Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,288
Hatua kubwa imechukuliwa na CHADEMA, kwa mwamvuli wa UKAWA, kumkaribisha kubwa la maadui awe miongoni mwao, na hatua hiyo imeshagawanya wafuasi wa chama hicho kifikra.
Wapo walioungana na kauli za kishujaa kuwa "Kwenye Siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu" na "Adui wa adui yako ni Rafiki yako" na wapo ambao wamepinga waziwazi hatua hiyo, wengine wakitishia kujiondoa kushabikia siasa.
Ukweli ni kuwa kubwa la maadui bado ana cheo chake cha jambazi kuu, maana mawaa yaliyomfanya awe na cheo hicho bado anayo na waliompachika mawaa hayo ndio hao anaojiunga nao.
Kama tulivyoona kwenye vyama vingine, kwenye vilabu vya soka na kadhalika kuwa maamuzi makubwa huibua makundi, wapo akina 'Asilia', 'Masilahi' na hata kwenye Klabu ya Simba kuliwahi kuwa na kundi la Mashabiki liliojiia UKAWA kutokana na historia ya wanachama wake.
Tetesi ni kuwa Kubwa la Maadui anakubalika kwa kuwa ana nguvu ya fedha, kwa hiyo maslahi ndiyo yaliyowafanya wamkubali japo kwa taabu. Mjadala wa 'magamba', 'masilahi' na 'asili' ndani ya Chama cha Mapinduzi uliwahi kutokea kipindi cha nyuma, na Kubwa la Maadui alihusika kiasi fulani.
Je, kunaweza kuibuka kundi pinzani ndani ya upinzani ambalo licha ya kutokubaliana na hatua hii linataka kubakia ndani ya chama na Muungano wake? Tufahamu wazi kuwa, licha ya kutokubaliana na viongozi, mwanachama ana haki ya kuendelea kuwa mwanachama na akalindwa na katiba ya chama.
Tunaweza kushuhudia makundi ndani ya CHADEMA au UKAWA kutokana na msimamo huu?