Kuna mambo watu wanayapitia ili wengine wajifunze

Kuna mambo watu wanayapitia ili wengine wajifunze

GEMBESON

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2012
Posts
1,463
Reaction score
3,200
Nimeiona hii kitu mahali, inaweza kuwafunza wengine humu.

Na. Irene Mbowe

Wasichana mlio kwenye Ndoa natamani sana mambo yafuatayo muyaishi na kuyazingatia;
Jitahidini kuwaheshimu waume zenu ili Ndoa ziwe na Amani na Furaha.

Unajua wengi mnasemaga, ‘Maisha nayaweza bila hata uwepo wa mwanaume’

Lakini nimewahi kusoma kwenye kitabu kitakatifu cha dini imeandikwa ‘BORA WAWILI KULIKO MMOJA’.*MHUBIRI 4:9-12 ‘Ni afadhali kuwa wawili kuliko mtu kuwa peke yake. Ikijatokea mmoja akaanguka, huyo mwenzake atamuinua. Lakini ole wake aliye peke yake, akianguka! Huyo hatakuwa na mtu wa kumuinua! Hali kadhalika, wawili wakilala pamoja watapata joto; lakini mtu akiwa peke yake atajipatiaje joto? Mtu akiwa peke yake aweza kushindwa na adui, lakini wakiwa wawili watamkabili na kumshinda adui. Kamba tatu zikisokotwa pamoja hazikatiki kwa urahisi.

Sikia, Hao single Mothers na wajane mkikaaa nao karibu wakaamua kufunguka bila Unafiki nawahakikishia kabisa watawaaambia maneno ambayo tafsiri yake huwa ni kama hiyo iliyoandikwa kwenye Mhubiri 4:9-12

Mpende, muheshimu, mjali na umuombee mumeo. Wengi mnatabia mkilala na waume zenu mnawapa mdinyo kwa kuringa, na hamtoi show za kibabe.

Nakuambia hivi,ukiachika, mwanaume ambaye utampata (tena kwa mbinde) Hutamfanyia huo ujinga na maringo na akuvumilie.

Nakuambia hivii, huko chumbani itakulazimu kujifunza harakati zote kwa lazima. Utake usitake.

Kuna Dada mmoja yeye alifiwa na mumewe miaka mitatu iliyopita, alinisimulia kuwa ‘Mume wake alikuwa anamnyima unyumba na hampi style fulani fulani na ukimuuliza akwambie kwa nini mume wake alikuwa hamfanyii haya anayoyafanya sasa, hana sababu ya msingi kabisa,. Lakini kwa huyu mpenzi aliyempata sasa inamlazimu kubinuka hasa na anafanya mpaka anajiogopa. Ili tu apate company yake na pesa kidogo za matumizi.

Anasema ‘Hata nichokaje sijawahi kumnyima tendo la ndoa’. Na ni lazima nimpe kwa ustadi sana. Unaweza usiniamini ila ukweli ndio huo, Napika chakula kwa ustadi hasa, na ninahakikisha amekula.

Akinikosea, simtukani wala kumpandishia sauti. Naongea kama malaika.

NIMEJIFANYIA TASMINI NIKAGUNDUA MIMI NI WIFE MATERIAL HASA. (Sijui kwa nini sikuyafanya haya kwa mume wangu)

Sifanyi haya kwa shida hapana, ila upweke , kuwa mmoja kunanilazimu nifanye haya. NAJICHUKIA TU KWA NINI MUME ALIPOKUWAPO SIKUFANYA HAYA?

Sikuwa najituma hata kidogo, sikuwa namjali hata kidogo. Ila sasa Naona namna nilivyokuwa nimepwaya.

Anasema ‘Sikuwa najua kuna dawa ya kukausha hedhi’. Kuna wakati inamlazimu kufanya ngono kwa kunywa dawa akaushe hedhi. Ili tu kumfurahisha mwanaume anayempa ada ya watoto. Ni mwanaume gani kwa sasa angependa majukumu? Tena kuhudumia Mke na watoto ambao sio wake?.

Nilifika mbali kidogo na kujiuliza, nikasema hivi ni mwamke gani anaweza kuwa na juhudi hizi za kubinuka sarakasi za kitandani kwa mumewe? Wanawake wengi walioolewa wamekuwa wavivu, hawajitumi na wamekuwa wanalalamika kuchoka, au kuchubuka. lakini hali hii haipo wanapotoa ofa kwa watu ambao sio waume Wao.

Binti hembu tafakari kwa umakini.
Unaweza kuijenga na kuiboresha ndoa yako ukaisukuma tu na kidole bila hata kutumia nguvu nyingi sana na ikafanikiwa kuwa imara na mume asije kufikiria kutoka nje.

Hivi,michepuko ama makahaba, nguvu ya kudatisha mwanaume wanatoa wapi? Nao ni wanawake ujue...

Tujiulize..
Wana shida sana?
Wanajua sana?
Ama ni nini?

NATAKA UHESHIMU KUWA WAWILI. KUWA MMOJA SIO JAMBO ZURI HATA KIDOGO. MHESHIMU NA MJALI HASA MUMEO.

Ni rahisi sana kusema ..Mjane ajifunze kutafuta pesa, asimamie watoto wake. Ni rahisi.

Swala la PESA Ni kitu kingine na Mtu ni Kitu kingine. Huo ndio ukweli. Sasa hivi Maisha yanaonekana ni pesa tu na sio utu. Wanaoolewa wanaona pesa tu na sio Utu. Yani Pesa kwanza Utu badae.Any way. Sikuingilii lakini huu ndio ukweli kama sio nusu ya ukweli....

NDOANI UKIENDEKEZA SANA PESA NAKUAMBIA MUME HUTAMJALI NG'O, NA ITAKUKOSTI.


Pesa zinatusaidia sana lakini isifike mahali pesa ikabeba Thamani ya Utu wa mtu. Hasa Mume. uwezo wa kuwa na ndoa nzuri uko mkononi mwako

**************
 
Wanaume tunaopitia changamoto za ndoa pindi tuonapo andiko kama hizi tunafarijika sana na kujiuliza inamaana hawa wake zetu huwa hawaoni maandiko mazuri kama haya kweli? Au kwa sababu wameshaizoea ndoa basi wanafanya bora liende!
 
Wanaume tunaopitia changamoto za ndoa pindi tuonapo andiko kama hizi tunafarijika sana na kujiuliza inamaana hawa wake zetu huwa hawaoni maandiko mazuri kama haya kweli? Au kwa sababu wameshaizoea ndoa basi wanafanya bora liende!
Ndoa ndoa ndoa
 
Amini nakuambia ndoa haina kanuni kwani ukipendacho wewe mm nakiona kawaida tu sometimes tunapendwa lkn tunakuwa hatujapenda
 
Mnyanduo uendelee nasema huyu asiponibinukia Kama mchepuko napiga chini
 
Wanaume tunaopitia changamoto za ndoa pindi tuonapo andiko kama hizi tunafarijika sana na kujiuliza inamaana hawa wake zetu huwa hawaoni maandiko mazuri kama haya kweli? Au kwa sababu wameshaizoea ndoa basi wanafanya bora liende!
Wakat mwngne mabadliko ya mwanamke yanatokana na mwanaume.....​
 
Wanaume tunaopitia changamoto za ndoa pindi tuonapo andiko kama hizi tunafarijika sana na kujiuliza inamaana hawa wake zetu huwa hawaoni maandiko mazuri kama haya kweli? Au kwa sababu wameshaizoea ndoa basi wanafanya bora liende!
Kama yupo humu mwambie asome.
 
Mleta uzi naomba aliyeandika huo uzi,,,, apewe kila kitu anachotaka
 
Back
Top Bottom