Kuna nchi yoyote ya Ulaya iliwahi kopa Africa?

Safety last

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
4,227
1,389
Wanabidii Africa na rasimali zake kuna nchi yoyote ya ulaya iliwahi kukopa nchi za Africa rasimali au fedha kujikwamua kiuchumi 'tufahamishane?
 
Wanabidii Africa na rasimali zake kuna nchi yoyote ya ulaya iliwahi kukopa nchi za Africa rasimali au fedha kujikwamua kiuchumi 'tufahamishane?

Nchi za ulaya hazikopi zinaiba kiujanja. Kivipi?

kwanza walizitawala nchi za Afrika na Asia...hapo walikuwa wanakomba tu.

Haya ukaja unaoitwa uhuru...masoko ya kahawa na chai,kakao, dhahabu nk ofisi kuu zote ziko ulaya na ndio huko wanakopanga bei.

Mfumo wa kifedha, mabenki (fractional banking)pamoja na riba ni system zao kwa hiyo kila kitu kinawafuata wao,au kinawaendea wao. Wanakuka mkopo halafu utawatumikia kulipa riba tu mpaka utazeeka.

Lakini fikiria kama kadhia ya Libya au Ivory Coast...fedha za serikali za nchi hizo zimekuwa frozen na kwa hiyo, Libya yenye fedha zake katika nchi hizo hawawezi kuzitumia, huwa ndio kama zimepigwa tanji.

Hizi ni njia chache tu wanazotumia nchi za ulaya kuziibia nchi za Afrika. Bila shaka wataalamu wa mambo ya fedha na mikopo watajitokeza watatusaidia zaidi.

Umenichekesha kidogo.umenifanya nikumbuke benki ya posta walivyoniibia. Niliweka fedha na kujifanya nimezisahau kwa miaka hivi..siku nakwenda kuchungulia ziko ngapi,niliambiwa mimi ndio ninadaiwa kwani walianza kutoza ada kwa mwenye akaunti....sasa hapo utacheka au utalia?

Yaani hela yangu wameshaitafuna na bado wananiambia wananidai.
Of course, nilicheka kwa uchungu na nikamuuliza nadaiwa shilingi ngapi, akanitajia maelfu kadhaa.
Nikamwambia ok, ngoja nikakope ili nije nilipe deni lenu!!! Nikajiondokea na sikurudi tena.
Sasa siweki tena fedha benki.
 
watakopaje wakati wanauwezo wa kuiba na kukaba au umesahau kwamba wazungu na watu wa ulaya ndio majambazi wakuu wa afrika, kukopa ana kusaidia sio fedha tu, fedha ni makaratasi lakini wanakwiba rasilimali nyingi zaidi afrika
 
mbona zinakopa kila kukicha?
hata hivyo zenyewe zinakopa bila kufuata
taratibu ambazo zenyewe hutaka wengine kufuata pindi
wanapohitaji mkopo
 
Wanabidii Africa na rasimali zake kuna nchi yoyote ya ulaya iliwahi kukopa nchi za Africa rasimali au fedha kujikwamua kiuchumi 'tufahamishane?

wanakopa kwani wanavyotuibia ni sawa na gharama wanazotulipa? sie hatuhesabii kuwa wanatukopesha bali wanabudi kutusaidia kwani mali zetu wanatuzulumu
 
Toka enzi za karl peterz wazungu wanatuibia tu, hawana aibu ya kuja kuomba kistaarabu, wenyewe wanaiba tu.
 
Back
Top Bottom