Kuna Maandamano ya CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WILAYA YA MUFINDI, MKOA WA IRINGA Yakiongozwa na Viongozi wao Kitaifa akiwepo Mhe. Pinda Waziri Mkuu Mstaaf

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,260
2,000
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)MKOA WA IRINGA

TAARIFA

Kuna Maandamano ya CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WILAYA YA MUFINDI, MKOA WA IRINGA Yakiongozwa na Viongozi wao Kitaifa akiwepo Mhe. Pinda Waziri Mkuu Mstaafu.

Tunapenda Wananchi mjue Siku Chache vyombo Vya Dola/polisi vilizuia kikao cha Ndani kwa Amri ya DC wa Mufundi, ilipelekea polisi kuvuruga kikao chetu Kwa ndani kilichotakiwa kuongoza na Naibu Katibu Zanzibar Mhe. Salum Mwalimu, tuliishia mikononi mwa Jeshi la Polisi Kwa kipigo na kutukamata, Kutudharirisha, na kuzuia Kikao chetu cha Ndani kutokufanyika

Pili mtakumbuka Rais Magufuli amepiga marufuku Mikutano ya hadhara na Maandamano Kwa vyama vya siasa, Kwa Maandamano yanayoendelea wilaya ya Mufindi chini ya Viongozi Waandamizi Wa CCM, Je Rais Magufuli amefuta tamko lake la Awali la kuzuia Mikutano ya hadhara na maandamano?

Au Hii ndo Tafsiri Sahihi ya Kauli ya Mwenyekiti Wa CCM Taifa Kuwa Demokrasia inamipaka, Hii ndo Mipaka ya Demokrasia kwa CCM pekee Kufanya Maandamano huku Vyama Vingine Vikizuiliwa Kufanya Mikutano ya Hadhara na Maandamano Kama ilivyo kwa CCM

Vitendo Vya kuzuiliwa CHADEMA Tunachukulia kama ni Uvunjwaji Wa makusudi Sheria iliyoanzisha Vyama vya Siasa, ni Uporaji Wa haki za Vyama vyote na Ubaguzi wa waziwazi.
Chadema tunaliona likifanywa na vyombo vya Usalama ili kunusuru anguko kubwa la CCM, zaidi ni hofu ya CCM kuondoka madarakani mapema kwasababu imechokwa na wananchi na inaona njia ya pekee ya kuzuia ukuaji wa Vyama vya Upizani ni Kuzuia vikao vya ndani, Mikutano ya hadhara na maandamano lakini chama CCM wakifanya tena kwa ulinzi wa polisi ambao wanawazuia Chadema na Upinzani Kwa ujumla.

Tunapenda Wananchi Kujua CCM imechokwa, imepoteza Ushawishi tena kwa Wananchi Mkoa Wa Iringa, Maandamano wanayofanya ni kuwahadahaa na kuwaongopea Wananchi kuwa Chama Chao Bado kinaungwa mkono na Wananchi, wakati sio kweli.

Chadema Mkoa wa Iringa Tuna laani Sana upendeleo (Double standards) usiokuwa na aibu unaofanywa na Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa maana tunafahamu kabisa kwamba RPC anajua kinachofanyika Mafinga.

TUNAPENDA Kufahamisha Wananchi Wote waelewe kwamba mwaka 2019 SIKU ZA KUENDELEA KUTII MATAMKO YANAYOKWENDA KINYUME NA SHERIA NA KATIBA YA NCHI ZINAHESABIKA KWA WATAWALA tutapambana kuzidai haki zetu zote tunazonyimwa kinyume na sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama vyama vya siasa vyenye uhalali na vyenye utaratibu uliowekwa rasmi kisheria na kikatiba, tutatangaza rasmi namna na utaratibu wa kufanya mikutano yetu ya hadhara katika kila kona ya MKOA WA IRINGA, hatutaruhusu katazo haramu na lisilo na mashiko ya kisheria litumike kutuzuia kutekeleza wajibu wetu
_
Jackson mnyawami
Katibu CHADEMA
Mkoa Wa_ Iringa
 

wa ukae

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
1,779
2,000
Sasa kama chama kikitishwa kidogo tu wasiandamane nao wananywea wao kila siku ni kulalamika kwa mawazo yao wanafikiri nani atawaonea huruma

Hayo malalamiko ya kulialia kila siku sisi wengine tumeshawachoka na tumeshaanza kuwapuuza
Unataka tukatane mapanga ndio ujue tunadai haki?CDM hakijawahi kuona vurugu kama njia ya kutafuta haki,ila msibweteke sana maana maextremist hujiweka kando na chama na kufanya yao!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

mambio

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
1,255
2,000
Halafu rais kasema demokrasia siyo maandamano ila demokrasia ni kufanya kazi. Sasa labda hao CCM wanafanya kazi barabarani

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo mkiruhusiwa hamjui jinsi yakuongea na wananchi mmejaa mitusi tu, midomo michafu utazani sio waheshimiwa. Siasa kila mtu afanyie jimboni kwake. Ila CCM wanauhalali kwakuwa walishinda Uraisi jimbo la Raisi ni Tz nzima, hawana mipaka.
 

lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,991
2,000
Hivi huyu mzee Pinda amesahau kama aliishia kwenye kamati ya maadili? Ila CCM sijui huwa wanalishwa nini? Huyu mzee sijui dili la nyuki limegoma? Tukisema maisha magumu mnabisha sasa mpka wastaafu wetu wameshindwa kutegemea nyuki wanarudi kulekule waligodanganywa wachukue fomu za kugombea urais!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom