Mtini
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 1,491
- 2,355
Shule nyingi nchini haziko kwenye mazingira ya kuridhisha, baadhi hazin madawati, madarasa ya kutosha, walimu wa kutosha pamoja na vitendea kazi vya kutosha. Hali hii hupelekea wanafunzi wengi kufanya vibaya na hata wengine kumaliza elimu ya msingi bila kujua kusoma na kuandika. Majuzi juzi waziri wa elimu katoa agizo kwamba walimu wakuu ambao wanafunzi watafika darasa la tatu bila kujua KKK watafukuzwa kazi, hivi kweli katika mazingira ya shule zetu kama hizi (pichani) watajua KKK kweli au ni kumuonea tu mwalimu mkuu?
Mi kwa ushauri wangu naona kabla ya mwalimu mkuu kufukuzwa, Mkuu wa mkoa, wilaya na mkurugenzi katika maeneo zenye shule kama hizi wafukuzwe kazi maana wameshindwa kusimamia maendeleo ya wananchi
Mi kwa ushauri wangu naona kabla ya mwalimu mkuu kufukuzwa, Mkuu wa mkoa, wilaya na mkurugenzi katika maeneo zenye shule kama hizi wafukuzwe kazi maana wameshindwa kusimamia maendeleo ya wananchi