Kuna kesi gani kubwa leo Kisutu?

Kuna kesi gani kubwa leo Kisutu?

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Posts
38,380
Reaction score
88,735
Umepita msafara wa magari kama nane ya Polisi na katikati kuna gari ya magereza wanaelekea kama Kisutu.

Polisi wamevaa ninja wamejifunga vitambaa mdomoni na silaha zao wameelekeza juu kama vile wanajiandaa kwa mapambano. Na hii sio mara ya kwanza kuwaona wamevaa hivyo. Ni sahihi kwa polisi kuvaa hivyo?

Naomba kusema mimi ni muoga sana hasa nikiona silaha na mtu kavaa ninja naona kama chochote kinaweza kutokea. Sijui ni watu wangapi wanaharibikiwa siku wakiona hivyo, ila kwa mimi siku yangu imeharibika kabisa leo.
 
Weka mbali na watoto....
Hapo soln ni kujali kazi yako tu, kapige kazi na potezea yanayoendelea. Hiyo huwa ni alert kuwa wamepewa maagizo ya kumshughurikia vilivyo atakayeingilia shughuri ya kimahakama au kuwagusa targets wao!!!
 
Binafsi sijawahi kuwaogopa Polisi.

Hata waliponikamataga na ka bange tulitia story tu kama washkaji.

Ila sisemi wakuje kuliamsha dude.😀😀😀
Mimi nawaogopa wakiwa na silaha. Hata nikipishana na mtu barabarani ameshika kisu naogopa. Siwaogopi wao wenyewe ila silaha zao na muonekano wao wakati mwingine.
 
Back
Top Bottom