- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
- Tunachokijua
- Mtumiaji wa mtandao wa Facebook kwa jina la 'Tanganyika huru' leo Januari 13 amechapisha taarifa inayodaiwa kutolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na kudai kuwa ofisi hiyo inawatangazia mikopo isio ni riba ijulikanayo kama 'NIWEZESHA NA SAMIA 2025' itakayo wanufaisha vijana zaidi ya elfu ishirini na tano ambao ni wajasiria mali wenye umria wa kuanzia miaka (18-45) na kwamba mikopo hii itatolewa chini ya usimamizi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI.
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Kupitia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) imebainika kuwa haikutolewa wala kuchapishwa na Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI), bali imetengenezwa na wapotoshaji wenye nia ovu.
Aidha taarifa hiyo hiyo imekuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo ya kiundishi, matumizi ya njia za mawasiliano binafsi ikiwemo namba ya simu na barua pepe, jambo linaloitofautisha taarifa hiyo na taarfa halisi zilizowahi kutolewa na TAMISEMI.
