Kuna mambo yanakera sana

Kuna mambo yanakera sana

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
4,289
Reaction score
2,472
Yani nipo sehemu napata upepo mara unapigwa wimbo wa Juma Kakere. Kama ni mfuatiliaji wa muziki wa dance utaujua. Sasa ni wimbo mtamu sana, tena wa siku nyingi. Najiuliza, kilichomfanya kuimba wimbo mmoja kisha kushindwa kutoa tena wimbo mzuri ni nini?

Hapo ndio ninapoboreka na wasanii wa nchi hii (ukweli tasnia zote zinaboa). Fikiria kuna Kakere, Jumbe, Zoro, Bichuka, Majaliwa, n.k. Wote hawa wanaishia kuimba mahotelini tu. Hivi wakitoa nyimbo nzuri kwani zitakosa kupendwa? Kuna kizazi hapa kati kina ombwe la burudani. Mwisho tunaishia kusikiliza gospel hata sehemu zisizohusika.

Au tunasikiliza Bongo Fleva kabisa wakati lugha zao kwenye nyimbo baadhi, tena wengi wao haziakisi umri fulani.

Fikiria unasikiza wimbo mzuri halafu unasikia neno "Demu wangu". Nawasihi hawa wakongwe wa burudani wakiwepo kina Jaydee muimbe nyimbo nzuri kwa ajili ya kizazi chenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom