Wanabodi,
Moja ya faida za mitandao ni kuelimishana, hili ni bandiko la kutoa elimu kuwa japo kisheria makanisa yote yana hadhi sawa mbele ya sheria,lakini japo ni mchungu,lakini ndio ukweli wenyewe, kuwa makanisa hayafanani, Kuna Makanisa na Makanisa!,Makanisa makubwa, ,makanisa madogo, kuna Vikanisa vidogo na vijikanisa vidogo kabisa!, bila kujalisha ukumbwa wa jengo la kanisa, au uwingi wa waumini wa kanisa husika, mbele ya sheria, makanisa yote yako sawa!.
Kitendo cha kufungiwa kwa kanisa la Ufufuo wa uzima, ndiko kumeniibua kuulizia hili jambo, kuwa kuna Makanisa fulani hata yafanye nini hayawezi kufungiwa, na kuna makanisa mengine, ile kiongozi wake amekohoa tuu, limepigwa kabali?。
Japo ni kweli nchi yetu haina dini, secular state, na serikali yetu haina dini,secular government,lakini watu wake wana dini zao na viongozi wana dini zao.
Sasa ili kuepuka mifarakano ya kidini,serikali ikasisitiza viongozi wa dini wasichanganye dini na siasa, lakini je kuna dini ni muhimu zaidi ya nyingine, zinaheshimiwa na zinaogopwa hivyo viongozi wake wanaweza kusema lolote, popote, hata kuchanganya dini na siasa na wasifanywe lolote au kitu chochote, lakini wengine wakiongea wanafungiwa kwa kisingizio cha kuchanganya dini na siasa?
Hii hoja ya kuchanganya dini na siasa niliifanyia kipindi
View: https://youtu.be/_iDRrF9NqwA?si=w7VV-UBf_TYW9o34
Kuna dhehebu huwa linatoa waraka nikauliza
Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?
Waraka huo ulisomwa altareni, misa zote na jumuiya ndogo ndogo zote na haikuwa waraka wa neno la Mungu nikashauri
Je, Wajua Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu? Ili Kuepuka Kuchanganya Dini na Siasa, Kuna Haja Waumini Tuambiwe Ukweli Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu?
2016 baada ya Rais Magufuli kusema katiba sio kipaumbele changu, Baba Askofu Severini Niwemugizi,wa Jimbo Katoliki la Rulenge,alimshukia JPM mimbarini, JPM akajibu mapigo kwa Baba Askofu kushughulikiwa kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kunyanganywa passport na kuhojiwa uraia lakini kanisa halikufungwa!。
Mwaka 2010 Askofu Zakaria Kakobe aliwagomea Tanesco kupitisha umeme wa high voltage mbele ya kanisa lake
Askofu Kakobe Asipuuzwe: Ni kama David Koresh na Camp Davidians! halikufungiwa!。
Mwaka 2017, Askofu Kakobe alimuamuru Rais JPM lazima utubu kwa Mungu dhambi zake na asipotubu atakufa!,Kakobe ni alishughulikiwa yeye,akahojiwa uraia lakini kanisa lake halikufungwa!
Kauli ya Kakobe "Magufuli atubu", yaibua mambo! Je asili halisi ya Rais Magufuli ni Msukuma, Mhaya au Muha wa Kakonko?,
Mwaka 2012 Askofu Nabii na Mtume Mwingira aliipaka
Serikali, kanisa la Efata lilivamiwa na polisi, kutaka kumkamata Mwingira, waumini wakamkingia
, polisi walitembeza
Kichapo
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know! lakini kanisa halikufungiwa!
Ukiondoa kanisa la Kakobe,kanisa jingine lililofungiwa ni kanisa la Mfalme Zumaridi kule Mwanza na kanisa la Kiboko ya Wachawi ambapo nami nilitoa ushauri
Serikali iingilie kati Makanisa ya Miujiza? Watanzania masikini wa kutupwa wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli huku wahubiri wakigeuka mamilionea
Hitimisho
Kwa vile mbele ya macho ya kisheria,makanisa yote yana hadhi sawa,natoa vito kwa serikali yetu tukufu,makanisa yote yawe treated equal,sio makanisa mengine yahubiri siasa hayaguswi mengine yanaguswa!,kosa la mtu mmoja,haliwezi kusababisha kanisa lote kufungwa!,ila pia ukiondoa ile kadhia ya Msikiti wa Mwembechai, sijawahi kusikia msikiti wowote kufungwa kwa kuchanganya dini na siasa!, wenzetu misikitini ni ibada tuu na mafundisho ya neno la Mungu tuu,
Nashauri makanisa waweke jukwaa nje ya kanisa baada ya ibada, kiongozi apande jukwaani apige siasa kadri atakavyo, kutakuwa hakuna tatizo。
Hili mnalionaje?。
Paskali