bushman
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,411
- 743
Halafu Mwanakijiji anasema tusimnyoshee kidole polisi wanatekeleza amri ya nani kama sio yake maana yake nini kauli kama hizi?Je hizi ni kauli za kiongozi wa nchi?Kwa ujumla, anafurahia mauaji. Mnakumbuka maelekezo aliyoyatoa kwa makamanda wa vyombo vya ulinzi?
''Mimi nashangaa sana. Eti wananchi wasio na hata na silaha yoyote wanaandamana kwenda kuzingira kituo cha polisi. Na nyie mna silaha, kwa nini hamuwalazi chini? Pale Chato kuna wakati wananchi walizingira kituo cha polisi. Kama ningefika pale, nikakuta watu wamelazwa chini, hata wangekuwemo ndugu zangu, ningempandisha cheo mkuu wa kituo'' -- JPM akiwahutubia makamanda. Kwa hiyo polisi wanaoua wanasubiria kupandishwa vyeo.
Huyu ndiye kiongozi tuliye naye. Ndiye tunayemtegemea, kwa kutumia vyombo alivyo navyo, atulinde sisi sote!!!