Na jimbo la Polepole, Bashilu na Kheri ni lipi?Tatizo mkiruhusiwa hamjui jinsi yakuongea na wananchi mmejaa mitusi tu, midomo michafu utazani sio waheshimiwa. Siasa kila mtu afanyie jimboni kwake. Ila CCM wanauhalali kwakuwa walishinda Uraisi jimbo la Raisi ni Tz nzima, hawana mipaka.
Acha Ufa.la weweMkuu huo ndio mfumo ulivyo kwa Sasa
Nawashauri mngekifuta chama chenu
Sasa si wanatoka kwenye chama kilichoshika dola? Hujui kuwa serikali inaongozwa na ilani ya CCM?
Eti demokrasia ni kufanya kazi......ok, sasa vijana wanafanya kazi ya betting, na inaingiza kodi kwelikweli, na yeye bipolar anapenda kodi.Kichaa huyo hajui asemalo wala atendalo.
Eti demokrasia ni kufanya kazi......ok, sasa vijana wanafanya kazi ya betting, na inaingiza kodi kwelikweli, na yeye bipolar anapenda kodi.
Tuone kama atafuta hii demokrasia-betting.
Sent using Jamii Forums mobile app
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)MKOA WA IRINGA
TAARIFA
Kuna Maandamano ya CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WILAYA YA MUFINDI, MKOA WA IRINGA Yakiongozwa na Viongozi wao Kitaifa akiwepo Mhe. Pinda Waziri Mkuu Mstaafu.
Tunapenda Wananchi mjue Siku Chache vyombo Vya Dola/polisi vilizuia kikao cha Ndani kwa Amri ya DC wa Mufundi, ilipelekea polisi kuvuruga kikao chetu Kwa ndani kilichotakiwa kuongoza na Naibu Katibu Zanzibar Mhe. Salum Mwalimu, tuliishia mikononi mwa Jeshi la Polisi Kwa kipigo na kutukamata, Kutudharirisha, na kuzuia Kikao chetu cha Ndani kutokufanyika
Pili mtakumbuka Rais Magufuli amepiga marufuku Mikutano ya hadhara na Maandamano Kwa vyama vya siasa, Kwa Maandamano yanayoendelea wilaya ya Mufindi chini ya Viongozi Waandamizi Wa CCM, Je Rais Magufuli amefuta tamko lake la Awali la kuzuia Mikutano ya hadhara na maandamano?
Au Hii ndo Tafsiri Sahihi ya Kauli ya Mwenyekiti Wa CCM Taifa Kuwa Demokrasia inamipaka, Hii ndo Mipaka ya Demokrasia kwa CCM pekee Kufanya Maandamano huku Vyama Vingine Vikizuiliwa Kufanya Mikutano ya Hadhara na Maandamano Kama ilivyo kwa CCM
Vitendo Vya kuzuiliwa CHADEMA Tunachukulia kama ni Uvunjwaji Wa makusudi Sheria iliyoanzisha Vyama vya Siasa, ni Uporaji Wa haki za Vyama vyote na Ubaguzi wa waziwazi.
Chadema tunaliona likifanywa na vyombo vya Usalama ili kunusuru anguko kubwa la CCM, zaidi ni hofu ya CCM kuondoka madarakani mapema kwasababu imechokwa na wananchi na inaona njia ya pekee ya kuzuia ukuaji wa Vyama vya Upizani ni Kuzuia vikao vya ndani, Mikutano ya hadhara na maandamano lakini chama CCM wakifanya tena kwa ulinzi wa polisi ambao wanawazuia Chadema na Upinzani Kwa ujumla.
Tunapenda Wananchi Kujua CCM imechokwa, imepoteza Ushawishi tena kwa Wananchi Mkoa Wa Iringa, Maandamano wanayofanya ni kuwahadahaa na kuwaongopea Wananchi kuwa Chama Chao Bado kinaungwa mkono na Wananchi, wakati sio kweli.
Chadema Mkoa wa Iringa Tuna laani Sana upendeleo (Double standards) usiokuwa na aibu unaofanywa na Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa maana tunafahamu kabisa kwamba RPC anajua kinachofanyika Mafinga.
TUNAPENDA Kufahamisha Wananchi Wote waelewe kwamba mwaka 2019 SIKU ZA KUENDELEA KUTII MATAMKO YANAYOKWENDA KINYUME NA SHERIA NA KATIBA YA NCHI ZINAHESABIKA KWA WATAWALA tutapambana kuzidai haki zetu zote tunazonyimwa kinyume na sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama vyama vya siasa vyenye uhalali na vyenye utaratibu uliowekwa rasmi kisheria na kikatiba, tutatangaza rasmi namna na utaratibu wa kufanya mikutano yetu ya hadhara katika kila kona ya MKOA WA IRINGA, hatutaruhusu katazo haramu na lisilo na mashiko ya kisheria litumike kutuzuia kutekeleza wajibu wetu
_
Jackson mnyawami
Katibu CHADEMA
Mkoa Wa_ Iringa
Ndivyo katiba na sheria ya vyama vya siasa zinavyosema?!Sasa si wanatoka kwenye chama kilichoshika dola? Hujui kuwa serikali inaongozwa na ilani ya CCM?
utawala wa awamu ya 5 hauna kabisa ile aibu ambayo Mungu amewapa wanadamu , ni kama awamu ya wanyama , nachukua nafasi hii kumuonya Mizengo Pinda , tulimuheshimu kwa vile alijiheshimu , sasa maadam ameamua Liwalo na liwe basi akae mkao wa kula , hatutaki lawamaHawa watu hata sijui aibu waliisalimisha wapi.
Tutakula wapi tukifuta chama? Hii ndo Ajira yetuMkuu huo ndio mfumo ulivyo kwa Sasa
Nawashauri mngekifuta chama chenu
Mkuu huo ndio ukweli
Mkifosi mtaishia jelaTutakula wapi tukifuta chama? Hii ndo Ajira yetu
😱😱😱tunajua mwaka huu tunaweza itwa ikulu kunywa kahawaMkifosi mtaishia jela
Wanashindwa mapambano na wake zao majumbani wataweza mapambano na Serikali?Bado mnaendelea kuhesabu? Si mlisema mwaka huu ni wa mapambano?
Kelele za chura anazo mama yako.Tumechoka na matamko yenu ya kila siku yasiokuwa na mafanikio yoyote hizo ni sawa sawa na kelele za chura tu
Sent using Jamii Forums mobile app