nyumba lakini sio kuoa mke

Hiyo miaka kumi tunakuwa katika uchumba bado au inakuwaje?
 
basi sawa!!

sasa kama huyo ni mwanasheria halafu anakubaliana na hoja zako,

basi ujue wewe una master degree tayari, basi tu hujijui!

Hahahahaha hiyo itakuwa ya mtaa sio darasani mkuu....!
 
ni misingi ipi iliyowafanya mkawa pamoja kwa muda wote huo? itambue, kisha muidumishe! ndoa/uhusiano haujengwi na material things, bali upendo wa kweli baina yenu. kwa story jinsi ilivyo, mdada anakupenda kwa dhati, kwani ingekuwa kinyume, huko chuoni ameshakutana na wasomi wenzake angesha kutosa siku mingi kama angelikuwa wa hivyo, lakini bado uko nae, hiyo ni ishara nzuri. kuhusu wazazi, hata kama kutakuwa na kauzibe, itategemea support na msimamo wa huyo kimwana. ni imani yangu hatobadilika! epuka hisia hasi juu yako (inferiority complex) iwe katika elimu, fedha, mali nk. penda sana kujiendeleza ili kupata maarifa na stadi za kuboresha shughuli uifanyayo, mpendane unconditionally, mheshimiane na kujaliana pia! Mungu awasaidie..,,
 
Rudia kusoma utaelewa.. ISSUE ni ipi hapo.
we wa kiume kweli?
unaombaje ushauri wa kukaa na m2 unayemfaham wewe,wakati si hatumfaham?
unadhani mbinu anazotumia m2 kukaa na mkewe zitakufaa wewe?
Sasa usijidanganye, Wewe ushajitoa kifikra kukaa na uyo mdada,usipokuwa makini utajitoa kimwili kabisa,...!
Jitambue na tambua ndoa si maigizo ya kutafuta maoni ili uweze kuishi,bali ni maridhiano ya pande mbili kuweza kuheshimiana nyakati zote bila kujali uwezo wa mwingine...
ndugu yangu ongea na mchumba wako mkiridhiana funga ndoa,usitafute mawazo ya kukaa na mwanamke,Mjue na kama unaona anakufaa kwa tabia zake fanya mambo.....
ukichukua ushauri huku na kuufanyia kazi,siku mkitofautiana utakuja kutuomba msaada wa kutatua????????????
Funguka fanya maamuzi kuoa si kujenga nyumba,ukikosea kuoa ni janga la maisha,ila ukikosea kujenga nyumba utafanya ata ukarabati kama sikubomoa
 
ni misingi ipi iliyowafanya mkawa pamoja kwa muda wote huo? itambue, kisha muidumishe! ndoa/uhusiano haujengwi na material things, bali upendo wa kweli baina yenu. kwa story jinsi ilivyo, mdada anakupenda kwa dhati, kwani ingekuwa kinyume, huko chuoni ameshakutana na wasomi wenzake angesha kutosa siku mingi kama angelikuwa wa hivyo, lakini bado uko nae, hiyo ni ishara nzuri. kuhusu wazazi, hata kama kutakuwa na kauzibe, itategemea support na msimamo wa huyo kimwana. ni imani yangu hatobadilika! epuka hisia hasi juu yako (inferiority complex) iwe katika elimu, fedha, mali nk. penda sana kujiendeleza ili kupata maarifa na stadi za kuboresha shughuli uifanyayo, mpendane unconditionally, mheshimiane na kujaliana pia! Mungu awasaidie..,,

Umesomeka vizuri sana, Dr asante kwa mchango wako.
 
muoe tu mie kuna jamaa yangu ni mlinzi lakini ameoa mwanamke mwanasheria na wanaishi vizuri cha muhimu huyo mchumba wake awe na heshima kwako
 
Kwa kiasi fulani ni changamoto tu kwa sababu moyo wa binadamu ni giza nene,swala la elimu sio tatizo sana kama kuna mapenzi ya dhati,lakini lazima ujiandae kuwa mpole pindi mtakapokuwa mumepishana ndani ya ndoa ili kuepuka kashfa na maneno makali,kuhusiana na elimu yako,otherwise hakikisha unamzidi kipato,hapo utakuwa umemuweza kabisaaaaaa!!
 
Back
Top Bottom