Noel Shao
Member
- Jan 19, 2017
- 89
- 185
BAJETI HII HAITA MUACHA MTU SALAMA.
Na Noel Shao
Kuna maswali yafaa tujiulize kwa bajeti ya serikali ya 2017/18.
1. Uelewa wa bajeti yenyewe kwa wasomi walio wengi umekuwa shida. Kwa mfano spika wa Bunge Job ndugai alisema “Kwa kweli hii haijawahi kutokea, ni kwa miaka mingi hatujawahi kuona bajeti nzuri kama hii.”
Kama spika wa Bunge anaweza sema hivi, halafu anashindwa ainisha, Chambua, oanisha mambo, unajiuliza kwa wale wasio enda shule itakuwa Je?
Mara nyingi utekelezaji wa bajeti huwa ni kama abradakaraba tu. Huwa hazitekelezeki zaidi ya shangwe kwenye maandishi na taaluma kuingiliwa na siasa. Yamkini yupo sahihi ila kaifananisha bajeti hii na ya miaka ipi hadi iwe bora kuwahi kutokea.? Hapa utagundua kuwa tatizo la wengi katika CCM ni kumbukumbu ndogo na ushabiki wa Chama.
Kadhalika, Kinacho msumbua spika nadhani ni uspika 2020. Ndugai hivi karibuni ameshindwa jitathimini kama anasema kwa niaba ya 'kiti' yaani wananchi au chama chake na matazamio ya madaraka.
2. Kitendo cha serikali kufuta Road License. Kwa lugha nyepesi ni kuwa serikali imefanya Biashara moja kubwa mno. Serikali imeamua kutumia lugha kufuta badala ya 'kuhamisha '. Tozo za road licenses zimehamishiwa kwenye mafuta na siyo zimefutwa.
Hii maana yake nini:-
a) Walala hoi, na wavuja jasho wote watashiriki kikombe hichi cha kulipa kodi. Mafuta yanapo ongezeka kila kitu hupanda bei, na ikumbukwe wananchi wengi vjijini bado ni watumiaji wa mafuta ya taa, pia auli zitapanda, kile kitendo cha kufuta kodi katika usafiri wa mazao, gharama zake utalipia kwenye mafuta.
Dhana ya 'serikali ya wanyonge' katika bajeti hii tumeuziwa maneno. Vitendo ni kuwa wanyonge hao watawasaidia mabwenyenye katika kulipa kodi.
b). Serikali hapa haijacheza na vichwa vya wavuja jasho pekee, bali hata wabunge. Nilishangaa kuona wabunge wanapiga meza kushangilia kile kilicho itwa "kufuta" wakasahau kuwa huu pia ulikuwa mtego na mchezo wa kucheza na lugha . Kwa sasa ni kuwa lile zoezi la baadhi wa wabunge, Mawaziri kukwepa kulipa kodi, katika hili hawana namna. Lazima mashangingi yao watayaweka mafuta. Sasa watakwepa vipi hapo.
Labda kukwepa huu mtego, kwa kuwa nao ni wajuvi wa kucheza na lugha waanzishe Petrol station zao "VIP " kama bima zao za afya. Au wawe na vitambulisho wakienda sheli waonyeshe.
3. Kitendo cha serikali kuu kuamua kukusanya ushuru hadi ule ulio kuwa unakusanywa na halimashauri mfano ushuru wa mabango kimenipa shaka mbili, moja, halimashauri wao wataingiza mapato kupitia nini? Au watabaki wanakusanya ushuru wa taka??? Pili, kitendo hichi kina wingu kisiasa.
Mwisho, Bunge letu linatia shaka kuliko matumaini. Halina meno, limekuwa kibogoyo kumumunya maneno ya serikali. Halina changamoto kwa serikali, katika mazingira kama haya huwa sioni uhalali wa kuwepo kwake. Kama wanashindwa kuipa changamoto serikali kwenye masuala kma haya, uhai bunge uko wapi??
Una mtazamo gani kuhusu bajeti ya 2017 /18
"Noel Shao
[HASHTAG]#mjenziWaTanzaniaMpya[/HASHTAG]