Kuna haja yeyote kwa mfanyakazi wa umma kupewa zawadi kama asante yake na mteja?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,521
21,997
Hakuna asiyejuwa kwamba pamoja na madhaifu mbalimbali Kwa watendaji Wa ofisi za umma, wapo ambao kiukweli hujitahidi kuhudumia vizuri kiasi kwamba hadi Mteja mwenyewe unaweza shawishika kutoa chochote kama asante,
Asante hii pamoja na majina mengi iliyopewa kama TAKRIMA,CHAI, MAJI YA KUNYWA n.k Je, ina haja gani kutolewa wakati mtumishi anamshahara wake tayali?
Mnaotoa ASANTE HIZI hamuoni kwamba ndiyo mnaochangia wafanyakazi kuwa wavivu kazini?
Ukitafakari Kwa kina utagundua kwamba hata rushwa huzaliwa Kupitia migongo ya ASANTE tunazowapa hawa wafanyakazi.
Tujiulize kama lengo ni asante, kwanini wasipishe sheria, hata kama WAKUU WA MKOA AU WILAYA watoe tangazo kwamba, Ofisi zote za Umma kuwepo utaratibu Wa kuponi ya maoni, Ili wateja tutoe maoni yetu kuhusu huduma tuliyopatiwa, hii iwe pamoja na pongezi Kwa mfanyakazi unayemuona kakuhudumia vizuri! Ili asante yao waongezewe kwa kupandishiwa mishahara n.k?
AU WEWE MDAU UNAONA KUNA UMHIMU WA KUENDELEA KUTOA ASANTE HIZI?
Maana sisi tuliojaaliwa vitambi tunapapalikiwa sana huko maofini kwasababu wanajuwa mwisho Wa siku kuna ASANTE zao!
Nini maoni yenu wadau!
 
Unataka kutuharibia, tunaopitishwa mlango wa nyuma ! Mi sioni kama kuna tatizo kupeana
 
Ni wajibu wao/wetu kutuhudumia au kuwahudumia wananchi.

Asante ya mdomo naona inatosha,hizo nyingine ndio mashina ya rushwa. Kwamba anayetoa 'asante' next atachangamkiwa sana kwenye huduma,na kinyume chake ni hivyo hivyo.

Asante ya maneno inatosha sana. Ni priceless,kila mmoja anaimudu,wenye 'vitambi' na wasionavyo.
 
Zawadi yoyote unayopewa lazima uhiwasilishe kwa bosi wako wa kazi taratibu ziko hivyo
 
Zawadi inayozidi Tsh. 50,000/= ni Lazima Mtumishi aiwasilishe Ofisni otherwise ni Matumizi Mabaya ya Ofisi.

Rejea ya Mama Tiba kwny Escrow
 
kwa mujibu wa kanuni za kudumu za utumishi umma, mtumishi wa umma akipewa zawadi anatakiwa kutoa taarifa kwa mwajiri wake
 
Back
Top Bottom