Kuna mbunge wa kuaminiwa tena? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna mbunge wa kuaminiwa tena?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Speaker, Jul 24, 2011.

 1. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ni maswali ambayo sio rahisi kwangu kupata majibu,…

  Kwamba aliye kuwa katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini alikua ana
  Tafuta hela ili awape “hongo ” wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania
  Ili wapitishe bajeti bila matatizo.

  Katika barua ile imenukulia akitumia maelezo "unaombwa kuchangia jumla ya shilingi 50,000,000/="..

  Hiki sio kiasi kidogo cha hela,je huyo anae changia anatoa sadaka au atarudisiwa?

  Na kama atarudishiwa ni hizo hela zitanyofolewa toka wapi?

  Je huu ndo utaratibu kwa wizara zote kuhonga wabunge?

  Wabunge gani wanao hongwa?
  wale walio wengi na wanaweza kuipitisha kama wakiamua au wabunge wote kwa ujumla wao?
  Hii ni mara ya kwanza kufanya mchezo kama huu?

  Na kama hii sio mara ya kwanza,kuna mbunge anastahili kuaminiwa huko bungeni?
  Haijalishi ni wa chama gani,naimani kama hii kitu ipo miaka yote kwa namna
  Moja au nyingine lazima wabunge hata wa upinzani watakua wanajua,je kwanini wamekua kimya
  Siku zote hizo?

  Bajeti imeenda kurekebishwa,lakini bajeti general imekwisha pita na waziri wa nishati na madini
  alisema tatizo ni upungufu wa hela,
  je hizi hela zitatoka wapi wakati bajeti iliyo takiwa kurekebiswa mwanzo(general),imekwisha pita?

  Katika hali kama hii kuna mbunge anapaswa kuaminiwa pale anaposimama jukwaani
  na kukemea maovu ya wenzake?
   
 2. V

  Venoo Member

  #2
  Jul 24, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nasimama kusema wengi wamekimbilia kwenye nafasi za ubunge na kamati za kudumu kwa ajili ya ulaji tu.Nina sababu kusema hivi; nimewahi kushuhudia mazungumzo baina ya makamu mwenyekiti wa kamati mojawapo ya kudumu ya Bunge akihangaika kupata namba ya simu ya CEO wa shirika ili "kumsaidia" shirika lake litakapowasilsha taarifa yake!
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wabunge wote wa CCM wanajua huu ukweli na ndiyo maana hata leo wanamkimbia Mrema .Wabunge wa upinzani wanajionea makubwa na nadhani wako kimya wanajaribu kuujua ukweli uko vipi na kusema Bungeni hawawezi na wewe unajua alivyo yule mama sura mbaya so utawasikia majukwaani wanawapa somo wananchi .
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Waraka wa Jairo kwenda kwenye taasisi kwa ajili ya michango ina maneno, "kama ilivyo kawaida". Maana yake hii common trend.

  Na ndio nasema uchunguzu usiwe kwenye ofisi ya Jairo tu peke yake, wizara zote zimulikwe. Na hapa nahisi itakula kila upande hasa ile kamati ya Mrema. Hawa watu wamekuwa wanasamehe wafujaji hela kwenye local government waziwazi on camera. Kamati haina mamlaka kisheria kusamehe au kushitaki halmashauri, ila wanatakiwa watoe taarifa kwa bunge ili bunge kwa ujumla wake lichukuwe hatua. Sasa inakuwaje kamati inasamehe wizi?

  Jairo is nothing. bunge letu limeoza.
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu unategemea bunge la ndiyoooooooooooooo na nakubali 100 kwa 100 watafanya nini ? Hao ndiyo wanao tuhumiwa na wako wengi so usitegemee lolote hakuna cha Bunge na ndiyo maana wanatumia kila aina ya nguvu kushinda uchaguzi waunde serikali kwa kuwa wakishindwa mengi yatajulikana na walizo iba zote zitawatokea puani.Hakua bunge la aina hiyo Tanzania .Hadi CCM watakapokuwa wapinzani ndiyo utaona na kusikia mengi kwa sasa ni siasa tu .

  Hawa wamefanya ya Jairo wamefukia ya Kafulila now unaona hali hii ?Na wale walio pokea pesa je na ni wabunge mbona hawatajwi ?
   
 6. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Speaker hili ni swali muhimu sana badala ya kuhangaika na Jairo TAKUKURU inabidi ijikite hapa,kama Jairo alikuwa na uhakika hela zikipatikana kuna wabunge walikuwa tayari KUZIPOKEA.Jairo ni wa kushitakiwa mahakamani na abanwe kuwataja aliyetaka kuwapa kwa ahadi ya kupunguziwa mashitaka na atawataja tu.
   
 7. Tympa

  Tympa Member

  #7
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hapa inaonekana wabunge wengi sana wametumbukia kwenye hili shimo. Ila kama sikosei kuna taarifa zilisema kua MNYIKA aliwahi kugoma kupokea bahasha ambayo hakuambiwa ndani yake kuna nini.
   
 8. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana nawe kuwa uchunguzi ufanywe shida yangu ni kuwa ufanywe na nani? Serikali yenyewe chini ya CAG ijichunguze au Takukuru ya Hosea? Eti kisha ije na majibu kuwa kuna ni kweli...forget about it we have been there before. Je si CAG mwaka hadi mwaka anareport mishahara hewa kwa jana wa fedha ilifikia bilion 9 kama sijakosei..je ni nini kimefanyika?Serikali legelege ni kazi kweli kweli.
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Wabunge wote huwa wanachukuwa huo mgao inaoneka huo mgao umeanza siku nyingi hakuna mbunge wakumuamini tena
   
 10. T

  Tanganyika jeki JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Maswali yako yaonesha ni mmoja wa watanzania wachache wanaofikiri!! Angalau kwa hilo yatia moyo.

  Fuatlia mtiririko wa habari zifuatazo:-
  1. Gari la mbunge lakutwa na masanduku ya kura. Rais alimuona anafaa, akamteua kuwa waziri (naibu) - Makongoro. Rais alibariki hili
  2. Mbunge (wa NCCR, Kafulila) awatuhumu wabunge wenzake (akiwemo Zambi) kupokea hongo. Makamba mtoto alikiri hilo kutokea. Iliripotiwa Waziri Mkuu "aliwakemea" kwenye vikao vya ndani. Hakuna hatua ya maana liyochukuliwa
  3. Mbunge (Zitto) aliambia bunge kulikuwa na ushawishi usio halali "lobbying" kwa baraza la mawaziri kwa moja ya maamuzi yake. Zitto aliagizwa kuleta ushahidi. Akafanya hivyo. Mpaka sasa kimya kikuu!!
  4. Katibu mkuu wa wizara ya serikali aziagiza idara na taasisi zilizo chini yake kutoa sh milioni 50 za hongo ili bajeti ipite. Barua nakala yapelekwa Waziri Mkuu. Waziri mkuu (ajifanya) ashangaa. Ana pre-empt uamuzi. Rais k.k Katibu wake kiongozi afanya vinginevyo.

  Haya ni machache sana, lakini somo la kujifunza
  1. Baadhi ya wawakilishi wetu ni zao la rushwa
  2. Baadhi ya wawakilishi (wabunge) wetu ni watoaji na wapokeaji rushwa
  3. Mawaziri wetu ni sehemu ya rushwa. Wanabariki, wananyamazia, washiriki katika matendo ya rushwa
  4. Watendaji wakuu wa serikali ni wala na wapokea rushwa
  5. Serikali huionga (hutoa rushwa) serikali ili mambo yake yatendeke!!!!
  6. Serikali, bunge na (huenda mahakama) havina nia ya dahti kukomesha vitendo vya rushwa nchini
  7. Kuna ombwe la uongozi Tanzania
   
 11. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ukiwajumuisha wabunge wote wa ccm as if ndo wanamakosa utakua unakosea mkuu
  maana at the end of the day ni hao hao wa ccm ndo wametoboa siri,...

  Labda kama wanaohusishwa siku zote na huu uozo ni wale wa ccm,swali langu mimi ni
  kwa wabunge wote wa bunge letu,wawe wa chadema,cuf,tlp,nccr au ccm,....
  hawakujua haya siku zote?
  na kama walijua kwanini walikua kimya all this time?
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe,tukiacha ushabiki pembeni hakuna "mbunge" mwenye
  anae reflect maana halisi ya ubunge kwenye bunge letu,...wote wameoza na wananuka,...
  woooote ni wezi wakubwa sema wanazidiana viwango kutokana na nafasi zao
   
 13. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #13
  Jul 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sawa mkuu,lakini umesikia mbunge gani wa chadema,cuf,tlp,udp au nccr akiongelea hii ishu
  toka itokee?
  wote wana mlaani yule mama alotoa siri ya ulaji wao,no wonder wanaponda posho kumbe
  wana sehemu ya kuponea
   
 14. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #14
  Jul 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe mkuu,lakini hiyo red statement ni kitu cha mwisho nategemea
  kutokea
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  alotoa, hii lugha itakuwa Kishumundu ndani kabisa! Shule za kata ni janga la taifa kama kansa
   
 16. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  duh,uzoba ni mzigo kwa taifa,ila kwakua unapumua basi fanya kazi ulotumwa kufanya duniani
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Olutoa. Ulotumwa, kijana nenda shule unaona unavyoandika utumbo! Mimi sina cha kukusaidia zaidi ya kukupeleka shule za kata
   
 18. h

  hittler Member

  #18
  Jul 24, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hatua tuliyofikia ya kila anayetenda kosa either kwa kula rushwa kugawa rushwa kuingiza nchi katika hasara ua kushawishi rushwa kusafishwa na kuonekana hana hatia ni la ajabu sana na aibu mbele za umma.

  Kwa sababu hiyo basi ufisadi unaopigwa vita hautakaa uishe kwa sababu tuliowapa dhamana watuongoze au wasimamie rasilimali za nchi wamejitenge nakuona kuwa hao ndio bora zaidi na kuamua kufanya lolote watakalo kwa kuwa tu wanafahamiana kwa muda mrefu au wamewekana madarakani.

  Kwa sababu hizo Tanzania inahitaji mabadiliko makubwa sana ili tuweze kuwa na viongozi waadilifu na wazalendo wa kweli
   
Loading...