Kuna kupenda kwa aina mbili....

Kuna kupenda kwa aina mbili....

Papa Mopao

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2009
Posts
4,166
Reaction score
2,670
Kupenda kwa moyo na kupenda kwa akili.

Kupenda kwa moyo ni kumpenda mtu bila gharama yoyote japo aliye nje ya hapo atakuona unapenda sehemu yenye gharama...mfano, unaweza ukampenda mtu ambaye hana chochote nabukaingia naye kwenye mahusiano naye anakupenda kwa moyo vilevile, kwenye shida na raha ni rahisi kusaidiana kwa mioyo ya hawa wapendanao zinaongea kwa lugha moja.

La pili, kupenda kwa akili, hapa mara nyingi kuna vigezo vingi vimeshawekwa...kwa mfano, umempenda fulani kwasababu ana hela, kazi nzuri, amesoma, ana Masters na kadhalika....sasa katika mahusiano ya namna hii show offs huwa zinaonekana sana mitaani kwamba wao ndo wamefika na wanaenjoy life yao ila kwa ndani unaweza kukimbia ukijua mazingira yao ya maisha.

All in all, kila couple ina unique character tofauti na couple nyingine, hakuna couple moja characters zake zinafanana na couple nyingine, never never

Ila kupenda kwa akili, changamoto ni nyingi....

Wadau mna yapi ya kusema juu ya hili?
 
Amini nakwambia ukiwa na nye:ge unapenda yeyote yule bila kujali. Ngoja zikuishe kama hujaanza kumkimbia.
 
kupenda kwa moyo nimeijaribu hiyo kitu ila unaishia kuwa MTUMWAAAAAAA.
 
muogope sana mwanaume uliyemkuta ana kila kitu siku mkiachana unaondoka na begi lako la nguo tu
Bora huyo niliemkuta ana kila kitu hata nikiondoka roho haiwezi kuuma kuliko niliyetafuta nae baadae azingue. Inauma saaaana. Wanaume ambao hawa kitu wa kuanza nao maisha sitaki hata kuwasikia.
 
Bora huyo niliemkuta ana kila kitu hata nikiondoka roho haiwezi kuuma kuliko niliyetafuta nae baadae azingue. Inauma saaaana. Wanaume ambao hawa kitu wa kuanza nao maisha sitaki hata kuwasikia.
hivi mwanaume ambaye hana kitu yukoje my?
 
Bora huyo niliemkuta ana kila kitu hata nikiondoka roho haiwezi kuuma kuliko niliyetafuta nae baadae azingue. Inauma saaaana. Wanaume ambao hawa kitu wa kuanza nao maisha sitaki hata kuwasikia.
Si wote... after all.. wako wanaojielewa
 
Oenda kwa moyo.. coz ukipenda kwa akili hamta vumiliana hata sikumoja. Lakin kupenda kwa moyo kusiwe sana.. bali na akili itumike
 
Duniani ishavaa min skirt, upende kwa moyo ni shida upende kwa akili ni Shija vile vile,cku tutakapo kubali uhalisia wetu hakika mawadati yataongezeka baina ya mume na mke au wakeze
 
Kupenda nako siku hizi hakueleweki bhana, Mungu anawaona mjue woote mnaoigiza kupenda
 
Back
Top Bottom