Kuna Makanisa na Makanisa Kuanzia Makanisa,Vikanisa,Kikanisa na Vijikanisa!, Je Makanisa Yote Yanaweza Kufungiwa?au Vikanisa, Vijikanisa na Kikanisa?

Kuna Makanisa na Makanisa Kuanzia Makanisa,Vikanisa,Kikanisa na Vijikanisa!, Je Makanisa Yote Yanaweza Kufungiwa?au Vikanisa, Vijikanisa na Kikanisa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,103
Reaction score
128,721
Wanabodi,

Moja ya faida za mitandao ni kuelimishana, hili ni bandiko la kutoa elimu kuwa japo kisheria makanisa yote yana hadhi sawa mbele ya sheria,lakini japo ni mchungu,lakini ndio ukweli wenyewe, kuwa makanisa hayafanani, Kuna Makanisa na Makanisa!,Makanisa makubwa, ,makanisa madogo, kuna Vikanisa vidogo na vijikanisa vidogo kabisa!, bila kujalisha ukumbwa wa jengo la kanisa, au uwingi wa waumini wa kanisa husika, mbele ya sheria, makanisa yote yako sawa!.

Kitendo cha kufungiwa kwa kanisa la Ufufuo wa uzima, ndiko kumeniibua kuulizia hili jambo, kuwa kuna Makanisa fulani hata yafanye nini hayawezi kufungiwa, na kuna makanisa mengine, ile kiongozi wake amekohoa tuu, limepigwa kabali?。

Japo ni kweli nchi yetu haina dini, secular state, na serikali yetu haina dini,secular government,lakini watu wake wana dini zao na viongozi wana dini zao.

Sasa ili kuepuka mifarakano ya kidini,serikali ikasisitiza viongozi wa dini wasichanganye dini na siasa, lakini je kuna dini ni muhimu zaidi ya nyingine, zinaheshimiwa na zinaogopwa hivyo viongozi wake wanaweza kusema lolote, popote, hata kuchanganya dini na siasa na wasifanywe lolote au kitu chochote, lakini wengine wakiongea wanafungiwa kwa kisingizio cha kuchanganya dini na siasa?

Hii hoja ya kuchanganya dini na siasa niliifanyia kipindi
View: https://youtu.be/_iDRrF9NqwA?si=w7VV-UBf_TYW9o34

Kuna dhehebu huwa linatoa waraka nikauliza Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?

Waraka huo ulisomwa altareni, misa zote na jumuiya ndogo ndogo zote na haikuwa waraka wa neno la Mungu nikashauri Je, Wajua Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu? Ili Kuepuka Kuchanganya Dini na Siasa, Kuna Haja Waumini Tuambiwe Ukweli Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu?

2016 baada ya Rais Magufuli kusema katiba sio kipaumbele changu, Baba Askofu Severini Niwemugizi,wa Jimbo Katoliki la Rulenge,alimshukia JPM mimbarini, JPM akajibu mapigo kwa Baba Askofu kushughulikiwa kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kunyanganywa passport na kuhojiwa uraia lakini kanisa halikufungwa!。

Mwaka 2010 Askofu Zakaria Kakobe aliwagomea Tanesco kupitisha umeme wa high voltage mbele ya kanisa lake Askofu Kakobe Asipuuzwe: Ni kama David Koresh na Camp Davidians! halikufungiwa!。

Mwaka 2017, Askofu Kakobe alimuamuru Rais JPM lazima utubu kwa Mungu dhambi zake na asipotubu atakufa!,Kakobe ni alishughulikiwa yeye,akahojiwa uraia lakini kanisa lake halikufungwa!Kauli ya Kakobe "Magufuli atubu", yaibua mambo! Je asili halisi ya Rais Magufuli ni Msukuma, Mhaya au Muha wa Kakonko?

Mwaka 2012 Askofu Nabii na Mtume Mwingira aliipaka
Serikali, kanisa la Efata lilivamiwa na polisi, kutaka kumkamata Mwingira, waumini wakamkingia
, polisi walitembeza
Kichapo Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know! lakini kanisa halikufungiwa!

Ukiondoa kanisa la Kakobe,kanisa jingine lililofungiwa ni kanisa la Mfalme Zumaridi kule Mwanza na kanisa la Kiboko ya Wachawi ambapo nami nilitoa ushauri Serikali iingilie kati Makanisa ya Miujiza? Watanzania masikini wa kutupwa wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli huku wahubiri wakigeuka mamilionea

Hitimisho
Hii maana yake Tanzania tuna makanisa na makanisa,mengine ni makanisa,na mengine ni vikanisa, makanisa hayafungiwi bali vikanisa, huu ni ubaguzi!

Kwa vile mbele ya macho ya kisheria,makanisa yote yana hadhi sawa,natoa vito kwa serikali yetu tukufu,makanisa yote yawe treated equal,sio makanisa mengine yahubiri siasa hayaguswi mengine yanaguswa!,kosa la mtu mmoja,haliwezi kusababisha kanisa lote kufungwa!,ila pia ukiondoa ile kadhia ya Msikiti wa Mwembechai, sijawahi kusikia msikiti wowote kufungwa kwa kuchanganya dini na siasa!, wenzetu misikitini ni ibada tuu na mafundisho ya neno la Mungu tuu,

Nashauri makanisa waweke jukwaa nje ya kanisa baada ya ibada, kiongozi apande jukwaani apige siasa kadri atakavyo, kutakuwa hakuna tatizo。

Hili mnalionaje?。

Paskali
 
Unaposema Kanisa, maana yake ni mahali watu wanapoenda kujipatia shibe ya roho kulingana na imani zao. Kosa la mtu mmoja halikupaswa kuwanyima wengine huduma hiyo.
Tatizo kwa kanisa hilo,huwezi kutenganisha kanisa na mropokaji,yeye ndiyo kanisa kanisa ndiyo yeye, kiongozi mkuu wa kanisa kuongelea siasa kanisani huwezi tenganisha kanisa na hizo kauli za siasa
 
Unaposema Kanisa, maana yake ni mahali watu wanapoenda kujipatia shibe ya roho kulingana na imani zao. Kosa la mtu mmoja halikupaswa kuwanyima wengine huduma hiyo.
Hata huyo mmoja kosa lake ni lipi? Sidhani kama kukemea utekwaji, uuliwaji, uteswaji ni kosa kisheria.
Au kosa kubwa ilikuwa ni kutoa mfano wa mtoto wa mkubwa ikitokea amekamatwa na kesho yake akapatikana hana macho ndilo lilikuwa kosa la mpaka kufungia waumini wasipate haki yao ya msingi ya kuabudu? Kama kutolewa mfano tu mtoto pendwa imekuwa hivyo mkuu wa nchi anadhani wazazi wa mdude na wengine waliopotezwa wana maumivu gani mioyoni mwao.
 
Wanabodi,

Moja ya faida za mitandao ni kuelimishana, hili ni bandiko la kutoa elimu kuwa japo kisheria makanisa yote yana hadhi sawa mbele ya sheria,lakini japo ni mchungu,lakini ndio ukweli wenyewe, kuwa makanisa hayafanani, Kuna Makanisa na Makanisa!,Makanisa makubwa, ,makanisa madogo, kuna Vikanisa vidogo na vijikanisa vidogo kabisa!, bila kujalisha ukumbwa wa jengo la kanisa, au uwingi wa waumini wa kanisa husika, mbele ya sheria, makanisa yote yako sawa!.

Kitendo cha kufungiwa kwa kanisa la Ufufuo wa uzima, ndiko kumeniibua kuulizia hili jambo, kuwa kuna Makanisa fulani hata yafanye nini hayawezi kufungiwa, na kuna makanisa mengine, ile kiongozi wake amekohoa tuu, limepigwa kabali!.
Kuna Pascal, Paskali, Pasco wote hawawezi kuwa sawa.

"All animals are equal, but some animals are more equal than others"
- George Orwell
 
Unaposema Kanisa, maana yake ni mahali watu wanapoenda kujipatia shibe ya roho kulingana na imani zao. Kosa la mtu mmoja halikupaswa kuwanyima wengine huduma hiyo.
kanisa sio jengo broo Paskali, ni mkusanyiko wa waaminio

Sasa wamefunga jeno ila kanisa la Mungu hakijafungwa, popote wanaweza kukusanyika, hata wawili na wakasali
 
Tatizo kwa kanisa hilo,huwezi kutenganisha kanisa na mropokaji,yeye ndiyo kanisa kanisa ndiyo yeye, kiongozi mkuu wa kanisa kuongelea siasa kanisani huwezi tenganisha kanisa na hizo kauli za siasa
DINI NI SIASA DINI INAHAMASISHA HAKI,DINI INAJENGA SHULE,DINI INAHAMASISHA MAADILI RUDI CHUO AU SECONDAR KASOME TENA
 
Wanabodi,

Moja ya faida za mitandao ni kuelimishana, hili ni bandiko la kutoa elimu kuwa japo kisheria makanisa yote yana hadhi sawa mbele ya sheria,lakini japo ni mchungu,lakini ndio ukweli wenyewe, kuwa makanisa hayafanani, Kuna Makanisa na Makanisa!,Makanisa makubwa, ,makanisa madogo, kuna Vikanisa vidogo na vijikanisa vidogo kabisa!, bila kujalisha ukumbwa wa jengo la kanisa, au uwingi wa waumini wa kanisa husika, mbele ya sheria, makanisa yote yako sawa!.

Kitendo cha kufungiwa kwa kanisa la Ufufuo wa uzima, ndiko kumeniibua kuulizia hili jambo, kuwa kuna Makanisa fulani hata yafanye nini hayawezi kufungiwa, na kuna makanisa mengine, ile kiongozi wake amekohoa tuu, limepigwa kabali!.

Makanisa ni yanayothubutu kusimama na ukweli hata kama ni mchungu, si vijikanisa!

FB_IMG_17488591375144467.jpg

Wenye akili zetu kwenye hili, tunasimama na Gwajima dhidi ya watekaji, watesaji, wauwaji na wafiraji, je wewe?

Naamini hata mama atakuwa nasi. Hawezi kuwa sehemu ya wafiraji au wewe hudhani hivyo?
 
Back
Top Bottom