Kuna haja ya rais kupokewa na uongozi wote wa nchi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna haja ya rais kupokewa na uongozi wote wa nchi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by paesulta, Mar 19, 2009.

 1. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  http://3.bp.blogspot.com/_HO8ijU76ZcQ/ScJb1lnY7xI/AAAAAAAAl6c/5f0BkuJrKWs/s1600/8D6U2968.jpg
  JK+2.JPG (image)
  JK+2.JPG (image)
  JK+3.JPG (image)

  Ni kitu ambacho sielewi kabisa,je kuna haja kweli ya Rais kila anapokwenda ziarani nje ya nchi na kila anaporudi kupokelewa na uongozi wote wa nchi?kwa sababu gani hasa?maana unaona kuna Waziri Mkuu,Mkuu wa Mjeshi,Mkuu wa Polisi na viongozi wengine kedekede.kwani hawa hawana kazi nyingine ya kufanya?mi nadhani Rais angeweza kabisa kupokelewa na mtu kama Mkuu wa Mkoa,nayo inatosha sana...
  sijui wadau mnaonaje?!:confused:
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,173
  Trophy Points: 280
  Si unajua Tanzania ni nchi ya ki sultani?

  Halafu kila mtu - kuanzia na rais mwenyewe- anajua kuwa watu wengi hawapati promotion on the merit ila kwa kujikomba kwa wakubwa zao?

  Sasa kwa nini kila mtu asitake kujifanya yeye ndiyo hakosi mapokezi.

  Mi nashangaa Kikwete hataki watoto wampe maua lakini hajali kuona cabinet nzima inakwenda kumpokea.
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  kwa kukusaidia tu, pamoja na sababu nyingine za kiprotokali, suala muhimu zaidi ni usalama wa taifa.... we uliza yaliyowatokezea akina Nkurumah,Obote,Gowon n.k walipo safiri nje ya nchi zao wakiwaacha watu wao wa ndani wakiwa vichochoro visivyoeleweka.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Mar 19, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,406
  Trophy Points: 280
  Mimi sioni haja ya raisi kupokewa na yeyote yule. Huko ni kuendekeza u Mungu mtu.
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,173
  Trophy Points: 280
  Usalama gani wa taifa?

  Mi naona kwa kuwepo pale viongozi wengi kwa wakati mmoja ndiyo wanahatarisha usalama, mtu akiwapiga bomu anakuwa kaua serikali nzima.

  Usalama gani unaouongelea wewe?
   
 6. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hiyo picha ya chini
  Hapa ni kama amemuuliza Afande Kova...

  Mh.Raisi: Nipe maendeleo Bw.Kova???
  Afande Kova:[I]Tumefanikiwa kutimua vibaka na wavuta Bhang pale pembeni ya Ikulu...
  [/I]
  (Vicheko kutoka kwa Mwenye UWT,Kova na Mwamnyange...) Ha ha ha haaaaaa Mh.Raisi:Guuud boy!!![/I
   
 7. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo wakikusanyika wote viongozi Rais anafanya roll-call,kujua nani yuko wapi na wala si vichochoroni akipanga kumpindua?!Hakuna swala la usalama wa Taifa wala nini,hay mambo ya umangimeza tu,kutukuzana.
  Kwani viongozi wote hawa kuja Air-port ni gharama vilevile,fikiria misafara yote itakayokuwepo kuwasindikiza,barabara zitafungwakwa muda usio julikana,hivyo wananchi kukosa fursa ya kufanya shughuli zao za kila siku,si ajabu pia ukaambiwa kuwa wanapokea posho maalumu kwa kutayarisha mapokezi ya Rais...
  Sasa kama huu si umangimeza basi ni nini....!:mad:
   
 8. P

  Preacher JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa - halafu utakuta traffic police wanafunga barabara muda mrefu sana - it might huyo kiongozi ndio kwanza anaingia bafuni kuoga - au anakula - huku barabara zishafungwa - yaani kero kweli - kwanza wangeonja FOLENI wajue watu wanavyoteseka kukaa barabarani muda mrefu - LABDA WANGETENGENEZA BARABARA - HIGHWAYS ETC. sio barabara za mwaka 47 ni zilezile - zinawekwa viraka kila siku - na wakitaka kupita - wanapishwa - so they dont feel the pinch - RAISI APOKELEWE NA WATU WACHACHE TU - EXPENSES ZA FUEL, TIME WASTING ZA HAO WANAOMPOKEA NA WALE WACHEZA NGOMA - SIJUI HATA WANAPEWA MAJI YA KUNYWA NA HILI JOTO LA DAR
   
 9. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #9
  Mar 20, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hili swala sio gumu kupata jibu lake,kwanza tujiulize tunaviongozi wangapi?Pili nini wanachokifanya?Matatizo juu ya matatizo kila tatizo inaundwa tume.Kuundwa kwa tume inamanisha ya kua viongozi waliopo katika wizara au taasisi hawakutekeleza kazi zao ipashwavyo kwa maoni yangu ningelikua nakubaliana na tume hizo kama mwisho wake baada ya kugundua mapungufu wahusika wote wanaachia ngazi mara moja.Viongozi wetu hawafanyi kitu chochochote au hawana cha kufanya upataji wa vyeo au kupandishwa hakutegemei matokeo ya kazi zao bali ni nani wakati wote anakua karibu na rais au waziri mkuu n.k.Hiki ndicho chanzo cha wao wakati wote kukimbilia viwanja vya ndege na kuwalamba miguu viongozi wao wa juu>Bado tuna kazi>MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 10. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naona hakuna haja hata ya kumpokea sasa wakishampokea ndio iweje??Mkuu wa mkoa nadhani anatosha sana sio lazima viongozi wengine wawepo!!
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,866
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Au ni utamaduni wa woga wetu sisi Waafrika??

  Hivi maraisi wengine duniani wakiwa nje ya nje wakirudi hupokewa hivi??

  Mfano Bush alikuwa anapokewa na nani??

  In short overheads za viongozi ni kubwa mno ..na mzigo mkubwa mno kwa watu wa nchi maskini kama Tz!
   
 12. A

  Audax JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hiyo ni buget inaandaliwa kuwa watu wanaenda kumuaga president,mafuta,magari na mengineyo na goma kama wadau walivyosema,wakati tatizo likitokea hawaamui wanajifanya kuunda tume,tume nyingine hata implimentation ya majibu hamna,na wala hatusomewi ilifanya nini,iliyosoma taarifa ndo hadi leo watu wanawaandama sasa pesa yetu sisi walipa kodi inakuwa ilishaliwa. Hizi safari wangekuwa wanpangiana zamu,ijayo anaenda mkuu wa mkoa kuaga,itayofuatia saidi mwema,nyingine mwamnyange na kuendelea,sasa wote kwa sababu ni yeye aliyewateua basi lazima wawepo maana president akiamua anaweza ku reshufle ukakuta huna chako kisa hukwenda kumuaga.
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Mar 20, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,562
  Likes Received: 3,858
  Trophy Points: 280
  Hawana lolote, hata wenyewe hawapendi, lakini si unajua tena kujikomba!!
   
 14. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ulimbukeni wote huo!
   
 16. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naomba kukuuliza,

  unaporudi kutoka safari familia yako haikupokei
   
 17. j

  jimba Member

  #17
  Mar 25, 2009
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Labda tujiulize rizki zetu tutazipataje kama hajujamtumikia aliye juu? Ukijitahidi kuwa karibu na jiko utaambulia hata kuonja mchuzi kabla ya kuwekwa binzari. Kwa kuwa mheshimiwa yuko bize na wageni kila mara ikulu jamaa zetu wanajitahidi kutafuta appointment kinguvu kwani wanajua wakianzia airport msafara utaishia Ikulu tu na ndipo hapo watawakilisha matatizo yao.:oops:
   
 18. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nadhani rafiki yangu unalinganisha mambo ambyo hayalingani kabisa.familia yangu ikija kunipokea hawafungi barabara kwa zaidi ya saa moja,wala pesa ya watanzania walipa kodi haitumiki.Wanakuja kunipokea na tunapanda daladala yetu kurudi nyumbani.
  Tunaongelea swala kubwa hapa.Mwenzangu kwa jinsi ulivyoongea unakua kama unataka kumaanisha kuwa Rais ni kama baba wa familia na viongozi wengine wa serikali ni watoto wake or labda ndugu,lakini si hivyo,at leat sivyo inavyotakiwa kuwa.
  Nadhani kama utafuatilia zaidi maoni ya wadau hapo juu basi utaona kuwa tatizo letu ni kubwa zaidi.Kama umewahi kukutwa katika foleni ukiwa katikati ya mji,hasa maeneo ya posta ya zamani,kwa sababu barabara imefungwa kupishamsafara wa kiongozi fulani,basi utapata hasa nini kinachoongelewa hapa.kwa kumbukumbu yangu mara nyingi barabara inafungwa hata zaidi ya saa moja na nusu,nahiyo ni kwa msafara wakiongozi mmoja.Sasa fikiria kwa misafara ya viongozi wote hawa itafungwa kwa muda gani..!?Niambie ukutwe ndani ya daladala kwa masaa mawili ndo inakuwaje hapo.Huu ni mfano mmoja tu wa adha ya hili sala tunalolijadili...
  Nawakilisha
   
Loading...