Kuna mtu alishawahi kumiliki Mini Cooper?

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
53,102
53,357
Leo nimeamka na hili gari kichwani.

Nafuatilia reviews youtube hasa Mini Cooper Countryman.

Kama kuna mtu alishawahi miliki au kuendesha hili gari njoo tuchat.

1596341172676.png
 
@Kadukulilo kwa heshima ya kiongozi hapa alishawahi kujadili pitia haya na umuone kwa ushauri Wa kitaalamu

BMW MIN COOPER

moja kati ya gari ndogo lakini shughuli yake sio ya kitoto barabarani ni BMW min cooper , gari hii iliweza kupewa majina mengi kutokana na umbo na uwezo wake min hatch wanaiita hivyo huko U. S. A, gari hii inakuja na milango mitatu au mitano , ni gari ambayo ukiendesha kwa raha yake hutatamani kuacha kwenda ujerumani...ni gari ndogo lakini yenye parformance ya tofauti sana ,lakini pia ni gari imara sana
Upande wa ndani gari hii inakuja na

Umbo :Hatback
Extras: Panoramic Sunroof
Safety Features: ABS, brake assist, Electronic Brake Force Distribution (EBD), SRS Airbags, three point seat belts with ELR, Vehicle Dynamic
Control(VDC)
Exterior Features: Alloy Rims, Fog Lights, Roof Rails
Interior Features: Bluetooth
Connectivity, CD/DVD Player, Dual Zone

Upànde wa generetion gari hii kizazi cha kwanza kilianza mwaka 2000 kizazi cha pili kilianza mwaka 2006
Kizazi cha tatu kilianza mwaka 2014

Upande wa bodi stayle
3-door hatchback
5-door hatchback
2-door convertible

Upande wa kufanana gari hii inafanana sana na Mini Coupé,Mini Clubman,Mini Countryman,Mini Pacema..

Upande wa usanifu
Gari hii imesanifiwa vizuri ina umbo dogo lakini inawezesha kukata haswaa na kufanya ...kuwa na speed nzuri na ya kutosha ....upande wa bodi bodi lake ni gumu haswa sio mayai .....

Upande wa ndani
Gari hii inakuja na mistari iliyopangiliwa vizuri... Mstari wa kwanza unakuja na viti viwili na mstari wa pili unakuja na viti vitatu kwa ile yenye milango mitatu ...nafasi ya ndani imebanwa kidogo kwa mtu mrefu inaweza kuwa shida kuingia na kutoka hata kwa mtu mnene wakenya wanasema aliyenona .....

Upande wa injini......

1.4 L Prince I4 (One)

1.6 L Prince/BMW I4 (Cooper)

1.6 L Prince turbo I4 (Cooper S)

1.6 L Peugeot DV6 diesel I4 (One D and Cooper D (manual transmission)

1.6 L BMW N47 diesel I4 (Cooper D

2.0 L BMW N47 diesel I4

Hizi ndizo injini zinakuja na gari hii kunaninjini tofauti tofauti kunaninjini zilikuwa maalumu kwa soko la ulaya ,ndio maana ikiimport min cooper ya soko la ulaya na ya masoko mengine ziko tofauti sana ila injininzote zinafanya vizuri barabarani
Injini hii 1.6 L Peugeot DV6 diesel I4 iliundwa na kampuninyabpeugeotbkwa makubaliana maalumu na BMW inaonekana kuwa haina usumbufu sana ni dizel kibaya tu gari lenye injini hii linawa ni manual tu ..

Upande wa transmition
Gari hii inakuja na 6 speed manual au automatic ni gari nzuri sana ....ila kwa bongo hapa mambo tofauti watu wajuaji sana .....gari hii kwa upande wangu ,Manual inatembea sana yaani iko more power fully ...kuliko automatic transmition ...shida yake manual...nyingi ninazo ziona zimekufa gear box yake ....lakin haya yote yanasababishwa na matumizi ya ukanyagajinusio mzuri wa clutch pedol wakati mwingine ....kutembelea gia isiyo sahihi....gari za kule majuu kama BMW, ukitaka kuiabuse ijali sana SERVICE ZAKE ,usiruke wala usitafute mbadala wa oil utaumia siku sio nyingi na itakutoka hela ....mpk wallet isinyae

Technical specifications
Cooper na cooper S imeundwa na
rear axle na aluminium components ili kuifanya gari kupunguza uzito usiokuwa na maana na hivyo kuipunguzia injini mzigo na upande wa sport Sports kit imeundwa na comprising harder springs, damper na anti-roll bars, hivyo kunaiwezesha gari hii kupita hata katika sehemu ngumu ambazo gari ndogo nyingine haziwezi kwenye kona unaweza kunyooka nayo kwa speed kubwa bila ya kuwa na tatizo lolote.

kama haujawahi kuona shughuli ya gari hii tafuta movie moja inaitwa THE ITALIAN JOB "Utaona visanga vya gari hiii uwezo wake ...wa kuhimili mikiki kwa upande wa steering ipo upgraded electric power steering system, ambayo inasaidia kuongeza maujuzi kukata kona kukwepa.

Yaani laini sana ...acha kabisa ni wewe tu na control zako kwa lile toleo la michezo sport ,inakuja na batton moja ambayo inasaidia gari kuiongezea ufanisi wakati wa kubadilisha gear acceleretion yake isiathirike , upande wa injini valve zake ni valve tronic

Tuone upande wa acceleretion katika gari hili ipo vipi

1.4 L Prince I4 (One) inatoka 0-100km/h kwa sec 13.5

1.6 L Prince/BMW I4 (Cooper) inatoka 0-100km/h kwa 11

1.6 L Prince turbo I4 (Cooper S) inatoka 0-100km/h kwa 9

1.6 L Peugeot DV6 diesel I4 (One D and Cooper D (manual transmission)
Inatoka 0-100 km /h kwa sec 9.1

1.6 L BMW N47 diesel I4 (Cooper D inatoka 0-100km/h kwa sec 9

2.0 L BMW N47 diesel I4 inatoka 0-100km /h kwa 5.sec

Kuna haja kweli ya kuelezea matumizi ya mafuta katika gari hii au

1.4 L Prince I4 (One)

1.6 L Prince/BMW I4 (Cooper)

1.6 L Prince turbo I4 (Cooper S) inatumia km 20 kwa lita 1

1.6 L Peugeot DV6 diesel I4 (One D inatumia km 19.6 kwa lita 1

1.6 L BMW N47 diesel I4 (Cooper D
Inatumia km 18.4 kwa lita 1

2.0 L BMW N47 diesel I4 inatumia km 16 kwa lita 1

Uchague ipi mm napenda gari za European iwe ya dizel maana za petrol zinahitaji umakini hata utengenezaji wake ,unahitaji sana wasio mafundi nyundo ila injini ya petrol ni rahic kuifanyia injini tuning na ukaiongezea parfomance , hospower ...ikawa haikamatic kirahic hiki kitu bongo naona gereji chache ndio wanafany injini tuning ......

Changamoto katika gari hii
Clutch failure
water pump leaking
Movement katika Timing Chain inapelekea kelele ( Create Noise ) na Vibration
Electric Power Steering Pump kwa nyingi inazingua sana
Variable Valve Timing (VVT) Issues
Katika ufanyaji kazibwa timing systeam inahitaji oil ilikuweza kufanya kazi vizuri oil inapopungua hata kidogo hupelekea msuguana na kuvuja

Transmission Problems and Failure
Hili sehemu kubwa linasabbishwa na uendeshaji mbaya nankutosoma manual book ya gari

Matatizo machache nikiyoyaainisha ya min cooper BMW ukiwa mtunzaji mzuri unaweza usione tatizo lolote maana hii ni European car matunzo ndio muhimu zaidi

Mwisho
Min cooper ni gari ambayo sidhani kama itakuja kuchuja ...umbo ni dogo lakini bado kwenye parformance inafanya vizuri na ipo poa sana gari hii inamfaa mtu yoyote ...wanawake wau wanaume ...gharama yake ni ndogo ...na upande wa safari inamudu vizuri kuliko kawaida .

Jitahidi unaponunua au kuagiza lisiwe limetembea zaid ya km 150,000
 
Hapa ungeuliza kuhusu Toyota hii jamiiforum yote ingehamia Kwenye Uzi wako. Wabongo tumelogwa na Toyota ingawa sikuhizi nafurah Sana kuona barabaran kuna Magari mengi ya ulaya, Ile kasumba ya kishamba inaanza kupotea.

Hizi min copper zinahitaji uangalifu wa Hali ya juu ingawa Kwa wanaomiliki wenyewe wanakuambia hawana mpango wa kurudi Kwenye Toyota ni kama vile wanaomiliki subaru wengi wao hawataki tena kurudi Kwenye Toyota
 
@Kadukulilo kwa heshima ya kiongozi hapa alishawahi kujadili pitia haya na umuone kwa ushauri Wa kitaalamu

BMW MIN COOPER

moja kati ya gari ndogo lakini shughuli yake sio ya kitoto barabarani ni BMW min cooper , gari hii iliweza kupewa majina mengi kutokana na umbo na uwezo wake min hatch wanaiita hivyo huko U. S. A, gari hii inakuja na milango mitatu au mitano , ni gari ambayo ukiendesha kwa raha yake hutatamani kuacha kwenda ujerumani...ni gari ndogo lakini yenye parformance ya tofauti sana ,lakini pia ni gari imara sana...
Full! , Great!
 
Kaka yangu (rafiki alienizidi umri) kanunua ya 2013 I think, kagari kazuri sana. Country man na Clubman nzuri sana.
Hebu muulize, huwa inamsumbua nini hasa??

Spares huwa anazipata hapa bongo au anaagiza?

Nataka kufahamu zaidi mkuu.
 
Back
Top Bottom