Kuna mkono wa CCM kwenye kesi ya Slaa? Angalia picha hii!

attachment.php

Picha ya wabunge wa CCM (Sophia Simba na Esther Bulaya) wakimkumbatia Rose Kamili (Chadema) jana mjini Dodoma, ambapo Kamili amefungua kesi ya kupinga ndoa ya Dr Slaa na Josephine Mshumbuzi hiyo jana.

Mizimwi inayojuana hii we achana nayo
 
Usiumize kichwa mkuu waache waendele kuruka sarakasi na taulo sebuleni........Wakili anayemtete Rose Kamili Ni Tadayo CCM pure na ndiye mwanasheria wa Membe, anaye mtetea Mahimbo ni Mgombea wa Udiwani Ubungo kwa Tiketi ya CCM akadondokea pua.Ukipitia Madai ya Rose kamili hata kwa mtu ambaye siyo mwanasheria ukiyaangalia unaweza kugundua mengi. :wacko:

Huyu wakili Tadayo pia ni wakili wa fisadi Yusuf Manji , yaani zao la ufisadi, ni kijana wa kipare na jaji Kaduri pia ni mpare na CCM damu.
 
Uzinzi uzinzi uzinzi! laana juu ya laana juu ya laana. Kwa Kanoni, kwa Sharia, Kwa Sheria kote kote ayafanyayo Slaa ni uzinzi tu.

Huyo ndio kuna wachache wanaoona hilo si kosa wanataka awe Rais wa nchi hii? Dah!
Kuna rais aliyewahi kuchukua Utawala akioonyesha alikuwa bikra kabla ya ndoa yake?. Ama unataka tuseme vitu visiyvofaa hapa janvini maana sii mahala pale. Wee mwenyewe sii ama hukuwa bikra ulipofunga ndoa tuache siasa za kipuuzi..
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Nani anaeongolea ubikira hapa? Mbona hili la uzinzi mnalitetea sana, kiongozi mzinzi hafai hata kidogo.

Halafu kama hujui kuwa upadri una kigezo cha kutokufanya ngono, au ndio hicho kilichomfanya aondoke kwenye uongozi wa kanisa?
 
Hakuna katika makosa makubwa kama kuiba mke/mume wa mtu. Hii ni aibu ya karne kwa mtu eti aliyetaka aingine magogoni!

aaah mzee mwenzangu acha kudhalilisha wakina mama/baba. Utaiba mtu amekuwa commodity? Wao waseme wamezidiwa maujanja sasa wanataka malipo! By the way, huyo bwana Mahimbo alipata talaka yake, sasa anataka nini tena? No one owns anyone, talaka zipo kila mahali, Tom Cruise ndio anamalizana na Katie Holmes.

Tuachane na mambo ya watu, vipi ADC mmemaliza kuhakiki wanachama?
 
1.Aligombea jimbo la hanang akapata idadi kubwa ya kura ,tena baada ya nyie magamba kuzichakachua.
2.aliwezesha kupatikana madiwani 12 kati ya 26(ccm 13 na cuf 1) ,sehemu iliyokuwa na diwani 1 tu wa upinzani(cdm)
3.alifanya kampeni kubwa Dr.Slaa akaongoza kura za urais jimbo la hanang ,hata baada ya uchakachuzi wenu mlishindwa kumaliza kuziiba ,hasahasa baada ya Mary nagu kuchanganyikiwa kupoteza jimbo akajikuta anaconcentrate zaidi kuchakachua zake za ubunge.

baada ya kuwa mbunge....
1.muulize January Makamba kwenye Ripoti yake kutathmini hali ya kisiasa nchini na CCm kwenye Kamati kuu aliwaambia nini kuhusu Rose Kamili baada ya kuwavua Magamba viongozi wa ccm manyara,diwani wa ccm endasaki na kuvunja serikali za vijiji zaidi ya 13 kwa kuwavua magamba wenyeviti wa hivyo vijiji.
2.kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani Endasaki alisimamia kampeni akachuku kata hiyo ,sasa hivi hanang anamadiwani 12.
3.muulize mwigulu nchemba kwenye kampeni Arumeru na Igunga Rose kamili aliwafanya nini kwenye kampeni za mtaa kwa mtaa ,nyumba kwa nyumba...ndiyo utaipata majibu yake.[/QUOTE
LIKE! Huyo mama ametoa mchango mkubwa kuijenga CDM mkoani Manyara hasa wilaya ya Hanang. Nadhani haya mambo tuwaachie wahusika wayamalize kwa njia za kistaarabu.
 
Nani anaeongolea ubikira hapa? Mbona hili la uzinzi mnalitetea sana, kiongozi mzinzi hafai hata kidogo.

Halafu kama hujui kuwa upadri una kigezo cha kutokufanya ngono, au ndio hicho kilichomfanya aondoke kwenye uongozi wa kanisa?
Mzinzi ni mtu anayetembea nje ya Ndoa - Iwe umeshaoa ama hujaoa. Au wewe mwenzetu una kiswahili tofauti na hicho...
 
Naona wivu unakusumbua! Ulipigwa chini na Dr?
 
Huyu wakili Tadayo pia ni wakili wa fisadi Yusuf Manji , yaani zao la ufisadi, ni kijana wa kipare na jaji Kaduri pia ni mpare na CCM damu.
Ndiye pia wakili wa kina mramba,Mgonja na yona kwenye ile kesi ya matumizi mabaya ya ofisi.Kiufupi huyu Jamaa ni CCM pure na alikuwa mgombea wa ubunge jimbo la Magembe anaalikuwa anaungwa mkono na Msuya. Ila mambo hayakwenda vizuri alipata ajali na katika ajali ile akampoteza mwanae mpendwa.
 
1.Aligombea jimbo la hanang akapata idadi kubwa ya kura ,tena baada ya nyie magamba kuzichakachua.
2.aliwezesha kupatikana madiwani 12 kati ya 26(ccm 13 na cuf 1) ,sehemu iliyokuwa na diwani 1 tu wa upinzani(cdm)
3.alifanya kampeni kubwa Dr.Slaa akaongoza kura za urais jimbo la hanang ,hata baada ya uchakachuzi wenu mlishindwa kumaliza kuziiba ,hasahasa baada ya Mary nagu kuchanganyikiwa kupoteza jimbo akajikuta anaconcentrate zaidi kuchakachua zake za ubunge.

baada ya kuwa mbunge....
1.muulize January Makamba kwenye Ripoti yake kutathmini hali ya kisiasa nchini na CCm kwenye Kamati kuu aliwaambia nini kuhusu Rose Kamili baada ya kuwavua Magamba viongozi wa ccm manyara,diwani wa ccm endasaki na kuvunja serikali za vijiji zaidi ya 13 kwa kuwavua magamba wenyeviti wa hivyo vijiji.
2.kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani Endasaki alisimamia kampeni akachuku kata hiyo ,sasa hivi hanang anamadiwani 12.
3.muulize mwigulu nchemba kwenye kampeni Arumeru na Igunga Rose kamili aliwafanya nini kwenye kampeni za mtaa kwa mtaa ,nyumba kwa nyumba...ndiyo utaipata majibu yake.

Kwa mtaji huu ana haki ya kudai fidia ya mil 500, mambo yote haya yalomwezesha Slaa kupata umaarufu huko halafu leo aibiwe hivi hivi ! jamani let us be fair hapa ! mpeni mama haki yake ... Josephine mrudishie mwenzio mumewe jamani!
 
Rose Kamili mbona hakumpinga Dr. Slaa kipindi cha uchaguzi au alikuwa anasubiri apate ubunge wa viti maalum ili aanzihe malumbano baadae! Mbinu zote za kudhoofisha chama na kuchafu viongozi hazitafanikiwa kwa jina la maslahi ya umma!
 
Hakumpinga labda kwasababu kuu 3....
1.kupisha uchaguzi upite kwa maslahi ya chama.
2.kutoa nafasi kulimaliza hili suala nje ya mahakama.
3.Slaa hakuwa ametangaza kufunga ndoa na Josephine kissheria(ikumbukwe jumapili iliyopita ndiyo ilikuwa tangazo la 3 na la mwisho kanisani kwa mtu kuweka pingamizi)
 
Mzinzi ni mtu anayetembea nje ya Ndoa - Iwe umeshaoa ama hujaoa. Au wewe mwenzetu una kiswahili tofauti na hicho...

Kwa kuongezea hapo pia ni yule anayefanya ngono na wapenzi zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja au kwa lugha nyingine anayetembea nje ya mapenzi!!

'ndoa' ni siasa za vyumba vya kulala na ni mapatano kati ya watu wawili (au kwa utamaduni mwingine kati ya mume mmoja na wake zake au mke mmoja na waume zake) kuishi pamoja na kupeana huduma za kudumu za kingono. Hata hivyo wakati mwingine huo uhusiano ufika mahala ukachuja. Ikifikia hali hiyo wahusika huachana kwa njia mbalimbali vinginevyo watatoana roho. Baada ya ndoa kufikia mwisho haina maana kuwa wahusika wamezibiwa raghba zao za kuingia katika mahusioano na watu wengine. Wahenga zetu walilijua hili na kuliwekea utaratibu mzuri wa wanaume kuoa wake zaidi ya mmoja kama Waislamu walivyolizingatia katika imani ya dini kwamba mume anaweza kuwa na wake wanne kwa wakati mmoja. Wenzetu Wazungu waliotuletea utamaduni wao wa mke mmoja mume mmoja na haya ya kufunganishan ndo katika makanisa ndo yametongeza mgogoro wa binadamu kufikiri kuwa ndoa ikiishafungwa basi 'ni wewe na mimi' hata kama mapenzi yamekufa!!! Mh Kamili amwache Mh Slaa achukue kinachokoga moyo wake, Mh Mshumbusi.
 
kuna mtu jana alileta mada ya kashfa zinazomwandama Dk Slaa ila ile mada haikupokelewa vizuri, sio mbaya ni mtazamo wa wengi na ule ulikua ni mtazamo wake, sasa leo hii tunaambiwa kuna kesi ya kupinga ndoa ya Dk Mahakamani, hapa si kuna mchezo unaochezeka kweli??
hawa magamba walishaona kwamba hawawezi kuidondosha CDM majukwaani sasa wanatumia mlango wa pili, ambao ni mambo ya kubandikiana KASHFA, ni dhahiri shahiri yatupasa tukae sawasawa na imara kama tunakitakia mema chama chetu..M4C

hawa wana wake bana, ni watu dhaifu sana,japo sio wote ila wengi wao.. na hata Adam alilegezewa sauti tu na Hawa na mwisho wa siku kilichoendelea mnakijua, labda mwenye nakala ya madai ya huyu Rosi Kamili atubandikie hapa nasisi tujaribu kuwa wanasheria wetu wenyewe
 
quote_icon.png
By zomba

Uzinzi uzinzi uzinzi! laana juu ya laana juu ya laana. Kwa Kanoni, kwa sharia, Kwa Sheria kote kote ayafanyayo Slaa ni uzinzi tu.

Huyo ndio kuna wachache wanaoona hilo si kosa wanataka awe Rais wa nchi hii? Dah!

Mkuu, hilo ni kosa kwa wenzetu lakini kwetu sisi si kosa kijamii. Huwezi kulilinganisha na kosa la kuwalea mafisadi ambalo linafanywa waziwazi na viongozi wetu. Mzinzi katika jamii yetu anakubalika lakini fisadi hakubaliki. Usishangae kuona kwamba watu wakamchagua mzinzi kuwa kiongozi wao na kumkataa fisadi hata kama awe toashi namna gani! Huwezi kuwatakasa mafisadi kwa kuonyesha kwamba kiongozi wanayempenda ni mzinzi kwani watu hawajui kwamba hao wanaofanywa si wazinzi ni mafuska wasio na mfano? Utamdanganya nani siku hizi?

Hata hivyo, mimi wasiwasi wangu kuhusu hii ishu naona imekaa vibaya. Isije ikawa TISS wana mpango wa "ku-limboka" huyo Rose Kamili ili kuwakamata Dr Slaa na Madame Mushumbusi kwa kigezo kwamba "ni mgomvi" wao? Hiyo wenyewe wanaita kutengeneza "precedence" au kisababishi. Hao TISS ni watu janja sana. Wakati mwingine wanaanza mbali sana. Isije ikawa Rose kanaswa kwenye mtego wa panya usiomhusu? Kabanikwa kama chambo na hajijui? Kwani yeye uhusiano wake na Dr Slaa ni mbaya sana kiasi cha kuzuia ndoa ya mke mwenza? Si afadhali aache kuliko kujiweka chambo kwenye ugomvi ambao haupo? Ona sasa kapongezwa na wabunge wa CCM kwa kufanya lipi jema? Na wenzake wa CDM?
 
ni wanawake lazima wateteane kupinga ufisadi wa mapenzi

Wewe umetumwa? Una tofauti gani na wao? Hiivi hujui kuwa MTU ANAOPOAMUA KUKUACHA NI KUWA HAKUTAKI NA HATAKI KUWA NA WEWE TENA no matter how hard ujaribu kurudisha mahusiano. Hakuna fisadi wa mapenzi wala nn wewe unashadadia utadhani ulikuwa mshenga. Acha kiherehere au unawashwawashwa
 
Rozi kama Shibuda, pandikizi la pili ndani ya cdm limejidhihirisha, hakuna atakayebaki cdm akiwa ndumi la kuwili
 
Back
Top Bottom