kuna meli imezama leo ziwa victoria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kuna meli imezama leo ziwa victoria

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by dubu, Feb 23, 2012.

 1. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,071
  Likes Received: 421
  Trophy Points: 180
  sijapata habari kamili. nasikia kuna meli imezama mida ya saa tatu leo ziwa victoria. mwenye habari p'se atusaidie hasa watu wa mwanza.
   
 2. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  ngoja nifanye mawasiliano na washikaji zangu wa mwanza kisha ntarudi.
   
 3. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Is it true?OMG
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  duu kama ni kweli rip wote mtakao kufa maji..
   
 5. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  please get back with details
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Naomba habari hii isiwe ya kweli
   
 7. Eraldius

  Eraldius JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 569
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Mkuu tufahamishe vizuri hiyo OMG
   
 8. K

  Kiumbe duni Senior Member

  #8
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ooh My God.
   
 9. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  wamekufa tena??????????????????????????????????
  Mungu wangu we
   
 10. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inapendeza unapoingia jukwaani na habari kamili zenye uhakika!
   
 11. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Ni kweli meli imezama ziwa victoria!
   
 12. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  amefariki 1 wameokolewa 15!!!!!
   
 13. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Ni kweli mkuu,
  Meli imezama na amefariki 1 na 15 wameokolewa
  Nafatilia kujua ni meli gani(jina la meli)
   
 14. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Poleni wafiwa,Tanzania yaweza kuwa eneo hatari kwa maisha ya binadamu,kila siku kuna vifo vinavyoweza kuepikika.
   
 15. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Itakua siyo meli labda mtumbwi au ngalawa.
   
 16. HP1

  HP1 JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 3,353
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  WATU 16 wamenusurika kufa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria ya mv Nasebwa katika Ziwa Victoria kuzama. Watu hao walifanikiwa kuokoa maisha yao baada ya kuvaa maboya.

  Taarifa zinasema kwamba boti hiyo iliyokuwa ikitokea Maisome kwenda Kaunda ilizama baada ya kugonga mwamba na kuanza kuingiza maji, lakini kutokana na boti kuwa na vifaa vya uokoaji, watu wote walivaa maboya yaliyowasaidia kuelea majini hadi walipookolewa.

  Meneja Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), David Mziray alisema boti hiyo inayomilikiwa na Msita Francisco wa Kisiwa cha Maisome Sengerema ilipata ajali hiyo Jumapili iliyopita majira ya saa nane mchana.

  Mziray alisema, “tukio kama hilo la okoaji linaonyesha umuhimu wa vyombo vya usafiri wa majini kuwa na vifaa vya kutosha vya kujiokolea kama maboya ambavyo mara kunapotokea ajali, abiria au wafanyakazi wa chombo husika wanaweza kuokolewa na kuwa salama.”

  Alisema Sumatra inaendelea kusisitiza kuwa wamiliki na waendesha vyombo vya majini ili kuepuka ajali kuzingatia kuwa chombo chochote hakiruhusiwi kuanza safari kama hakijakaguliwa na kupewa cheti au hakijasajiliwa au kimepakiwa kuzidi uwezo wake.

  Pia chombo kisicho na mitambo (injini) hakiruhusiwi kubeba abiria huku chombo chochote hakiruhusiwi kuanza safari kama hakina vifaa vya kuokolea maisha, hasa majaketi kwa ajili ya wasafiri wake.

  Mziray alisema chombo kabla ya kuanza safari ni lazima kupata taarifa ya hali ya hewa na kutoanza safari pale inapobainika kuwa hali ya hewa ni mbaya katika sehemu yoyote ile ya njia inayotarajiwa kutumiwa na chombo na mengineyo.


  Source: Habari Leo
   
Loading...