Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,340
120,866
Wanabodi,

Preamble: Mimi ni mwana fasihi, hapa nimetumia tamathali za semi, kwa kubakwa kwa demokrasia, na sio kubakwa kule kwa wale wenye mawazo machafu!.

Hii ni thread ya swali!, "Jee Kubakwa na Kutulia Sio Kuridhia?!, Na Baada ya Kuridhia, Kuna Haja tena ya Kuhofia Kubakwa tena na tena na kuendelea kubwakwa?!.

Siku zinasonga, sarakasi za hatma ya Zanzibar zinaendelea!. Leo tumenyimwa hulua ya MCC!, who knows kesho tutanyimwa nini?!.

Kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar halikuwa ombi, wala sio ushauri, kesema watu watajadili, ile ni amri, japo ni amri batili kwa sababu haikuandamana na ufafanuzi wowote wa kifungu chochote cha sheria, amri ile, mimi naiita ni amri ya ubakaji wa demokrasia!, amri ikiishatolewa inafuatiwa na utekelezaji tuu na sio mjadala au majadiliano!. Kitendo cha amri ile ya ubakwaji wa demokrasia, kwa kufutwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar, kutekelezwa moja kwa moja bila pingamizi lolote!, mimi nakuita huku ni kuridhia ubakwaji, ule!. Hivyo Wazanzibari wameridhia wenyewe kwa ridhaa zao kubakwa!.

zenji-3.jpg


Tangazo la amri ile ya kufuta uchaguzi, liliandamana na amri ya haja ya kurudia uchaguzi, ila kwa vile amri ya kurudia uchaguzi ilitanguliwa na uwepo wa haja, ya kuurudia uchaguzi huo, iwapo Wazanzibari wenyewe ndio walioridhia kubakwa kwa demokrasia, wakiona hakuna haja, then sio lazima uchaguzi huo urudiwe!, na kuiachia CCM iendelee tuu kutawala kwa kubaka demokrasia kama inavyoendelea sasa, ambapo hapa ni mbakaji na mbakwaji wote wameridhia na kukubaliana kuendelea kuishi pamoja kama wanavyoishi sasa, wataokoa fedha nyingi zitakazopotea kwenye uchaguzi wa marudio.

Kwa vile Jecha ameufuta uchaguzi kwa "uwezo alionao yeye Jecha!", kitendo cha hakuna yoyote aliyepinga rasmi tangazo hilo, zaidi ya kupiga kelele tuu kama kelele za mlango, au zile za chura kisimani, tafsiri yangu ni kuwa Wanzanzibari wote katika umoja wao, wameikubali amri hiyo ya Jecha, bila ya pingamizi lolote rasmi!, hivyo ni kweli Jecha anao uwezo huo mkubwa kweli kweli aliouonyesha wa kufuta matokeo halali ya uchaguzi halali,huru na wa haki, bila kutumia kifungu chochote cha sheria, taratibu na kanuni na Wazanzibari wote wameridhika na amri hiyo, na wametulia tuu ndio maana hakuna yoyote aliyeipinga amri hiyo popote mpaka sasa!, huku ndiko mimi nikakokuita kubakwa kwa demokrasia, na aliyebakwa katulia tuli, kajinyamazia kimya bila kupinga kwa kushitaki popote!, jee huku sio kuridhia?!, kama umebakwa ukaridhia na kuendelea kuishi na mbakaji kwa ridhaa yahoo!, does it make any sense kuendelea kupiga kelele za kuogopa kubakwa tena na tena?!.

Sasa kama Wanzanzibari katika umoja wao, wameikubali amri hiyo batili ya Jecha, jee hiki kigugumizi cha kurudiwa uchaguzi wa Zanzibar ni cha nini?!. Kama kufutwa kwa uchaguzi ni amri batili na imetekelezwa, ili batili iwe batili ni lazima ibatilishwe, Batili isipo batilishwa hugeuka halali. Hivyo amri batili ya Jecha ya kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar pia ni amri batili iliyohalishwa na kutobatilishwa na kinachofuatia ni utekelezaji tuu hiyo amri batili na sio mjadala!, hizi kelele za Zanzibar ni za nini wakati hakuna yeyote aliyechukua hatua yoyote kuzuia ubakaji?!.

Naomba kufafanua, kuna kitu kinachoitwa amri, ni one thing, na uhalali wa amri husika is another thing!, inapotolewa amri ambayo sio amri halali, ilipaswa isitekelezwa kwa kupingwa rasmi kwa kutumia sheria, taratibu na kanuni, lakini kwa vile mpaka sasa hakuna pingamizi lolote hadi leo, kisheria hii inaitwa kuridhia by default!.

Hata sheria ndoa inasema ndoa halali hufungwa kwa ridhaa ya wanandoa husika, ndoa ikifungwa bila ridhaa, haiwi ndoa batili, bali ni ndoa batilifu!, yaani void na voidable mariages!. Hata ikitokea, watu wakachukuana na kuishi kinyumba bila kufungwa kwa ndoa yoyote rasmi, ule tuu utekelezaji wa majukuma ya ndoa, kunawafanya wanandoa hao kuhesabika wanaishi kwenye "dhana ya ndoa", yaani "presumption of marriage", na inahesabika kuwa ndoa halali na wanandoa husika wote wameridhia yaani "consent", hivyo kuihalalisha hiyo ndoa yao mbele ya sheria!.

Kubaka ni kosa la jina!, na likifanyika kwa mtoto wa chini ya umri wa miaka 14, hata akiridhia, huo utahesabika ni ubakaji!, lakini ukimbaka binti mwenye umri zaidi ya miaka 15, na kumgeuza ni mkeo, binti huyo, asipolalamika au kupeleka mashitaka popote, atahesabika kuwa ameridhia ubakaji ule!.

Kwa Tanzania, umri wa mtu mzima (age of the majority or legal age) ni kuanzia miaka 18, sasa ikitokea binti wa miaka 18, amebakwa, akajinyamazia kimya, akaendelea kuishi na mbakaji maisha ya kinyumba, na akatimiza majukumu yake ya kindoa, kisheria, atahesabika binti yule ameiridhia na mahusiano hayo yatahesabika kama ni wanandoa halali hadi pale mmoja au wote watakapoamua kubatilisha au kuhalilisha kwa vyeti.

Kitendo kilichofanywa na Jecha, ni ubakaji mkubwa kabisa wa wazi wa demokasia kuwahi kutokea katika sehemu moja ya JMT, umefanyika mchana kweupe mbele ya Watanzania na jumuiya ya kimataifa ikishuhudia, lakini kwa vile wapiga kura wote wana umri wa zaidi ya miaka 18, watu wote waliofanyiwa ubakaji huu, ni watu wazima na akili zao timamu!, kitendo cha wote hawa kubakwa, wakaishia kupiga tuu kelele kuwa "tumebakwa, tumebakwa". lakini hakuna yoyote aliyechukua hatua yoyote kuupinga rasmi ubakwaji huo, wala kupeleka mashitaka popote kuhusu ubakwaji huo, huku wakiendelea kuhudumiwa ma mbakaji huyo, na kutimiza majukumu yao ya kisiasa na wabakaji hao, tafsiri ya hali hii kisheria ni kuwa Wanzanzibari katika umoja wao, wameridhia kubakwa huku kwa ridhaa zao wenyewe!.

Swali la kujiuliza ni kuwa kama ni kweli CUF ilishinda kihalali, lakini demokrasia ikabakwa, na wao CUF kuukubali ubakwaji huu na kuridhia kwa kutokufanya lolote, jee sasa CUF inaogopa nini kuendelea kutekeleza masharti ya mbakaji huyo, kwa sababu, kama walishinda, hata uchaguzi ukirudiwa mara 100, si ni bado CUF itashinda?!, sasa hiki kigugumizi cha nini?!.

Kama, CUF imeshinda kihalali lakini ushindi huo ukabakwa!, kwa nini mpaka sasa haijachukua hatua zozote rasmi kupinga ubakwaji huu?!. Hivi inakuwaje kweli baada ya kubakwa, mbakaji na mbakwaji, wanakaa chini meza kunegotiate jinsi ya kuendelea na maisha ya unyumba yaliotokana na ubakaji?!.

Nauliza tena, Zanzibar! Jee Kubakwa na Kutulia Sio Kuridhia?!, Jee Kuna Haja Ya Kuhofia Kurudiwa Uchaguzi?!, kama umeweza kubakwa na ukatulia tuu, ili mbakaji akubake vizuri, hata uchaguzi ukirudiwa una wasiwasi gani?!, kama ni kweli ulishinda, ukabakwa na ukatulia, hata ukirudiwa utashinda tena, hata ukishinda na demokrasia ikabakwa tena, si utakuwa umeisha zowea kubakwa?. Mtu akiishazowea kubakwa anaweza tena kuhofia kuendelea kubakwa ili hali ni yeye mwwnyewe ameridhia kubakwa?!
Ni swali tuu!.

Jumapili Njema!.

Paskali.




 
Pasco Tatizo sio kurudia na kushinda Tatizo ni kuwa CCM hawako Tayari kushindwa. Ni kweli Uchaguzi leo CUF Watashinda bila ya shida . Lakini katika mazingira Gani ? Ya tume ile ile ambayo imevurunda kusimamia na kukiri kuwa ilishindwa na uchaguzi haukua huru. Kukiri tu huku wakati Vyama na Serikali imepoteza fedha nyingi kujiandaa uchaguzi ule.

Hili Peke hili la ZEC na Jecha kwa msemo wa sasa ni JIPU

Kwanza kabla ya kurudiwa hili jipu halina budi Kupasuliwa wao ndio walowafikisha wa znz hapo. Sheria ya Tume ni kwamba Hakuna wa kuwalazimisha kuachia madaraka, watakaa mpaka muda wao umalize sasa kwa vile CCM wao ndo walo shika bango la kuwa uchaguzi umeharibiwa ingekuwa vyema wakatangaza kuwa hawana imani na tume ya uchaguzi kwa kushindwa kusimamia uchaguzi sawa sawa.

CCM waishinikize Tume ijuuzulu, baada ya hapa ni kuchagua Mpya, na kwa bahati nzuri sheria na katiba ya Zanzibar inaruhusu kuchagua Mkuu wa Tume kutoka kwa Jaji yoyote kutoka Jumuia ya Madola. Hivyo Rais aliemaliza muda wake Shein achague Mwenyekiti Kutoka nchi za Jumuia ya Madola katiba inamruhusu. Hili ni kwa nia njema kabisa.

Pili kwa mazingira ya sasa ya vikosi vya CCM vya Zombies kuachiwa kuendesha mateso na kutisha watu lipigwe stop na jukumu lote la ulinzi lichukuliwe na JWTZ Bila ya upendeleo. na kazi yao iwe kulinda amani. jeshi la polisi pia halifai limekua likitumiwa na CCM . Pia returning officers wote watoke Jumuia ya EA .

waangalizi wa nje waruhusiwe kwa wingi kusimamia uchaguzi
 
Last edited by a moderator:
Kuna gazeti moja la leo limeripoti katika ukurasa wake wa mbele kuwa mawaziri wa CUF wamerudisha "Maprado" ya serikali. Nikajiuliza siku zote hizi walikuwa wanakaa nayo ya nini?

Back to the topic,Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) haiwezi kufikishwa Mahakamini kama sikosei.
 
Kwa fasihi zenu uko , kubakwa ukatulia inaweza kuwa kiridhia ila kwenye mivitabu vya sheria kutulia au kuzimia vyoyote vile hakuna kubakwa kwa kuridhia! Stahili zooote , kubakwa na kubakwa tu!
 
Kuna gazeti moja la leo limeripoti katika ukurasa wake wa mbele kuwa mawaziri wa CUF wamerudisha "Maprado" ya serikali. Nikajiuliza siku zote hizi walikuwa wanakaa nayo ya nini?

Back to the topic,Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) haiwezi kufikishwa Mahakamini kama sikosei.

Aliyefuta uchaguzi wa Zanzibar ni ZEC au ni Jecha?!. Mambo yote ya serikali yanafanywa kwa kufuata taatibu, shria na kanuni, na zote hizi ziko kwenye maandishi!, Jecha alipofuta uchaguzi ule, alitumia mamlaka yapi?, sheia ipi?, kanuni zipi?, na taratibu zipi?!, Jecha hakuwa na mamlaka yale, wala hakutumia sheria taratibu na kanuni yoyote ila Wazanzibar wamemkubalia!, ukimshamkubalia mbakaji, umekubali kubakwa, jee utakuwa na sababu ya kuogopa kurudia tena kwa sababu unaweza ukabakwa tena?!, kama ulibakwa hukulalamika popote, jee kuna chochote kitakachomfanya mbakaji aogope kubaka tena?!.

Wengi wanautafasiri mgogoro wa Zanzibar kama ni wa kisiasa, hivyo unahitaji suluhisho la kisiasa!, in reality, mgogoro wa Zanzibar sio wa kisiasa, ni ni wa kisheria, taratibu na kanuni, na suluhisho lake ni la kisheria, taratibu na kanuni!.

Pasco
 
Pasco Tatizo sio kurudia na kushinda Tatizo ni kuwa CCM hawako Tayari kushindwa. Ni kweli Uchaguzi leo CUF Watashinda bila ya shida . Lakini katika mazingira Gani ? Ya tume ile ile ambayo imevurunda kusimamia na kukiri kuwa ilishindwa na uchaguzi haukua huru. Kukiri tu huku wakati Vyama na Serikali imepoteza fedha nyingi kujiandaa uchaguzi ule.
Mkuu, ujue tangu kufutwa kwa matokeo ya Zanzibar, hakuna aliyelalamika!. Huku ni kukubali hata kama ni kwa shingo upande!, there is no any official records kwa yoyote aiiyelalamika!

Pasco.
 
Aliyefuta uchaguzi wa Zanzibar ni ZEC au ni Jecha?!. Mambo yote ya serikali yanafanywa kwa kufuata taatibu, shria na kanuni, na zote hizi ziko kwenye maandishi!, Jecha alipofuta uchaguzi ule, alitumia mamlaka yapi?, sheia ipi?, kanuni zipi?, na taratibu zipi?!, Jecha hakuwa na mamlaka yale, wala hakutumia sheria taratibu na kanuni yoyote ila Wazanzibar wamemkubalia!, ukimshamkubalia mbakaji, umekubali kubakwa, jee utakuwa na sababu ya kuogopa kurudia tena kwa sababu unaweza ukabakwa tena?!, kama ulibakwa hukulalamika popote, jee kuna chochote kitakachomfanya mbakaji aogope kubaka tena?!.

Wengi wanautafasiri mgogoro wa Zanzibar kama ni wa kisiasa, hivyo unahitaji suluhisho la kisiasa!, in reality, mgogoro wa Zanzibar sio wa kisiasa, ni ni wa kisheria, taratibu na kanuni, na suluhisho lake ni la kisheria, taratibu na kanuni!.

Pasco
Pasco nchii hii huijui?

Kama kwenye Bunge la Katiba watu walipiga kura mpaka kwa email,leo unashangaa nini kuhusu Jecha na ZEC?

Nchii hii kila kitu kinawezekana bwana hata kwa goli la mkono ikibidi.
 
Last edited by a moderator:
Unajuaada mzur sana lkn nikweli.km cuf walishinda kihalai je ukirudiwa wanaweza kushinda tena hlo ndo swali lako..? Watashinda ndio lkn watatokea vchogo kutoka tanganyika chungumzma kuja zanzibar kupga kura sasa hapo kweli cuf inaweza kushinda tena..? Hayo ni mawazo yangu tuu maana nlkua naputa tuu
 
Kwa fasihi zenu uko , kubakwa ukatulia inaweza kuwa kiridhia ila kwenye mivitabu vya sheria kutulia au kuzimia vyoyote vile hakuna kubakwa kwa kuridhia! Stahili zooote , kubakwa na kubakwa tu!
Hata kwenye sheria, kubakwa ya kubakwa tuu, ni kwa minors, under 14!. Lakini jitu zima likibakwa na kuamua kujimanyazia tuu kuepuka aibu, huko kunahesabika ni kuridhia, na hakuna kesi!. Jee kwenye huo ubakaji wa Zanzibar, kuna yeyote aliyelalamika?!, achana na haya makelele ya kutwa kucha, jee kuna malalamiko rasmi?!, huko ndiko kuridhia kwenyewe!, kama watu wameridhia kufutwa kwa matokeo na wamekaa kimya!, what is the basis kususia kurugiwa kwa uchaguzi?!.

Pasco
 
Unajuaada mzur sana lkn nikweli.km cuf walishinda kihalai je ukirudiwa wanaweza kushinda tena hlo ndo swali lako..? Watashinda ndio lkn watatokea vchogo kutoka tanganyika chungumzma kuja zanzibar kupga kura sasa hapo kweli cuf inaweza kushinda tena..? Hayo ni mawazo yangu tuu maana nlkua naputa tuu

Hili la kuitana machogo, sisi wengine halitusumbui sana, mke umuoe mwenyewe, umlishe, umvishe, na umpe kila kitu, lakini kama ni mwanamke mwenye ghubu, haeshi kulalamika!, kama unapenda kwa dhati, ghubu lake utalizoea na kuendelea tuu na maisha as long as anatimiza majukumu yake ya kindoa!. Masimango tumeyazoweya, tunaendelea kuwahudumia umeme bure, mishahara bure, jeshi bure, polisi bure, fedha bure, mambo ya nje bure, na asilimia 4.5% ya misaada yote kutoka nje!.

Kipenda roho hula nyama mbichi, tumependa, tunaendelea kupenda na tunatunza licha ya masimango!.

Pasco
 
kuna njia nyingi za kutatua migogoro PASCO! CUF wamechagua diplomasia kwa sasa! pia upo bara ni business as usual.Zanzibar wanategemea utalii.watalii hawaji mahotel yako tupu .watu.hawana kazi.inflation ipojuu.ulitaka kuwa na vita kama ya Burundi? kuwa na huruma kwa wapemba waliozungukwa na nguvu ya dola ya CCM.mbona huku bara EL kachakachuliwa na tumetulia?hujasikia ya meya TANGA au UBUNGE mbagala?unataka vita tu!
 
Mtoa mada sijaona hoja yako ipo wapi dhidi ya kukuona unaruruka tu na hoja za ubakaji,kiufupi jecha(ccm)ndiyo iliyobakwa kupitia sanduku la kura tarehe 25,huku kwetu tunauita mtarimbo umewaganda na hawana vya kuupapatua na ukitaka uthibisho wa kubakwa kwa madalali wenu ni kule kwa maalim seif kuyapata matokeo yote ya uchaguzi na kuyaweka hadharani.
 
Linapokuja suala la kuijua siasa Tanzania basi wazanzibar wa CUF wao ni walimu na ndio maana wamekuwa wakigain something kila unapofanyika uchaguzi mkuu Zanzibar! Na ndio maana mara nyingi hutumia akili kuliko kukurupuka.

Sasa kitendo alichokifanya Jecha cha kufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa October 25 2015 kwa kila mwenye akili basi anajua kitendo cha Jecha kimewaumiza zaidi CCM kuliko CUF!! Na ndio maana kila siku inayoingia wanawatowa watu tofauti tofauti kukisemea na kujaribu kukipa uhalali kitendo cha Jecha.

Ni CCM ndio walioilalamikia tume ya uchaguzi ili kukipa uhalali kitendo cha Jecha sasa tujiulize kama tume ya uchaguzi ilishindwa kufanya majukumu yake jee itapataje sifa ya kusimamia uchaguzi wa marudio!!!??? Ikiwa wao CCM wameipa kasoro tele jee CUF wao wataiamini!!??

Nina uahakika CUF wako tayari kuingia katika uchaguzi wa marudio pale ambapo washindani wenzao (CCM) watakapokuwa tayari tume ya kimataifa ndio ije isimame huo uchaguzi marudio!! Hili likifanyika litapunguza mateso na shida wanazopata wazanzibar kila unapofanyika uchaguzi mkuu!!! Nikawaida kwa wazanzibar kila uchaguzi mkuu unapofanyika Zanzibar basi nilazima uache watu wakiwa majaraha ya risasi, marungu, kuibiwa na kuharibiwa mali zao na wakati mwengine vifo.

Mwisho ni kuwa wazanzibar mara hii wako kimya hivi ni kwasababu viongozi wao wamewataka watulie huku wao wakionesha ni nini maana ya uongozi!! Hawako kimya kwa kuwa ni WAOGA! Hiyo siyo sifa ya wazanzibar wa CUF na watawala wanalijua hili na ndio maana sijambo la ajabu KABLA, WAKATI NA BAADA YAUCHAGUZI kuona jukumu la ulinzi wanakabidhiwa jeshi kutoka mikononi mwa polisi!!?? Pia sijambo la ajabu katika kipindi hicho kuona vikundi vya kiharamia vilivyofunika uso kupiga na kutesa watu hasa UNGUJA maana kwa upande wa PEMBA wao wanaitumia vyema SERA YA JINO KWA JINO "WAULIZE WALIOKUWA WANAENEZA VINYESI KILICHOWAPATA KATIKA KIJIJI CHA SHENGEJUU PEMBA" hadi hii leo hawajathubutu kurudia tena uchafu wao.

Mwisho ni kuwa kila mwenye akili ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania anajua ni chama gani kimeshinda matokeo ya uraisi Zanzibar hivyo CCM wanajitekenya na kucheka wenyewe maana mara hii MTARIMBO UMEWAGANDA hivyo hawana namna zaidi kuikabidhi CUF ushindi wake!! Vyenginevyo tutarajie mengine makubwa zaidi ya MCC ya marekani.
 
Mkuu, ujue tangu kufutwa kwa matokeo ya Zanzibar, hakuna aliyelalamika!. Huku ni kukubali hata kama ni kwa shingo upande!, there is no any official records kwa yoyote aiiyelalamika!

Pasco.

Wewe Pasco pale ulipokuwa ukishindikiza siasa za CCM hukuwa ukitamba na nguvu za dola zilioko mikononi mwa CCM wewe? Usiwe mpotevu wa faham wewe, unataka wakashtaki mahakama ya nani na kwa sheria gani? Katiba zote mbili haziruhusu ku despute the presidential polls mahakamani wala kuishitaki tume mahakamani. Hii ilikiwa ni mpango wa mikakati iliyowekwa tayari kuwanyima haki wananchi.
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Preamble: Mimi ni mwana fasihi, hapa nimetumia tamathali za semi, kwa kubakwa kwa demokrasia, na sio kubajwa kule kwa wale wenye mawazo machafu!.

Hii ni thread ya swali!, "Jee Kubakwa na Kutulia Sio Kuridhia?!, Na Baada ya Kuridhia, Kuna Haja tena ya Kuhofia Kubakwa kuendelea kubwakwa?!.

Siku zinasonga, sarakasi za hatma ya Zanzibar zinaendelea!. Leo tumenyimwa hulua ya MCC!, who knows kesho tutanyimwa nini?!.

Pasco

Umeandika vizuri tu fasihi yako.

Mimi naomba unisaidie kumjua mbakaji.

Huyu mbakaji unayemzungumzia ni nani? Je ni Jecha?

Na amembaka nani ?

Kama ni Jecha, je Jecha amebaka kama Jecha au kama Taasisi?

Kama Jecha ni mbakaji wa demokrasia kwa nini analindwa na taasisi na vitengo?

Je mbakaji ametenda kosa la kubaka kwa utashi wake tu au ana washirika?

Kama Jecha ana wasaidizi waliomshawishi au kumsaidia kubaka, je nao ni wabakaji?

Umemalizia fasihi yako kwa kulalamika kuwa tumenyimwa halua ya MCC. Kwa nini sisi tulionyimwa halua hatumchukulii hatua yoyote mbakaji?

Je na sisi tumeridhia na kukubali kunyimwa halua?

Je na sisi kwa kuridhia kunyimwa halua ni kuridhia pia kuwa ni accomplice wa mbakaji wa demokrasia/wabakaji wa demokrasia?

Je mbakaji amewabaka wapigakura na waliowapigia kura?

Kwa hiyo mbakaji amewabaka CCM, CUF na wasiokuwa na vyama?

Na wote hawa wameridhia kwa kukaa kimya, huku mbakaji akijipanga ili aendelee kuwabaka?

Mbakaji ni nani? Pasco mtaje hadharani ili kila mtu, kila binadamu, kila kiumbe apate kumjua. Sema kweli , msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Mtaje mbakaji ili mtumbua majipu apate kazi ya kumshughulikia. Tumepata mtumbua majipu ambaye naamini akioneshwa jipu(mbakaji) hatafanya unafiki, atafanya kweli na atatenda kweli. Atalitumbua jipu. Au unafikiri mtumbua majipu naye anaridhia kunyimwa halua?

Ubakaji umefanyika wapi? Nchi ipi?

Kwa nini tunalaumu waliobakwa na tunamsahau mbakaji?

Mbakaji wa demokrasia ni nani Tanzania?

Ajabu ya Tanzania na watanzania utaiona pale wanapomhukumu kibaka mtaani lakini hawaoneshi kukerwa na mbakaji wa demokrasia, pia ni wazuri katika kulalamikia kukosa halua.

Tanzania ni nchi ya wadanganyika.
 
Msilo lijua mablo Maalimu seifu this time anaonekana kulingamua ni kuwa, CCM shida yao ilikuw amachafuko yatokee na fasterfatser waitishe uchaguzi under machafuko ili wafanye fujo na mgombea wao ashinde wamekuw awkaifanya hivi mara nyingi na miaka yote kwa maana ya kuwachokoza CUF na wanachokozeka.

This time hakuna aliye fanya fujo na watu wote kimyaa wansubiri uchaguzi urudiwe na nauwakika kw aamzingira yaamani bila fujo polisi na majeshi, hata wakirudia usiku w amanane mara 1000, CCM lazima wapigwe tu.

So Pasco kaa ukujua utulivu unaoendelea ni wmiba mkubw akwa CCM, wao wantamani zitokee fujo ili wafanye yao.
 
Last edited by a moderator:
Pasco nchii hii huijui?

Kama kwenye Bunge la Katiba watu walipiga kura mpaka kwa email,leo unashangaa nini kuhusu Jecha na ZEC?

Nchii hii kila kitu kinawezekana bwana hata kwa goli la mkono ikibidi.

Unafikiri haijui?

Wewe hujui Pasco alimtabiri mtumbua majipu kuwa atasimikwa ugombea na uraisi?

Anaijua vizuri? Anachokoza fikra mbadala tu, ili wale wasioona wapate kuona na wagonjwa wapate kuponywa na wanafiki wapate kuadhirika.

Pasco pia anaelewa, ikitokea mtu, chama au taasisi kwenda mahakamani kufungua kesi, madai, mbakaji ndio atakuwa amepata ile kitu anapenda, "suala hili halipasi kuzungumziwa tena kwa sababu liko mahakamani".

Au hujui maana ya "jambo hili liko mahakamani na kuliiibua tena au kulizungumzia unaingilia uhuru wa mahakama"?

Mbakaji atakuwa amepata mwanya wa kuendelea kubaka kwa raha zake. Kwa aliyebakwa atapata maumivu mara mbili. Muda unayoyoma, ukifungua macho miezi 2 imepita, mwaka umepita na msimu mpya wa uchaguzi umefika na bado suala, shauri liko mahakamani. Mahakama ya nyani kwa ajili ya kumhukumu ngedere, mahakama ya mamba kwa ajili ya kumhukumu kenge.

Kwa sasa kama hali ilivyo ni afadhali, mbakaji pia inamlazimu ajitokeze hadharani yeye mwenyewe kujitetea na kujaribu kuushawishi umma kuwa kwa amani ya nchi yetu(kung'angania madaraka), alilazimika abake au unaona wawakilishi wake wanajitokeza na kuvamia media kuimba "uchaguzi urudiwe, na mbakwaji asiwe na woga wala wasiwasi" haki itatendeka.

Kukoseshwa halua sio ngoma ya kitoto, watoto watakufa njaa.
Hata mbakaji hataki watoto wake wafe njaa na kutembeza bakuli itakuwa ni kazi ngumu.

Uongo hata ukirudiwa mara milioni au bilioni hautabadilika na kuwa ukweli, wako wataoamini uongo kwa kuimbwa sana kuwa ni ukweli lakini uhalisia ni kuwa uongo utabaki kuwa ni uongo.

Ni msema kweli tu ndiye mpenzi wa Mungu! Na ukweli unajulikana.
 
Naona wengi hamkumfahamu PASCO huyu jamaa amekuja na hoja kuwa ikiwa Tanzania imenyimwa msaada na MCC kwanini uchaguzi usifanyike ili Misaada ipatikane. Aliebakwa sio Zanzibar pekeyake hata Tanzania nayo imebakwa na wanaotoa misaada ndio maada ukaja na huu msemo wako wa kubakwa.

Ukienda KEKO kuna nyapala huonea wafungwa nae nyapala huonewa na afisa wa Magereza. ndio maisha yalivyo kaka Pasco
 
Back
Top Bottom