Kuna haja gani mahakama kutoa hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa mshtakiwa wakati Rais akipelekewa form aisaini ili wanyongwe anakataa?

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
19,142
2,000
Hukumu ya kunyongwa hadi kufa inapotolewa na mahakama kwa mshakiwa kama mnavyojua kwa mujibu ya sheria Rais anatakiwa kusaini ili hukumu ya kunyonga itimie ,je!kama mahakam hiyo inatoa hukumu alafu mhusika wa mwisho anakataa sasa kuna haja gani ya mahakama kutoa hukumu hiyo ya kunyongwa,kama ni hivyo ni bora katiba kifungu cha kunyongwa hadi kufa kwa mshtakiwa anapokutwa na kosa hilo kifutwe kutafutwe sheria nyingine ya hukumu inayoendana na kosa.
 
Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
3,337
2,000
Sheria haisemi kwamba Rais atatia saini fomu za wahukumiwa wa kunyongwa (hadi kufa); sheria inasema kwamba baada ya kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa, adhabu hiyo itatekelezwa baada ya Rais kutia sahihi yake.

Kwa hiyo hukumu ya adhabu ya kifo haihusiani hata kidogo na uamuzi wa Rais kutia saini au kutofanya hivyo. Muhimu zaidi, sheria haitaji muda ambao Rais anapaswa kusaini utekelezwaji wa adhabu hiyo.
 
Sasa mbona Rais huwa anatamba jukwaani anasem kuwa ameletewa majina kwenye karatasi asaini ili wakanyongwe na anasisitiza kuwa kakataa na kaelekeza hukumu nyingine hii imekaaje sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
50thebe

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,688
2,000
Hukumu ya kunyongwa hadi kufa inapotolewa na mahakama kwa mshakiwa kama mnavyojua kwa mujibu ya sheria Rais anatakiwa kusaini ili hukumu ya kunyonga itimie ,je!kama mahakam hiyo inatoa hukumu alafu mhusika wa mwisho anakataa sasa kuna haja gani ya mahakama kutoa hukumu hiyo ya kunyongwa,kama ni hivyo ni bora katiba kifungu cha kunyongwa hadi kufa kwa mshtakiwa anapokutwa na kosa hilo kifutwe kutafutwe sheria nyingine ya hukumu inayoendana na kosa.
Hukumu ya kunyongwa inatekelezwa kwa ridhaa ya Rais. Ndio Sheria zetu zinavyosema! Yeye Rais ndio mtu wa mwisho ku-approve ama ku-decline maamuzi ya Mahakama.

Ikimpendeza Rais, akatengua maamuzi ya mahakama haina maana sheria hii haitufai.
 
wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
19,142
2,000
Hukumu ya kunyongwa inatekelezwa kwa ridhaa ya Rais. Ndio Sheria zetu zinavyosema! Yeye Rais ndio mtu wa mwisho ku-approve ama ku-decline maamuzi ya Mahakama.

Ikimpendeza Rais, akatengua maamuzi ya mahakama haina maana sheria hii haitufai.
Ndio maana namaanisha kama inaendana na maamuzi ya Rais basi kwenye hukumu ingefutwa itafutwe namna ingine ya hukumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
50thebe

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,688
2,000
Ndio maana namaanisha kama inaendana na maamuzi ya Rais basi kwenye hukumu ingefutwa itafutwe namna ingine ya hukumu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu

Design ya hii sheria inampa fursa mkosaji kuwa na Imani kwamba hata kama mahakama itaamuru anyongwe mpaka kufa, bado anayo nafasi ya maamuzi yale kutenguliwa.

Kwa maoni yangu design hii ni nzuri sana! Maana imejengwa kwa msingi wa IMANI /Faith ambayo ndio dhana inayoongoza kila kitu around mwanadamu!

Ima Imani iwe potofu ama kinyume chake bado ni Imani mchango wake kwenye Maisha haumithiliki.
 
iam Lucha

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
1,744
2,000
Hiyo hukm ipo kisheria na vitanzi kila siku vinafanyiwa marekebisho, siku akiingia Rais alievurugwa akisain tu watu wanavalishwa vitanzi.

Na ambao wako jela kwa hukum hiyo kule ndan ya jela wana jela yao nyingne , wanataman hat knyongwa maana jins wanavyoish kwa waswas had baadh wameanza kuwa kama vichaa na ni hatar kuwachanganya na wengne

Mungu atunusuru na jela
 
Noma sana
 
Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
3,337
2,000
Sasa mbona Rais huwa anatamba jukwaani anasem kuwa ameletewa majina kwenye karatasi asaini ili wakanyongwe na anasisitiza kuwa kakataa na kaelekeza hukumu nyingine hii imekaaje sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo unataka Rais wetu mpendwa ashangilie watu kufa, regardless ni wahalifu??? Ukisikia JPM anasema hivyo, maana yake ni kuwa asingependa kabisa kuona hilo likiwatokea watu, hasa raia ambao yeye ni President wao. Kumbuka kwamba adhabu kubwa zaidi kuliko zote, kwa kosa lisilostahili kuvumiliwa, kufumbiwa macho na kuhafifishwa, ni KUMSAMEHE MKOSAJI. Najua kulielewa hili siyo leo wala keshokutwa.
 
Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
3,337
2,000
Hapana mkuu

Design ya hii sheria inampa fursa mkosaji kuwa na Imani kwamba hata kama mahakama itaamuru anyongwe mpaka kufa, bado anayo nafasi ya maamuzi yale kutenguliwa.

Kwa maoni yangu design hii ni nzuri sana! Maana imejengwa kwa msingi wa IMANI /Faith ambayo ndio dhana inayoongoza kila kitu around mwanadamu!

Ima Imani iwe potofu ama kinyume chake bado ni Imani mchango wake kwenye Maisha haumithiliki.
Hii ni nzuri sana nimeipenda!!! Imagine baada ya kukaa huko gerezani appeal ikaonesha hana hatia!!! Anatolewa gerezani. Ila akinyongwa maana yake ni kwamba ndiyo hivyo tena
 
Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
3,337
2,000
Hukumu ya kunyongwa inatekelezwa kwa ridhaa ya Rais. Ndio Sheria zetu zinavyosema! Yeye Rais ndio mtu wa mwisho ku-approve ama ku-decline maamuzi ya Mahakama.

Ikimpendeza Rais, akatengua maamuzi ya mahakama haina maana sheria hii haitufai.
Yes ndiyo sheria hiyo
 
wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
19,142
2,000
Kwa hiyo unataka Rais wetu mpendwa ashangilie watu kufa, regardless ni wahalifu??? Ukisikia JPM anasema hivyo, maana yake ni kuwa asingependa kabisa kuona hilo likiwatokea watu, hasa raia ambao yeye ni President wao. Kumbuka kwamba adhabu kubwa zaidi kuliko zote, kwa kosa lisilostahili kuvumiliwa, kufumbiwa macho na kuhafifishwa, ni KUMSAMEHE MKOSAJI. Najua kulielewa hili siyo leo wala keshokutwa.
Kwa hiyo unataka kuaminisha umma kuwa Rais hawezi toa amri ya kuua na wala hajawahi toa hiyo amri mtu auliwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,327
2,000
Tena hii ni adhabu kali sana ya kisaikolojia, pale unapokuwa huna uhakika wa lini utanyongwa
Hiyo nayo ina "faida" zake kwani husaidia kupunguza matukio kama hayo mtu akikumbuka adhabu ya kosa analotarajia kulifanya anaweza kughairi zoezi.

Ila kama adhabu ingekuwa nyepesi si ajabu makosa ya aina hiyo kuongezeka.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom