Kuna Majogoo wa Jirani wanawika Saa 6 hii ya usiku je ni Majogoo kweli au ndiyo wale Ndugu zetu?

Ondoa woga na mtumainie Mungu utashinda

Sasa unaniambia nimtumainie Mungu wakati hapa nilipo hata sikumbuki ni wapi nimeiweka ' Biblia ' yangu ili kusudi labda niikumbatie ninapolala ili hawa Kwiyo Kwiyo Watu wasinichawie. Kumba ndiyo maana kwa siku za karibuni kila nikiamka tu najikuta miguu yote ina vumbi tena la Kutukuka kabisa Mkuu.
 
GENTAMYCINE. Hao wametoka Shamba wakiona Umeme hudhani kumekucha
Au yeye ndo ametoka shamba, mbona haya majogoo ya mjini ni kawaida sana? Hayana usiku wala masaa, full mwanga. Halafu, mjini wote au wengi wana saa, yeye bado anategemea jogoo kumuamsha? Jokes.
 
Tangia nizaliwe ' hakyanani ' sijawahi kusikia ' Jogoo ' akiwika / wakiwika mida hii ya Saa Sita ( 6 ) za usiku kama huu ila nashangaa muda huu naandika huu ' uzi ' huko nje nyumba ya Jirani ' Majogoo ' yameanza ' kuwika ' tena kwa fujo na yanapokezana.

Je hawa ni ' Majogoo ' kweli au labda wale Ndugu zetu ( Wachawi / Wanga ) ndiyo wanaitana sasa ili kufanya ' parade ' yao ya kuanza kutuchosha kwa ' kutulimisha ' na ' kutubebesha ' mizigo mizito usiku kucha huu?

Naombeni msaada wenu tafadhali kwani kwa ' kuwika ' Kwao huku hawa ' Majogoo ' tayari nimeshaingiwa na hofu hasa ukizingatia siku mbili hizi kila nikiamka najikuta nimechoka mno halafu miguu ina vumbi tupu utadhani nilikuwa nafyeka uwanja wa Simba SC kule Bunju.

Nawasilisha.
Usilale leo, hawatakuchukua, kesha tu baani.
 
Na mbona sasa wakiwika wanaelekezea Shingo na Sauti zao upande wa dirisha langu Mkuu? Nimewakosea nini? au labda wanadhani na Mimi nipo pengine katika list ile ya Makinikia hivyo wanataka ' kuninyoosha ' kwa ' kuniadhibu ' mapema? Hii sijapata kuona katika maisha yangu yaani ' Majogoo ' yanawika mapema hivi Saa Sita ( 6 ) hii kweli! Ninavyojua wengi muda wao wa kuwika huanzia Saa 9 usiku au Saa 10 alfajiri ila hii ya Saa 6 hii ndiyo naishuhudia rasmi leo tokea nizaliwe. Na hata huko Vijijini huwa naenda kutembelea na wanafuga sana hawa Kwiyo Kwiyo / Kuku ila huwa ' hawawiki ' Saa 6 kama hawa.

Halafu hata Biblia yangu nayo nimesahau nilipoiweka kwani ni muda mrefu umepita tokea niishike achilia mbali kuifungua tu na kusoma ' maandiko '. Leo nitakiona cha moto ' wajameni '.
Ila Gent hunaga akili walahi aisee
Na utakiona cha mtema kuni..
 
Mentality za kuwa na sababu za kishirikina kwa kila kitu ni mentality zisizo na uwezo wa kufikiri. Finyu.

Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda.
 
Tangia nizaliwe ' hakyanani ' sijawahi kusikia ' Jogoo ' akiwika / wakiwika mida hii ya Saa Sita ( 6 ) za usiku kama huu ila nashangaa muda huu naandika huu ' uzi ' huko nje nyumba ya Jirani ' Majogoo ' yameanza ' kuwika ' tena kwa fujo na yanapokezana.

Je hawa ni ' Majogoo ' kweli au labda wale Ndugu zetu ( Wachawi / Wanga ) ndiyo wanaitana sasa ili kufanya ' parade ' yao ya kuanza kutuchosha kwa ' kutulimisha ' na ' kutubebesha ' mizigo mizito usiku kucha huu?

Naombeni msaada wenu tafadhali kwani kwa ' kuwika ' Kwao huku hawa ' Majogoo ' tayari nimeshaingiwa na hofu hasa ukizingatia siku mbili hizi kila nikiamka najikuta nimechoka mno halafu miguu ina vumbi tupu utadhani nilikuwa nafyeka uwanja wa Simba SC kule Bunju.

Nawasilisha.

Inawezekana ndio mkuu, especially kama hayo majogoo yakiwa yakizungu.. hayanaga formula za kuwika.
 
Back
Top Bottom