Kuna Majogoo wa Jirani wanawika Saa 6 hii ya usiku je ni Majogoo kweli au ndiyo wale Ndugu zetu?

afadhari kwako mimi jiran na kwangu yamekusanyana mapaka kama matano hivi yaani ni kelele mtindo mmoja
 
Salama tu Kiongozi. Mmmmmh Kiongozi hawa ' Jogoo ' nawaogopa sana kwani wanawika sana na siyo kawaida yao kabisa. Sasa sijui labda wamewaona akina mshana jr na MziziMkavu wakipaa angani kuwanga au la!
Nimecheka sana ujue, binadamu tunajitengezea hofu wenyewe kisha tunajitisha wenyewe kisha tunalia wenyewe, mkuu ondoa hayo mawazo ya uhirikina utaishi kwa aman sana hapa duniani.
Washirikina huwa na athari kwa wale wanao waamin tu.

Relax and enjoy living
 
Tangia nizaliwe ' hakyanani ' sijawahi kusikia ' Jogoo ' akiwika / wakiwika mida hii ya Saa Sita ( 6 ) za usiku kama huu ila nashangaa muda huu naandika huu ' uzi ' huko nje nyumba ya Jirani ' Majogoo ' yameanza ' kuwika ' tena kwa fujo na yanapokezana.

Je hawa ni ' Majogoo ' kweli au labda wale Ndugu zetu ( Wachawi / Wanga ) ndiyo wanaitana sasa ili kufanya ' parade ' yao ya kuanza kutuchosha kwa ' kutulimisha ' na ' kutubebesha ' mizigo mizito usiku kucha huu?

Naombeni msaada wenu tafadhali kwani kwa ' kuwika ' Kwao huku hawa ' Majogoo ' tayari nimeshaingiwa na hofu hasa ukizingatia siku mbili hizi kila nikiamka najikuta nimechoka mno halafu miguu ina vumbi tupu utadhani nilikuwa nafyeka uwanja wa Simba SC kule Bunju.

Nawasilisha.
Jogoo akiwika saa 6 ni dalili ya kutatokea kifo hapo mahali. Jogoo anatakiwa awike alfajiri sio saa 6 usiku.
 
Mentality za kuwa na sababu za kishirikina kwa kila kitu ni mentality zisizo na uwezo wa kufikiri. Finyu.

Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda.
nenda mwenyewe hiyo safari dada, wengine hatuendi! Tunafanya kazi.
 
Zamani majogoo waliwika alfajiri kutokana na mazingira ya kipindi kile jua na mwanga huanza kuonekana alfajiri. Siku izi Kuna umeme mwanga upo almost mda wote ndo maana majogoo huwika hata saa sita usiku kwa sababu ya mwanga wa umeme. Sio uchawi mkuu. Kuhusu vumbi miguuni mhh ilo sijui
 
Tangia nizaliwe ' hakyanani ' sijawahi kusikia ' Jogoo ' akiwika / wakiwika mida hii ya Saa Sita ( 6 ) za usiku kama huu ila nashangaa muda huu naandika huu ' uzi ' huko nje nyumba ya Jirani ' Majogoo ' yameanza ' kuwika ' tena kwa fujo na yanapokezana.

Je hawa ni ' Majogoo ' kweli au labda wale Ndugu zetu ( Wachawi / Wanga ) ndiyo wanaitana sasa ili kufanya ' parade ' yao ya kuanza kutuchosha kwa ' kutulimisha ' na ' kutubebesha ' mizigo mizito usiku kucha huu?

Naombeni msaada wenu tafadhali kwani kwa ' kuwika ' Kwao huku hawa ' Majogoo ' tayari nimeshaingiwa na hofu hasa ukizingatia siku mbili hizi kila nikiamka najikuta nimechoka mno halafu miguu ina vumbi tupu utadhani nilikuwa nafyeka uwanja wa Simba SC kule Bunju.

Nawasilisha.
Hahahahaaa. Eti wanga wanaitana kwenye parade!
 
Zamani majogoo waliwika alfajiri kutokana na mazingira ya kipindi kile jua na mwanga huanza kuonekana alfajiri. Siku izi Kuna umeme mwanga upo almost mda wote ndo maana majogoo huwika hata saa sita usiku kwa sababu ya mwanga wa umeme. Sio uchawi mkuu. Kuhusu vumbi miguuni mhh ilo sijui
Mkuu yanaanzaga kuwika saa tisa usiku , then yana wika tena baada ya muda hivyo hivyo mpaka kuna kucha, hayasubiri mwanga wa alfajiri,
Hayo ya saa sita usiku kuna kitu kingine hapo mbali na taa za umeme,
 
Ukiona jogoo amewika wakati wa usiku kabla ya muda wa alfajiri basi Amka usome dua, viumbe hao uwa wanaona malaika, jitahidi sana usome dua kwa Mwenyezi Mungu, maana malaika wanakuwa karibu na maeneo hayo.
Kuna kipindi malaika wanakuwa mbali na maeneo kumbe? Basi lazima dhambi zingine wawe wanashindwa kuzinakili vitabuni mwao wakiwa mbali, mi ningependa wawe watakuja kwangu mchana tu, daftari langu litakuwa safi jeupeee?
 
Back
Top Bottom