KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 36,577
- 89,222
Nyumbu huitaji maji ili kukata kiu na kama tujuavyo umuhimu wa maji kwa viumbe endapo akiyakosa huweza kufa(hii ni hatari) lakini kwenye maji kuna hatari nyengine ambayo ni mamba.
Sasa ili aweze kuipepuka na hatari ya kwanza inambidi ajiingize kwenye hatari nyengine ili ajiokoe kwenye hatari ya kwanza, hapa wengine hupoteza maisha, hupata ulemavu na wengine hubaki salama.
Hili ni moja kati ya funzo kwa mwanadamu maana hata sisi pia hukutana na hali hii na inakupasa uingie kwenye hatari zaidi ya moja kwa wakati mmoja
wapo wanaoingia katika hali hii lakini hukata tamaa, wengine huogopa, wengine hufeli na wengine hufaulu haya yote ni matokeo.
Kikubwa hapa unapokuwa katika hali hii ni vyema ukatuliza akili yako vyema nakufanya maamuzi sahihi, lakini pia jiandae kwa matokeo yoyote coz we are on the world of action.