MTENDAHAKI
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,013
- 1,443
Acha ubabaishaji, hivi unakumbuka enzi zile hakuna VAT na kulikuwa na kodi ya kichwa??Unadhani ni kipindi gani mwananchi analipa kodi zaidi kati ya sasa na enzi za kodi ya kichwa??Nikusaidie jibu kwamba ni sasa (maana utanipotezea muda na lengo)!Huu ni mtindo wa kuwafanya wananchi walipe kodi biila shuruti kwa urafiki kadri ya uwezo wao na uwezo wa matumizi yao. Namna hizi za kodi zinaboresha mapato ya serikali huku zikiwafanya wananchi wasipate maumivu makali (kwa kulipa kiasi kidogokidogo) hivyo kuipa uwezo wa kupanua huduma zake pasipo kuwepo kwa malalamiko ya kundi fulani hasa la watu wanyonge!Nauli za daladala hupanda pia sio kwa sababu ya shs 40 ya mafuta sababu huwa zipo nyingi tu, watu wana - adjust kulingana na gharama mara nyingi! Hata sasa kuna route ikifika saa 12 nauli huwa mara 2 wakati bei ya mfuta ni ileilke, ni hulka tu! Upatikanaji wa kodi za kirafiki namna hii pia unaongeza hamasa kwa wananchi kujituma kufanya kazi ili wapate hela!Aisee, una kichwa kigumu kweli kweli kuelewa mantiki....
Ni kweli mafuta hupanda na kushuka bei kila wakati, kila siku.....
Lakini unasahau kuwa hii 40/= iliyoongezwa kwa kila lita ni fixed....
Mwezi huu kama lita ya petrol ni Tshs. 2200/= maana yake weka na ya Road Licence 40/= na kwa hiyo itakuwa 2240/=.... kwa kila mtu mwenye gari na asiye na gari !!
Mwezi ujao ikiwa 2150/= kwa lita, maana yake ongeza na ya Road Licence 40/= sawa na 2190/= kwa kila mtu mwenye gari na asiye kuwa nalo !!
Usiye na gari utalipaje hii kodi wakati huna gari ?
Ni rahisi tu, utalipia kwenye huduma zitokanazo na kutumia usafiri wa vyombo vya moto kama magari, Pilipili nk.... i. e nauli za usafiri wa abiria na bidhaa kupanda maradufu......
In return, ni kuwa, bei ya bidhaa itapanda am sema mfumko wa bei...!!!
Ukiangalia Road licence ilikuwa ni kodi inayobana kundi fulani tu wakati huduma za jamii zinazotolewa kutokana kodi hii zinatolewa kwa jamii yote, huoni mantiki ya watu wote kuchangia huduma??Obviously mwenye misere mingi ya gari atachangia zaidi na maskini atabalnce safari zake!
Nimetumia mifano rahisi ili twende sawa.
Mtendahaki