Kuna kitu hakipo sawa kwenye matumizi ya MB kwenye simu kwa sasa

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,627
Habarini wakulungwa.

Nadhani wadau mtakuwa m'menotice kuwa hivi sasa simu zetu janja yaani smartphones ni kama zimekuwa na high consumption ya data isivyokawaida.....

Mimi ni mtumiaji wa internet kwenye smartphone tokea 2013. Na kwa miaka yote hii sikuwahi kuexpirience hii hali ya kuona simu inafyonza data... Na hii kitu nimeanza inotice kuanzia mwishoni mwa mwaka jana kuja mwaka huu ila its like inazidi kuwa worse....

Nimejaribu kutazama mitandao ipi inaleta shida ila nimeona ni yote wateja wake wanacomplain especially users wa bundles zilizo chini ya 5000 tsh amount.

Kuna kitu kinaniambia kichwani these guys yaani mitandao ya simu wako under some certain instructions kubana bundles ili sisi raia tusitumie sana katika kushare taarifa au kucheki yanayojiri ukizingatia kwasasa the only source ya valid na sensible information ni kupitia mtandaoni yaani social media na social networks.

Sasa kwa bahati mbaya watz sio wadadisi na kuhoji. Wanaweza jua tatizo then wakalikaushia as if haliwaathiri.

Kwa hali ilivyo sasa mtu unaweza jikuta unatumia hadi 50,000 kwa mwezi kwa hivo hivi vifurushi vya kuunga unga vinavyokatishwa kwa namna hata hazieleweki.

Nachelea kuzilaumu kampuni za simu kwa maana kwa namna wamebadilika ghafla naotea tu watakuwa under some kind of pressure from the government authorities under special and specific instructions.

Hii kitu inatuumiza sisi wengine ambao Issues za politics za tz zinatukera tu maana unakuta mtu kazi zako zina uhusiano sana na matumizi ya internet so kukosa internet ya kueleweka inafanya mambo yanasimama..... Hii kitu inaboa sana.....


Hebu mamlaka husika watambue kuwa internet na matumizi ya internet ni vitu viwili tofauti. Wadeal na matumizi mabaya ya internet na sio kuharibu kabisa internet uses kwa kuweka General restrictions kwa users.
 
Speed ya data imekuwa juu sana Siku hizi, zamani tulizoea YouTube videos zilikuwa zina buffer kwa sekunde kadhaa kabla ya kuanzia kuonekana , Siku hizi ni straight forward , uki click video link , ndani ya sekunde kadhaa imesha download video yote, utakapoamua kutoangalia video hiyo tayari ulishaidownload na unakuwa ushapata hasara ya MB .
Nadhani inatakiwa tubadili mbinu za ku browse internet zenye speed Kali.
 
Umeibua hoja fulani ambao ni dhahiri nami pia ningependa kuweka maoni yangu japo Mimi ukubwa wa matumizi hayo nayaona kwa sababu ya utofauti kidogo.
Kwanza nianze kwa kugusia mizozo inayoendelea duniani nitatolea mfano wa mzozo wa tiktok ili upate mwanga wa kile ninachodhani kisha niendelee na changamoto hiyo kwa hapa nchini. Kutokana na ukuaji wa teknolojia na maboresho ya uundwaji wa software za simu kuna mambo mengi yanaweza kutokea katika simu yako bila ya wewe kuwa na taarifa. Maboresho yameruhusu wetengeneza wa software za simu kupata na kufanya mambo mengi bila wewe kuwa na taarifa wala kufahamu nini kinaendelea, Marekani kwa kutambua hilo imekua ikiwawekea zengwe kubwa ticktock kuwa inafanya michezo ya kuiba taarifa za watumiaji wake bila wao kutambua michezo ambayo imeasisiwa na kurathimishwa kwa kampuni za Marekani.
Kwa uzoefu huu elewa kuwa makampuni kama Facebook na Google wanaservice nyingi ambazo zinafanyakazi kwenye simu yako bila wewe kufungua application yako kwa njia ya kawaida huku zikitumia kifurushi chako Kama kawaida.
Wao wanamalengo na sababu zao lakini kimsingi ndio chanzo hasa cha matumizi makubwa ya internet ambayo tunayashuhudia sasa, sioni muingiliano wa moja kwa moja wa serikali na matumizi hayo ila ni miundo na mifumo ya application za sasa ndio inayochangia matumizi hayo.
Kwa watumiaji wa WiFi ni rahisi zaidi kupata kiwango halisi cha data kilichopita kwenye vijidongo vyao na kuthibitisha hoja yangu hii.
#nimtizamotu
 
yaani mitandao ya simu wako under some certain instructions kubana bundles

mmmh sio kweli kwa kweli

nakazia points zilizonenwa na komredi wawili hapo juu

suala la spidi ya intanet, uboreshwaji toka koo za 2G > 3G >3.5G > 4G, limeathiri sana matumizi ya data ,hakuna tena issue za video buffering ( na kama ipo ni kwa kiasi kiduchu mno) , hapo lazima data iende sana kwa mda mfupi, kama una stream video, video quality inaji auto switch to 720p uko au zaidi, bundle hapo lazima liende kwa kutitirika kama maji kwa mda mfupi ukidhani umeibiwa

tech imekua, rejea mifumo endeshi ya Android mathalan,kuanzia koo ndogo zile za zamani za Jellybean na KitKat na wenzake, sasa tuna izi koo za kisasa, Android 6 kuja juu, zimekua kinara namba moja kwenye ulaji wa data kimyakimya
hii mifumo ya kisasa, wanasema yenyewe ina optimize simu ila ndio majini ya kula data , kuna service kibao za google zinajiendesha nyuma ya pazia kwenye simu bila wewe kujua ( au hata kama unajua huna control nazo )

services/apps kama auto data syncers ,mara software update checker, mara security patch update checker, google analytics, sijui manini uko na zingine ambazo sizijui ( ila simu inazijua )
ambao watu wengi hawana ufaham nao, hawajui ni vitu gani, vinafanya nini, ni majini data yaliyokubuhu,

kwa kumalizia ni kwamba hakuna ISP anaekudhulumu matumizi ya data au kuku restrict kama ulivyodai ( wanavyodai ),
wawezatumia 3rd party application 'data usage manager' ( baadhi ya simu zina built in ya hii ) ku monitor utumiaji wa data, kwa siku, kwa wiki mpaka kwa mwezi ( miezi )
 
Kiufupi speed ya internet ndio inatuponza ! YouTube lukiwa na shallow connection huwa inakbuffer videos katika very low quality, speed ikiwa nzuri utakuta unapata very high quality videos plus crisayl clear sound that's is your data!
 
Speed ya data imekuwa juu sana Siku hizi, zamani tulizoea YouTube videos zilikuwa zina buffer kwa sekunde kadhaa kabla ya kuanzia kuonekana , Siku hizi ni straight forward , uki click video link , ndani ya sekunde kadhaa imesha download video yote, utakapoamua kutoangalia video hiyo tayari ulishaidownload na unakuwa ushapata hasara ya MB .
Nadhani inatakiwa tubadili mbinu za ku browse internet zenye speed Kali.
Kweli kabisa
 
Hii mada Ni nzuri sana
Ni wakati Sasa IT wa Tanzania kufanya mambo ili walao wazungu wasitusababishie hasara za matumizi ya bando bila ridhaa yetu
 
Hawa wanao manage hii mitandao wanaangalia nani mwenye sauti na nani mwenye mamlaka ya kuwafanya wao waogope.

Wakishajua hilo basi watafanya kila namna kupeleka huduma iliyo bora kwa hiyo mamlaka ili kuwapumbaza.

Nyie mkilalamika kwamba mnapewa huduma kwa namna isiyofata haki mtaonekana kama ni waongo kwasababu hiyo mamlaka ikijaribu kuangalia tatizo mnaloliongea kwa upande wake kule halipo
 
Hawa wanao manage hii mitandao wanaangalia nani mwenye sauti na nani mwenye mamlaka ya kuwafanya wao waogope.

Wakishajua hilo basi watafanya kila namna kupeleka huduma iliyo bora kwa hiyo mamlaka ili kuwapumbaza.

Nyie mkilalamika kwamba mnapewa huduma kwa namna isiyofata haki mtaonekana kama ni waongo kwasababu hiyo mamlaka ikijaribu kuangalia tatizo mnaloliongea kwa upande wake kule halipo
Mafala sana. Sijui nijifunze programming nihack nitoe bundles za bure
 
Mafala sana. Sijui nijifunze programming nihack nitoe bundles za bure
Wale ma-IT waliodukua website ya tigo wiki zilizopita walikua wadwanzi tu.

Unadukua website ya tigo halafu unashindwa kutoa free access ya data kwa wananchi wakati lengo lako ni kuwakomoa?
 
Back
Top Bottom